Kudos chadema !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kudos chadema !!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nguruvi3, Sep 9, 2010.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  source: Tanzania Daima

  na Mwandishi wetu, Meatu

  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe hafanyi jambo lolote kwa kukurupuka.
  Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Meatu mkoani Shinyanga, kuhusiana na tuhuma kadhaa zinazoelekezwa kwake.
  Mgombea huyo ambaye alipata mapokezi makubwa alipowasili mjini hapa kwa kutumia helikopta yake iliyotengemaa baada ya kupata hitilafu siku chache zilizopita, alisema Kikwete na vigogo wenzake ndani ya CCM wanaweweseka kutokana na mwamko unaoonyeshwa na Watanzania kuiunga mkono CHADEMA tangu kuanza kwa kampeni hizo na ndiyo maana wamekuwa wakimzushia kashfa mbalimbali.
  "Sasa hivi nasikia wameenda kuwatafuta watu wasioona ili waseme nilipokuwa kiongozi wao nilitafuna fedha, mwanzoni walisema nimetumwa na kuungwa mkono na Kanisa Katoliki, hivi sasa wamenifungulia kesi kudai sh bil. moja. Kwa kawaida sifanyi jambo kwa kukurupuka, tutakutana huko huko mahakamani," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliofurika kumsikiliza.
  Alisema anashangazwa na ahadi nyingi zinazotolewa na mgombea huyo wa CCM ikiwamo ya kutaka kujenga viwanja vya ndege, wakati serikali yake haina hata ndege moja baada ya kuuawa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC).
  "Lakini hata kama kungekuwa na ndege, Watanzania wa Wilaya ya Meatu mtapanda hiyo ndege kusafirisha ng'ombe wenu sokoni? Kina mama wajawazito watapanda ndege hizo kwenda kupata matibabu? Ndiyo maana huwa nasema Kikwete si makini, kwa nini hizo pesa asizitumie kujenga zahanati, kununua magari ya wagonjwa na kujenga barabara?" alihoji Dk. Slaa.
  Akisikilizwa kwa makini na wananchi hao, Dk. Slaa alitaja ahadi nyingine aliyoiita kuwa ni ya ununuzi wa baiskeli za miguu mitatu 400 (Bajaj) kwa ajili ya kina mama wajawazito.
  "Leo wakati nakuja, nilikuwa napitia kumbukumbu za Bunge lililomalizika, nikaona ahadi hiyo ya Kikwete ya kununua Bajaj, ilikuwa kwenye kumbukumbu za Bunge wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma, leo miaka minne baadaye anatoa ahadi hiyo hiyo. Sijui kama Rais Kikwete huwa anasoma, hiyo ahadi alishaitoa na leo anaitoa tena kwenu," alisema Dk. Slaa.
  Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya kuwasaidia kina mama wajawazito, alipaswa kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri ambao kila mmoja ana shangingi la sh mil. 200, sawa na kujenga zahanati nne ili fedha hizo zitumike kununulia magari ya wagonjwa. "Kabla sijapanda hii helikopta yangu, nilifanya mikutano kadhaa njiani na wakati nakuja, nilishuhudia mikokoteni mitano ya kuvutwa na punda na nyingine ng'ombe, ikitumika kuwabeba wagonjwa kuwapeleka hospitalini, lakini Kikwete anaahidi Bajaj 400 ambazo hata njia za kupita hazipo kutokana na uchakavu, huo ni mzaha kwa Watanzania, safari hii msimchague, chagueni CHADEMA," alisema.

  Akizungumzia tatizo la elimu nchini, Dk. Slaa alisema taifa liko kwenye msiba kubwa wa umaskini uliotokana na ukosefu wa elimu.
  Alisema licha ya serikali ya CCM kutamba na ujenzi wa shule za kata, matokeo ya mitihani ya shule hizo ni mabaya na elimu inayotolewa haiwasaidii vijana wanaomaliza masomo yao kutokana na ukosefu wa walimu, maabara na vifaa vingine katika shule hizo.
  "Hapa Meatu, takwimu za serikali ni hizi hapa, zinasema kuwa wilaya yenu ilikuwa na wanafunzi 8,461, waliofaulu walikuwa 1,962 na waliobaki takriban 6,000 wametupwa mitaani. Hii ndiyo sera ya CCM inayojivunia ya Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya, sasa wamekuwa na Nguvu Zaidi," alisema Dk. Slaa.
  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, CHADEMA ikiingia madarakani itahakikisha elimu ya awali kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha sita itakuwa bure, afya itatolewa bure huku akisisitiza kuwa itafuta kodi ya vifaa vyote vya ujenzi ili kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.
  "Wapo wanaohoji tutapata wapi pesa, sisi tunasema fedha zipo, tatizo CCM haina vipa umbele. Kwenye suala la kufuta vifaa vya ujenzi, tutaangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwa viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi ili mabati, nondo, sementi, misumari, rangi na vingine vipatikane kwa bei ya chini," alisisitiza.
  Kabla ya mkutano huo, Dk. Slaa alifanya mikutano ya kampeni katika Kata ya Kidarafa, Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida na Bukundi, Wilaya ya Meatu, ambapo aliwaomba wananchi kuipigia kura CHADEMA kwa ajili ya kubadili hali zao za maisha. Kwa upande wake, mgombea mwenza wa CHADEMA, Mzee Said Mzee, aliwataka wananchi wa maeneo hayo kutokubali kuuza shahada zao za kupigia kura na kuacha kufanywa mabango ya CCM kwa kuvaa fulana zenye picha ya Kikwete. "Msikubali kuuza shahada zenu kwa sh 5,000 au kwa kanga, fulana na kofia yenye picha ya Kikwete. Tunawaambia kabisa kwamba mwaka 2010 hatudanganyiki," alisema Mzee.

  I hope you will find the above post useful. Finally Chadema is trying to position itself in the ongoing campaign. The campaign is all about how the party is connecting to voters.The manifesto of election should serve as a compass to what the party is in for. Always, it is a technical document which needs erudites to contemplate; therefore the candidate should focus and narrow it to answer the basic wananchi's concern.
  In this context, I would urge Chadema to discuss issues retrospectively and then propound the vision. Majority of wananchi in rural area would not be interested to hear the complex mathematics of revenue collections, rather will be enticed to hear their own stories as regarding to health,education and water supply, as well as how much of their revenue have been embezzled. These are core issues which affect a wide cross section of our population.
  Chadema, the silver bullet is; address the concern of intended population, remind them on empty promises for the past 5 and 50 years, outline your strategy with specifics and let them compare the notes. In your narratives you can chip in some burning issues of national interest to put the ''opponent'' on defensive, while electrifying your audience.
  However depending on the audience, still the Manifesto has a room for discussion where scholars are approached.
  Kudos Chadema
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Jamani Slaa si apewe uwaziri tuu jamaa ni makini
   
Loading...