Dunia tambara bovu, mie hayo yamenipata.yuko mbosi wangu mmoja alipigwa chini kwa tuhuma za ufisadi, nimekutana naye juzi juzi nikajikausha asije kujisikia vibaya; alikuwa amevaa kandambili zilizochoka kama hizo halafu rangi zimetofautiana.Kweli dunia tambara bovu halikawii kuraruka.
Sio wote wanaovaa hivyo wamechacha! Wengine wanavaa hivyo kwa kutii masharti ya FUNDI
Sio wote wanaovaa hivyo wamechacha! Wengine wanavaa hivyo kwa kutii masharti ya FUNDI
Hizi ndo zilikuwa BATA za ukweli... Achana na maUMOJA ya siku hizi mikanda inakatika wakati kanyagio bado nzima!du yana mikanda migumu kweli bado mikanda ni mipya!
Ni kweli kabisa mkuu, kuna mzee moja tajiri wa ng'ombe huko kijijini kwetu lakini siku zote analalia ngozi ikiwa imetandikwa chini. Moja wa watoto wake alimletea kitanda na godoro akijaribu kumlazimisha kulala kitandani ilishindikana na akawa anatishia kumlaani mtoto wake kama akiendelea kumlazimisha kulala kitandani.