Makene
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 1,475
- 282
Taarifa za kukamatwa raia kuhusiana na kuchomwa kwa ofisi ya kamanda wa polisi ni uonevu na matumizi mabaya ya nguvu za dola.
Haingii akilini kusikia eti ofisi ya kamanda imechomwa moto.
Mbona hatusikii ni hatua gani zimechukuliwa kwanza dhidi ya askari waliopaswa kuwa lindo. Hii ni aibu kwamba ofisi ya wanaodai kulinda raia haina ulinzi. Raia waliokamatwa wanafanyiwa uonevu kwa udhembe wa askari wetu wachovu wasio na kazi.
Hata baadhi ya raia wamehama makazi yao kuhofia masaibu yatakayowakuta.
Isitoshe maelezo ya raia yanaonyesha kuna askari waliofanya uporaji vibanda vya raia na bila shaka ndio waliochoma moto huo.
Je tulitegemee jeshi la polisi kwa ulinzi wa mali zetu sisi raia?