Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Ngao One, May 18, 2011.

 1. N

  Ngao One Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kuna tetesi kuwa Saed Kubenea, mhariri mkuu na mmiliki wa gazeti pendwa la MwanaHALISI naye ni miongoni mwa waandishi wa habari walionunuliwa na Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge kwenye mkakati wa kuzuia mafisadi hawa wasifutwe uanachama wa CCM.

  Tetesi ziliopo ni kuwa Kubenea kapewa pesa na mali kadhaa zenye thamani kubwa ili gazeti lake la MwanaHALISI liache kabisa kuwaandika habari yoyote mbaya (negative) kuhusu kina Rostam, Lowassa na Chenge tangu CCM ilipowataka wajitoe wenyewe kwenye uongozi.

  Pamoja na kupigwa marufuku kuandika habari zozote mbaya kuhusu Rostam, Lowassa na Chenge, Kubenea pia amepewa kazi maalumu kuandika habari za kumchafua Rais Jakaya Kikwete, mtoto wake Ridhwani Kikwete, Samuel Sitta, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa CCM.

  Baada ya kuangalia mwenendo wa MwanaHALISI kwa wiki kadhaa na kuona ni kweli gazeti hili limekuwa na kigugumizi cha ghafla cha kuandika maovu ya Lowassa, Rostam na Chenge na badala yake linamshambulia Kikwete na Sitta kila kukicha, nimepata hofu kuwa huenda hizi tetesi si za kupuuza hata kidogo.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Maneno matupu, tetesi kama hizi peleka Manywele Salon.
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata mimi utasema nimenunuliwa

  Sioni kosa la RACHEL ndani ya chama cha magamba

  wamefanya lipi baya kwa ccm watimuliwe

  Mbona gamba kuu JK Mkapa Meghi waendelee kuwemo.

  RACHEL wanaqualities zote za kubaki CCM
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dreaming!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!????
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mihandarati hii!
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Vipi kama alishamaliza kuandika yote yanayowahusu RACHEL na isitoshe hawana tena office za umma ambazo wanaweza kufanya ubadhirifu mpya unataka aandike habari za kutunga ili tu kuwachafua?
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hajanunuliwa wala kunadiwa na hatanunulika!! Ila anasema ukweli ambao hata mafisadi wameamua kuusema hivi sasa!
   
 8. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tetesi za Mukama kutoka chama cha magamba
   
 9. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  ahaaa kumbe ni tetesi, ngoja niwahi foleni
   
 10. W

  Warofo Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi ni msomaji wa miaka mingi wa Mwanahalisi. Kusema kweli hata mimi nimekuwa nikishangaa mbona kwa wiki kadhaa sasa gazeti hili limekuwa likiwagwaya kina Chenge, Lowasa na Rostam? Mwahalisi lilijichotea sifa nyingi kwa kuandika habari kubwa bila woga. Sasa huu woga wa ghafla dhidi ya mafisadi umetoka wapi?

  Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu mwenendo wa gazeti hili kwa kweli, maana mafisadi wana billions of shillings at their disposal na wanaamini kuwa everyone has a price. Au wamefika bei kwa KUBENEA?
   
 11. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,971
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kwani hao unaowatetea si mafisadi au? Kashasema saana mengi tu ya kina RACHEL sasa anakuja kwa hawa mafisadi wanaojifanya wasafi jk and the band, yaani mshaanza mtu akisema ukweli wenu kanunuliwa jamani mnafikiri kila mtu anaingia kingi kichwakichwa ka nyie 2005? Mawe pande zote mtafurahi
   
 12. N

  Ngao One Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ahsante kwa kuona hilo!
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  :mimba::mimba::mimba::mimba:
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  :mimba::mimba::mimba::mimba::mimba::A S 103::A S 103::A S 103::A S 103:
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lisemwalo lipo. Taarifa kwamba huyo bwana ameshakaa na RACHEL zipo sana mjini. Nasikia sasa hivi wanamtumia kumchapa JK ambaye tayari wanamuona adui. Ngoja tusubiri, najua mambo yata-unfold soon.
   
 16. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa Napita. Naona napoteza Muda tu na Tetesi Tetesi !!! Leteni Habari za Uhakika !!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Sio lazima uanzishe thread kama hauna cha kuandika.
   
 18. N

  Ngao One Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nimejaribu kufanya utafiti pori. Mbele yangu nina faili zima la magazeti ya MwanaHALISI. Toleo la mwisho ambalo gazeti hili liliandika habari ya kumbamiza Lowassa ni tarehe 6 Aprili kwa kichwa cha habari: "Lowassa hasafishiki."

  Baada ya hapo, matoleo yote 6 yaliyofuata ya MwanaHALISI yamekuwa na habari za kuwatetea kiaina kina RACHEL, kumwandama Kikwete na kujaribu kumgombanisha Kikwete na Sekretariati ya CCM.

  Angalia kama ifuatavyo matoleo haya mfululizo ya MwanaHALISI:

  1. Kikwete 'jino kwa jino' na Lowassa (13 Aprili)

  Habari hii ilipotoshwa makusudi kujaribu kuonesha kuwa uamuzi wa NEC wa kuwafuta kazi mafisadi ndani ya CCM ni vita kali vya madaraka kati ya Kikwete na Lowassa na si uamuzi rasmi wa CCM kama chama.

  2. Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete (20 Aprili 2011)

  Habari hii iliyokuja immediately baada ya kikao cha NEC ya CCM imesema kuwa Slaa amtaja tena Kikwete katika ufisadi. Ikaongeza kuwa avuruga mkakati wa "gamba." Habari nyingine kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ikasema kuwa: Lowassa, Rostam, Chenge bado

  3. Mukama amdanganya Kikwete (27 Aprili 2011)

  Habari hii ikitaka kuonesha kuwa Sekretariati ya CCM mpya iliyochukua nafasi baada ya kufukuzwa kwa mafisadi haifai.

  4. Kikwete mahakamani (4 Mei 2011)

  Huku habari nyingine ikisema CCM yafyata kwa mafisadi

  5. Nyumba ya Kikwete yazua utata (11 Mei 2011)

  Gazeti hili likiwa linaendelea kumwandama Kikwete kwa tuhuma huku likikaa kimya kuhusu kina RACHEL.

  6. Kikwete ndani ya CCJ (18 Mei 2011)

  Huu ni muendelezo ule ule wa mkakati wa kina RACHEL wa kuibua tuhuma dhidi ya Kikwete kupitia MwanaHALISI ili wao waweze kusalimika.

  Naomba kuwasilisha...
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na tetesi kwamba hata wewe umenunuliwa na Ridhiwani na baba yake mzazi kwamba uje hapa jamii forum kuhakikisha unawatetea kwa namna yeyote uwezayo lakini mimi nilipuuzia hii tetesi, lakini sasa naanza kuhisi hizi tetesi si za kuzipuuza.
   
 20. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mh kweli, nipeni simu ya kubenea nimweleze live, huyu kijana ataponzwa na visenti vya mafisadi na kuharibu kabisa future yake. nataka nimweleze kama amepokea pesa ale lakini mashambulizi paleplae. je mkurugenzi mwenzake wa mwanahalisi, Antony KOMu, ambaye pia ni mkurugenzi wa fedha na utawala wa chadema naye kapewa chochote na akina lowasa?
   
Loading...