Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,585
- 4,270
Wakati nikiwa mdogo kulikuwa na kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi Kigamboni (Kama sijakosea). Nafikiri Mwalimu Nyerere alijua kuwa tukinunua mafuta ghafi, bei itakuwa nafuu sana lakini pia tutabakiwa na end products nyingine kama lami nk ambazo tunazihitaji sana, lakini bado kuna faida za kukuza Ajira nk.
Nafikiri kuna umuhimu wa kufufua hiki kiwanda au pengine kuanzisha Kipya kama kile kimekuwa chakavu. Nasema hivyo nikijua kuwa, hivi karibuni Uganda itaanza kuzalisha mafuta ghafi kwa kiasi kikubwa tu; kwa nini tusitumie hiyo fursa kuchakata hayo mafuta na kuyauza hapa ndani na East Africa hata kama sio yote yanayo baki ndio yakaenda ughaibuni?
Naona kama ni fursa ya wazi wazi.