Uchaguzi 2020 Kuchaguliwa kwa Tundu Lissu kupeperusha bendera ya CHADEMA ni kukiua chama

Gerald, hivi umeshindwa kweli kuona jaribio la jana la kutaka kulipotezea tukio la Tundu Lissu kuchaguliwa kuwa mpeperusha bendera wa CDM, na bado inashindikana. Licha ya vyombo vingi vya habari kukwepa kwa makusudi kuupa Mkutano Mkuu uliomchagua, na hata pia matokeo ktk uchaguzi yalionyesha kutopewa umuhimu wake.

Je! Iliweza kuona "reaction" ya watu mitaani? Watu wengi walipata matokeo kupitia mitandao ya kijamii, huku wakionyesha kufurahishwa na matokeo hayo waliyokuwa wakiyasubiri kwa hamu kubwa. Mkuu, natambua ulichokiandika hata wewe mwenyewe hukiamini, pengine ni katika kutaka kuonekana na watu fulani. Hivi kwa akili ya kawaida tu huwezi kuona licha ya jitihada zote za kuwajaza watu hofu na hata kutaka kuzuia shamrashamra za kumlaki Tundu Lissu aliporejea hapa nchini, na pia licha ya taifa kuwa ktk kipindi cha maombolezo ya kitaifa ya kifo cha Mzee Mkapa, bado watu wengi pamoja na kuwa na hofu ya kukabiliana na vyombo vya dola, bado walipata ujasiri wa kumlaki na kumpokea mpendwa wao.
 
Alie soma naomba summary, lissu, zitto, mbowe siasa ndo maisha yao ndo kazi zao hawana kazi nyingine mjini
 

Ujenzi wa Chama una madaraja mawili, 1) kukijenga chama ama kimeanzishwa au baada ya kupata dhoruba. Baada ya uchaguzi kama tutashindwa uchaguzi huu, Majibu ya mapigo kwetu yatapigwa kwa kipimo ambacho hatutoweza kuhimili tena kama Chama.

Wasi wasi ni kuwa, kuna wanao iangalia Chadema kwa jicho la karibu, lakini tunalazimika kuangalia na jicho la kesho ili tuchukue tahadhali sambamba na mahitaji ya kisiasa ya kesho ili kesho yetu isije ikaleta majuto ndani yake ambayo marekebisho yakawa taabu..
 
Hizo siyo agenda, kwa sababu, TASAF zipo shughuli zinaendelea, watumishi wanapanda madaraja, korosho wamelipwa baada ya kujua hila za wapiga dili, ajira zipo na isitoshe kwa awamu ya tano ya viwand sekta binafsi imeajiri kwa wingi. Meli mpya ni ajira, ndege zimetengeneza ajira, tren dsm moshi, tanga moshi ni ajira. Think big
 
acha habari za kuungaunga. unabore.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…