Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,723
- 9,189
Unaweza kunipa mfano wa kudeka kwa mtu aliye mbali na mtu au watu wanaomdekeza?
Unaweza kunipa mfano au mifano ya mtu anayejitegemea na ambaye anadeka?
Nakushukuru kwa michango yako.
MTU WA MBALI:
mfano ni mtu ambaye haiishi siku bila kupiga siku kulalamikia (kwa anayemdekea) mazingira anayoishi na watu hata kama mazingira sio mabaya kihivyo.
Hiyo ni kwa sababu kuna mambo anayakosa kutoka kwa mdekezaji wake.
Kama umepitia maisha ya hosteli utaelewa hapa. Tena wengine hadi wanalia.
Kila jambo kwao ni baya pengine kwa sababu linafanywa tofauti na alivyozoeshwa.
WANAOJITEGEMEA:
mfano ni wale ambao kila likizo ya kazi lazima aende kwao (kama anadekezwa na mzazi) pia wapo tayari kuomba viruhusa au hata kuacha shughuli zao warudi kwao au kama ameoa hupenda kuishi na wazazi wake pia.
NB: Katika hiyo mifano inawezekana pia wakawa wanafanya hvyo kwa sababu zingine na sio kudeka.