Uchaguzi 2020 Kuchaguliwa kwa Tundu Lissu kupeperusha bendera ya CHADEMA ni kukiua chama

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,496
1,796
Kampeni za chama zimeisha na tayari chama kimempata mgombea ambaye ni Tundu Lissu. Tunampeleka kwenye mkutano mkuu na naamini atapata baraka za mkutano mkuu.

KAZI ZINAZO FUATA NI KUMUUZA MGOMBEA NCHI NZIMA

Mgombea wetu amaleta msisimko mkubwa kwa wanachama wa Chadema na hasa wajumbe. Hali hii kwa wanachama inaeleweka Lissu ni shujaa lakini kwa wananchi wa Tanzania bado yapo maswali wanampokea kama shujaa ama kama msaliti?

Wakuu kila mtu anaweza kutoa maoni yake na akawa sawasawa kwa muono wake, lakini siasa ina takiwa kuwa na uchambuzi ambao hauna macho ila unajua ukweli tuu, na kwa kufanya hivi ndio chama kitabaki salama.

SWALI: Je, Tundu Antipas Lissu ndio Chadema, yaani Lissu ndio chama?

JIBU : Hapana ila Lissu ni mmoja ya wanachama wanaogombea kupeperusha Bendera ya Urais wa Tanzania kupitia Chadema.

SWALI: Je, Lissu akishindwa katika Uchaguzi mkuu kupata Urais wa Tanzania kwa hiyo Chama cha Chadema kife?

JIBU: Hapana cham lazima kiendelee na ndio ilivyo vyama vingi Duniani.

SWALI: Katika kila kinyag'anyiro cha Uongozi wote wanaoshindwa wanaondoka kwenye chama?

JIBU: Hapana ila uchaguzi wowote ule lazima utengeneze makundi ili kutengeneza ngome ya Ushindi.

SWALI: Je, uchaguzi huu unaweza kuwa tofauti na chauzi zingine zilizo pita na hata mifano ya nchi nyingine?

JIBU: Hapana ila uchaguzi wowote ule Mkali huacha makovu makubwa ama ndani ya chama au kati ya chama na vyama washindani.

SWALI: Tunayo mifano ya chaguzi zilizo pita zili acha makovu makubwa kwenye chama chetu ili iwe kama mfano?

JIBU: Chaguzi za Ubunge Jimbo la Kinindoni tulipo rudia Baada ya Mh. Mtulia kuhama chama.

SWALI: Madhila chama kilicho yapata jee yamepona ? na chama kipo imara sana sasa hivi kuliko kabla ya Uchaguzi?

JIBU: Hapana chama kilipigika

1) Kwa Wabunge kupoteza muda mwingi Mahakamani.
2) Chama kilipoteza pesa nyingi kwa kukodisha mawakili
3) Wabunge kutumia muda mwingi nje ya bunge na kupoteza posho.
4) Wabunge na viongozi kulala gerezani (mahabusu)kwa mara kwa mara
5) Kulipa faini kubwa baada ya hukumu na hatuna hakika sana ni Wabunge na viongozi, Chama au wanachama ndio walio lipa hiyo faini?

Sasa hivi Viongozi wakitaka kuwa wakweli watakuambia Chadema kimepigika na kuchakaa na nguvu ya kutosha ya chama imetawanyika.

SWALI: Chama kinaweza kuvumilia tena kwa miaka 5 kipigo kilicho kipata kwa miaka mi 5 iliyo pita?

JIBU: Chama hakina uwezo huo kwa leo, kwa hiyo tunakiwa kujitibu majeraha kwa hii miaka mitano ili tujenge uwezo na nguvu ya kutosha.

TUMPE BENDERA LISSU ILI TUPOTEZE CHAMA, AU TUMPE NYALANDU ILI TUJITIBU MAJERAHA NA TUBAKI NA CHAMA CHETU?

CCM Conservatives wanataka Lissu ashinde ili mkulu akifute chama kabisa. Kwa sababu katika vitu Mkulu hapendi ni kadharauliwa.

Lissu ameachiwa sio kwa sababu ya huruma, HAPANA: ameachiwa ili afanye kampeni yake ndani ya Chadema atimize CCM kulia lia wanavyotaka. Nina mengi lakini kwa leo I rest my case.
 
Mkuu nilidhani utaeleza ni kwa namna gani Lissu atakiuwa chama na Nyalandu kukitibu kama ulivodai ila sijaona kwenye mada yako yote.

Nimeandika ili nipate michango yenu pia, naweka michango yangu wazi ili michango iwe ya kutosha.
 
Wenzako wanasikitika ni wapi walipokosea kumuua Tundu Lissu na ni jinsi gani wanavyoweza kusahihisha makosa yao wakamumaliza kabisa Tundu Lissu, wewe unasema CCM wanataka CHADEMA wampitishe ili Magufuli aifute CHADEMA utafikri chama ni mali ya Lissu wakati chama ni cha watanzania.
 
Lumumba's Monitor umeandika hivi na umeteuliwa kwa kukuamini ili upost vitu kuntu vya kufarakanisha Chadema na wafuasi wAke. Sasa kama ww hv kweli huko si mtakuwa na kiwewe cha Lisu tu? Mkubali tu Nyalandu kashindwa
. Point yenu ilikuwa moja tu kama nyalandu angepita, "CCM NDIO TUNAWAPA CHADEMA MGOMBEA WA URAIS TENA YULEE TUNAENUONA HAFAI NA MAJEMBE YAPO HUKU" Mkirejelea kwa Lowasa
 
Lissu only and only Lissu! Ndiye pekee wa kumuweza jiwe na uharamia waliouzoea! Watanzania tusitolewe kwenye mstari na makuhani wa uhalifu
Sasa tundu na jiwe nani anamweza mwenzake, simple tu, jiwe linaziba tundu.
 
Wenzako wanasikitika ni wapi walipokosea kumuua Tundu Lissu na ni jinsi gani wanavyoweza kusahihisha makosa yao wakamumaliza kabisa Tundu Lissu, wewe unasema CCM wanataka CHADEMA wampitishe ili Magufuli aifute CHADEMA utafikri chama ni mali ya Lissu wakati chama ni cha watanzania.
Mkuu, binafsi, sina cha kuongezea!
 
Back
Top Bottom