Kuchanganya rangi: Ndoa zake hazidumu

Kuchanganya rangi: Ndoa zake hazidumu

mkuu ndoa wala haina formula sikuhizi hata same color ni kimbembe,tena afadhali hizo tangi tofauti inaweza ikawa ya muda mfupi lakini ukaenjoy kuliko hizi za same color muda mrefu ila wa mateso mno
Ni kama aina fulani ya hallucination au fashion fulani kupenda kuolewa au kuoa au kuoana na mtu wa taifa fulani hasa wazungu atu wengi hasa kinadada wanawazimia mno wazungu nk ili tu kupata half cast, yaani kwa mfano mpare na mzungu au Mchina au Mchaga mfilipino.

Mwanzoni mwa mapenzi motomoto na hata kufikia ndoa na kwa wengine mpaka watoto ni vigumu kugundua tofauti au kuona mapungufu lakini kadiri siku zinavyosonga
mgongano wa kimtazamo katika mila desturi utamaduni na mazoea hujitokeza taratibu na hatimaye kujenga nyufa ambazo hazizibiki na mwishoni kuishia kwenye talaka, kutengana au kupigana vibuti vya moja kwa moja.

Uasili, mila na desturi ni kigezo kisichopewa kipaumbele kwenye mahusiano yanayomaanisha ndoa, watu huongozwa na mihemko ya mapenzi zaidi hasa kwenye kigezo cha cash umaarufu na uzuri lakini kikubwa zaidi rangi ndoa nyingi zilizochanyanganya rangi kitaifa na kimataifa hazikudumu.

Wewe kama unatoka kishimundu mtafute mkishimundu mwenzako ukienda mbali sana mtafute mgweno maana wote mnakula ndizi kwa style yenu, kama uko kwenye mchakato wa ndoa pita hapa utaokota chochote.
 
ni vema ukaowa mtu mwenye similar background ili kipndoa hzo challenges. bcs apart from mke/mume unaunganisha ukoo mzima unatakiwa uutendee mema ukoo wako .Ndio maana mara nying wazee wanatushaur tuoe wanawake wa makabila yetu.
 
Mbona una ukabila sana we we.halafu utakuwa mchagga
 
Unaweza kua ushauri mzuri, tatizo hao wenzetu tunawapatia wapi maana maisha yanaenda Kasi sana na huku tunakoishi na kufanya kazi tuko multicultural so mpk kumpata wa kwetu kwetu ni kazi sana
 
Ndege wafananao daima huruka pamoja....ni vigumu sana kuishi na mtu mliotafautiana mitazamo mingi ya msingi hasa hasa ya kimila na desturi....hata mimi nimewahi kushuhudia mara nyingi ndoa za hivyo zikivunjika.....
Na ukiona imedumu NYINGI mmoja wa wanandoa anaamua/mazingira yanamlazimu kuwa mtumwa/zoba.
 
Na ukiona imedumu NYINGI mmoja wa wanandoa anaamua/mazingira yanamlazimu kuwa mtumwa/zoba.
Hebu angalia tu ndoa za wazungu na wabongo au wachina na wabongo kwa miaka 15 tu iliyopita hapa Tanzania kama kuna zilizo hai hazifiki tano, hasa za wachina hakuna hata moja
 
Back
Top Bottom