Kumbukumbu zangu kwenye mitongozo

Kumbukumbu zangu kwenye mitongozo

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,694
Reaction score
12,354
Kutongoza ni arts ambayo ukiiwezea utacharaza mboko kijiji kizima lakini usipokuwa fundi utaaibika usione pa kupitia ukienda kwenye mishe mishe zako.

1. Hapa nikiwa form2 way back 2010 hiyoo, kulikuwa na classmate namzimika kinoumah sasa kila nikitaka nitupie swaga aibu kibao kwani alikuwa mtu wa kujichanganya na masela au wahuni wa darasa huku mimi nikiwa John kisomo basi nilikuwa namuogopa nikimuona tu ndukii

Siku moja bana tukatangulizana way to school, nikasema hapa niko mwenyewe lazima nitupie ndowano sasa aliponiona namkimbilia kumkuta nae akaongeza mwendo dah! Yani ile namkuta tushafika shule nikajikaza nikamuita akasimama, nikaanza kumwelezea kuwa nampenda ila ananikimbia, Ile hajajibu kawaona masela wake uyoo kasepa alooh ilikuwa nikimuona darasani namkwepa maana nilihisi kanitangaza kwa wenzie na mpaka tunamaliza sikumtongoza tena tulikuwa tukiangaliana tu
 
2. Hapa nipo first year second semester kabla sijadisco mwaka wa pili. Lilikuwa ni kipindi cha TP (teaching practice), sasa bana kulikuwa na lile vibe la maticha wa tp na kufuata mkumbo kuvibaruza vitoto vya form4 vinavyomaliza

Sasa kulikuwa na kimoja hicho nilikielewa lakini kinaonekana ni kimanzi cha misimamo ya dini, nikaanza kukiset na nikakiambia kije kichukue materials ndichi moja hivi ambapo ndio tulipo kuwa tukikaa maticha wa field. Nikawaset wana wakasema tunakuachia uwanja kaka mpira wa penalty huo nikaandaa na mazaga mambo ya chipo nini na hakukuwa na materials wala nini

Ikafika muda wa kuchinja toto likaibuka limejazia fulani hivi nikasema yees! Nikamkaribisha ndani akakataa akasema tukae tu kwanza sebuleni nikasema isiwe shida, nikaleta mazaga tukaanza kupiga huku naimbisha mdogo mdogo kumbe muda wote huo dogo kaja na kaka yake ambae akitoka huyo kaka ndio kuzaliwa yeye mara shwaa jamaa hilo "assalam aleikhum" hee! Ni kazuga zuga pale na vile sikuwa hata na tilio hata la kuzugia ile ilikuwa total embarrassment ila nikachomoka uzuri ndio tulikuwa tunamaliza tp likaisha namna hiyo
 
3. Hapa lilikuwa vibe la kumaliza form4 kulikuwa na manzi naifukuzia prepo sasa ilikuwa hamna kusoma ni kutongozana ile kihindi hindi na tukitoka prepo yeye na marafiki zake nikiwa na rafiki zangu tutatoka njia nzima ni kuomba mechi bila mafanikio. Siku moja tukatoka tunafika sehemu kuna uwanja wa shule moja ya rafiki yake akanivuta nikajua anataka kunipa mbinu ya kumpata rafiki yake badala yake akaniambia yeye ananinipenda ila anaona nahangaika na rafiki yake na alikuwa anataka akalale kwangu

Nikaona ile ni mbinu ya kunitoa mchezoni labda yule manzi ananipima imani nikakataa nikamwambia pole ila mimi sikutaki na nikamtajia na maboy wake ambao nilikuwa nahisi wanamuweka. Alooh ile ni kama nilijiroga maana kumbe alikuwa serious na kilichofata ile crew ikafa na nikakosa jukwaa la kuendelea kumpambania yule manzi, kiufupi niliwakosa wote
 
4. Hapa nilipata manzi mmoja hivi baada ya kumaliza olevel huyu pia alikuwa classmate ila huyu tuseme kanitongoza maana sikumbuki nilivyompata nilijikuta nipo kwenye mahusiano nae

Sasa bana siku moja tukiwa chuo alizingua akaanza kunikataa huku mimi nikiwa deep kwenye mahusiano, kibaya zaidi tulikuwa vyuo tofauti hivyo nikaona hapa Kuna mwana kashanizidi kete alooh nilichanganyikiwa kiasi cha kudisco mwaka ule kwa ajili ya stress

Katika kuhangaika kujinasua nikajikuta namsimamisha manzi mmoja wa first year, nikatupia kamba akanipa masharti kibao eti hadi tuoane ndio tufanye nikamwambia sio kesi huku nikiwa namlengesha aje getto nitoe ule mzizi wa fitina ila kila akija anakaza namuachia

Mwisho wa siku manzi wangu wa mwanzo akajirudi tukawa na mawasiliano vizuri nikamfuata uyu anaenilingia nikamwambia manzi yangu karudi kwenye mstari hongera kwa kukaza maana sijui ingekuwaje ila alilalamika kinoumah eti ashanipenda nikashangaa hivi hawa manzi mtu anakupendaje wakati hajakutunuku tunda?
 
Back
Top Bottom