Kudanganywa Ajira Mwanza: Natures Way

Kudanganywa Ajira Mwanza: Natures Way

Mimi mkazi wa Tabora. Naomba kuwasilisha taarifa kuhusu mfumo unaotumia ahadi za ajira kuwavutia vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda Mwanza kwa maelezo ambayo hayatoi ukweli kamili wa shughuli zinazofanyika.

Mimi binafsi nilielekezwa kuwa kuna nafasi za kazi ya kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini. Kutokana na maelezo hayo, nilisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza kwa matumaini ya kupata ajira ya kawaida.

Baada ya kufika Mwanza, nilitakiwa kufanya malipo mbalimbali yaliyoelezwa kuwa ni sehemu ya mchakato wa ajira. Malipo hayo yalihusisha:

• Kodi ya makazi ya miezi mitatu
• Ada ya semina
• Ada ya usajili/form
• Gharama za chakula

Jumla ya fedha nilizolipa ni Tsh 167,000.

Shughuli hizi nimezikuta zikifanyika katika kampuni linalojiita Natures Way (Empowered Consumerism), lililopo maeneo ya Mlango Mmoja, Mwanza.

Baada ya kuanza kushiriki kwenye shughuli hizo, niligundua kuwa hakukuwa na ajira ya kawaida kama nilivyoelekezwa kabla ya kuondoka Tabora. Badala yake, shughuli inayofanyika ni mfumo wa Network Marketing, tofauti kabisa na maelezo ya awali niliyopewa kuhusu ajira.

Kutokana na hali hiyo, nimeona nimepotezewa muda pamoja na fedha zangu kwa kupewa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu kazi niliyokuwa naenda kufanya. Hadi sasa, baada ya kugundua ukweli huo, nimesitisha kushiriki kwenye semina hizo.

Aidha, kutokana na kujitoa kwenye mfumo huo, kwa sasa wanataka kuniondoa katika eneo nililolipia makazi ya miezi mitatu, huku nikiwa sina uwezo wa kupata nauli ya kurudi Tabora.

Nina wasiwasi kuwa bado kuna vijana wengi wanaendelea kuvutwa kwa ahadi kama hizo za ajira, kisha kuombwa kulipa fedha mbalimbali wakiamini wanaenda kuajiriwa.

Naomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa suala hili pamoja na kusaidia kupata ufumbuzi wa hali ninayopitia, ili kuzuia vijana wengine kuendelea kuathirika kwa namna hii.
Utapeli ni biashara halali kabisa Tanzania.

Pole boss
 
Uvivu wa kufanya kazi na kujitaftia kijana anataka akitoka kumtegemea baba ake akamtegemee muajiri yeye mwenyewe hawezi kuishi kwa kujitegemea

Hivyo vitu mtaji ni mdogo sana unakuta huyo anaelalamika ajira anatumia simu ya 500k na makolokolo kibao getoni, tv sabufa kitanda kikubwa godoro inch10 lakin mtaji wa 300k au 200k hana
Kweli hapo hata mimi nakuunga mkono! Mtu ambaye hawezi kujishusha kufanya kazi ya laki 3 hata miezi 6 ili akusanye kimtaji kidogo hmm! Hapo sijui tumsaidieje aisee..!
 
Aachane na kutafuta ajira ajiajiri kwa biashara yoyote ile astick nayo hakuna anaezaliwa mfanyabiashara au mfanyakazi yote tunafanya kujifunza
 
Mimi mkazi wa Tabora. Naomba kuwasilisha taarifa kuhusu mfumo unaotumia ahadi za ajira kuwavutia vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda Mwanza kwa maelezo ambayo hayatoi ukweli kamili wa shughuli zinazofanyika.

Mimi binafsi nilielekezwa kuwa kuna nafasi za kazi ya kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini. Kutokana na maelezo hayo, nilisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza kwa matumaini ya kupata ajira ya kawaida.

Baada ya kufika Mwanza, nilitakiwa kufanya malipo mbalimbali yaliyoelezwa kuwa ni sehemu ya mchakato wa ajira. Malipo hayo yalihusisha:

• Kodi ya makazi ya miezi mitatu
• Ada ya semina
• Ada ya usajili/form
• Gharama za chakula

Jumla ya fedha nilizolipa ni Tsh 167,000.

Shughuli hizi nimezikuta zikifanyika katika kampuni linalojiita Natures Way (Empowered Consumerism), lililopo maeneo ya Mlango Mmoja, Mwanza.

Baada ya kuanza kushiriki kwenye shughuli hizo, niligundua kuwa hakukuwa na ajira ya kawaida kama nilivyoelekezwa kabla ya kuondoka Tabora. Badala yake, shughuli inayofanyika ni mfumo wa Network Marketing, tofauti kabisa na maelezo ya awali niliyopewa kuhusu ajira.

Kutokana na hali hiyo, nimeona nimepotezewa muda pamoja na fedha zangu kwa kupewa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu kazi niliyokuwa naenda kufanya. Hadi sasa, baada ya kugundua ukweli huo, nimesitisha kushiriki kwenye semina hizo.

Aidha, kutokana na kujitoa kwenye mfumo huo, kwa sasa wanataka kuniondoa katika eneo nililolipia makazi ya miezi mitatu, huku nikiwa sina uwezo wa kupata nauli ya kurudi Tabora.

Nina wasiwasi kuwa bado kuna vijana wengi wanaendelea kuvutwa kwa ahadi kama hizo za ajira, kisha kuombwa kulipa fedha mbalimbali wakiamini wanaenda kuajiriwa.

Naomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa suala hili pamoja na kusaidia kupata ufumbuzi wa hali ninayopitia, ili kuzuia vijana wengine kuendelea kuathirika kwa namna hii.
Pole sana mkuu.
Japo vijana wangu wa Tabora mnaniabisha sana Wallah why kila siku nyinyi kwa matukio yasiyoisha mara kalyinda mara Qnet lakini bado hamjifunzi.
Mnaniangusha wanyamwezi wenzangu
 
Mimi mkazi wa Tabora. Naomba kuwasilisha taarifa kuhusu mfumo unaotumia ahadi za ajira kuwavutia vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda Mwanza kwa maelezo ambayo hayatoi ukweli kamili wa shughuli zinazofanyika.

Mimi binafsi nilielekezwa kuwa kuna nafasi za kazi ya kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini. Kutokana na maelezo hayo, nilisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza kwa matumaini ya kupata ajira ya kawaida.

Baada ya kufika Mwanza, nilitakiwa kufanya malipo mbalimbali yaliyoelezwa kuwa ni sehemu ya mchakato wa ajira. Malipo hayo yalihusisha:

• Kodi ya makazi ya miezi mitatu
• Ada ya semina
• Ada ya usajili/form
• Gharama za chakula

Jumla ya fedha nilizolipa ni Tsh 167,000.

Shughuli hizi nimezikuta zikifanyika katika kampuni linalojiita Natures Way (Empowered Consumerism), lililopo maeneo ya Mlango Mmoja, Mwanza.

Baada ya kuanza kushiriki kwenye shughuli hizo, niligundua kuwa hakukuwa na ajira ya kawaida kama nilivyoelekezwa kabla ya kuondoka Tabora. Badala yake, shughuli inayofanyika ni mfumo wa Network Marketing, tofauti kabisa na maelezo ya awali niliyopewa kuhusu ajira.

Kutokana na hali hiyo, nimeona nimepotezewa muda pamoja na fedha zangu kwa kupewa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu kazi niliyokuwa naenda kufanya. Hadi sasa, baada ya kugundua ukweli huo, nimesitisha kushiriki kwenye semina hizo.

Aidha, kutokana na kujitoa kwenye mfumo huo, kwa sasa wanataka kuniondoa katika eneo nililolipia makazi ya miezi mitatu, huku nikiwa sina uwezo wa kupata nauli ya kurudi Tabora.

Nina wasiwasi kuwa bado kuna vijana wengi wanaendelea kuvutwa kwa ahadi kama hizo za ajira, kisha kuombwa kulipa fedha mbalimbali wakiamini wanaenda kuajiriwa.

Naomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa suala hili pamoja na kusaidia kupata ufumbuzi wa hali ninayopitia, ili kuzuia vijana wengine kuendelea kuathirika kwa namna hii.
Kwenye nchi hii ya Malawi kuna viongozi wamebariki haya kufanyika maana kila siku yanatokea wanakamatwa wanarudi tena kivingine.

Inshort now kuna msemo mmoja wa KiGENZ tunasema
"Ukiona unatafutwa kupewa fursa ,jua wewe ndiyo fursa yenyewe"
KAA KIJANJA
 
Uvivu wa kufanya kazi na kujitaftia kijana anataka akitoka kumtegemea baba ake akamtegemee muajiri yeye mwenyewe hawezi kuishi kwa kujitegemea

Hivyo vitu mtaji ni mdogo sana unakuta huyo anaelalamika ajira anatumia simu ya 500k na makolokolo kibao getoni, tv sabufa kitanda kikubwa godoro inch10 lakin mtaji wa 300k au 200k hana

Kwahiyo mtu unataka auze vitu geto akaanzishe baishara gani? Mbona huwa mnaongea vitu haviendani?

Uuze godoro,kitanda na simu uanzishe biashara hiyo ni kupiga hatua au kurudi nyuma. Mnavyoongelea biashara ni kama sehemu ya kwenda tu nakuchukua pesa,kitu ambacho sijawahi kubaliana nacho.

Ukiwa unahivyo vitu vya msingi ndani ukanzisha biashara ni rahisi kupiga hatua zaidi ya kuviuza ili uanzishe biashara.

Biashara zina pande mbili,kufeli na kufaulu. Na hizi biashara ndogo ndiyo zenye aslimia kubwa ya kufeli kuliko kubwa. Biashara ya laki/ milioni ni biashara ambazo hata matumizi yako ya kawaida haziwezi yatosheleza.
 
Dogo polee,inaonekana we si mtu wa kufanyia jambo research kabla ujafanya maamuzi,fanyaa hivi neenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya au mkoaa,then muulezee utasaidiakaa mno saidi mtanda ni msikivu
 
Kwahiyo mtu unataka auze vitu geto akaanzishe baishara gani? Mbona huwa mnaongea vitu haviendani?

Uuze godoro,kitanda na simu uanzishe biashara hiyo ni kupiga hatua au kurudi nyuma. Mnavyoongelea biashara ni kama sehemu ya kwenda tu nakuchukua pesa,kitu ambacho sijawahi kubaliana nacho.

Ukiwa unahivyo vitu vya msingi ndani ukanzisha biashara ni rahisi kupiga hatua zaidi ya kuviuza ili uanzishe biashara.

Biashara zina pande mbili,kufeli na kufaulu. Na hizi biashara ndogo ndiyo zenye aslimia kubwa ya kufeli kuliko kubwa. Biashara ya laki/ milioni ni biashara ambazo hata matumizi yako ya kawaida haziwezi yatosheleza.
Pesa za kununulia ivo vitu kaitoa wapi hadi akose mtaji wa 300k? Kumbuka hapa nilikuwa namjibu Seran alikuwa anasema mtaji ni tatizo kwa vijana wengi ndio nikatolea huo mfano
 
Back
Top Bottom