Fidel80,Unajua Mwakalinga mbona kile kikundi ambacho kilikuwa kina jinadi kuwa kimeahidiwa laptop mbona hukukanusha na wala hukuwakataa kama ndo wapiga debe wako sasa hawa ndo walio chafua hali ya hewa.
tutashinda!....................Fidel80,
Mbona nilikanusha hilo la laptop? Hakuna shule au mtu yeyote niliyemwahidi laptop, unajua JF watu wanakuza mambo mpaka unacheka.
Hata huko jimboni wakati mwingine inabidi uwe mkali. Unakuta mtu uliyeongozana naye amesema jambo ambalo mpaka unaona aibu. Inabidi ukitoka hapo umwambie, mambo kama hayo hutaki. Mtu anatangazia umma kwamba una uwezo wa kujenga mbingu, wakati hata uwezo wa kutengeneza baiskeli huna.
Siasa za TZ zinatakiwa mabadiliko makubwa sana hasa upande wa kusema ukweli. Wapambe wanaweza kufikiri wanamjengea mtu kumbe wanambomoa. Mimi kule Kyela baada ya siku ya kwanza, nikawatoa wapambe kwenye utangulizi maana walikuwa wanawaambia wananchi uwongo ambao nisingependa kusikia.
Ukiwaambia hapana tusifanye hivyo, wanakumabia mambo mengine utarekebisha baada ya kupata. Ukiwakataza tayari ni ugomvi, wanaanza kudai huwaamini, unaleta mambo ya Ulaya nk.
Ni kazi kweli kweli, muhimu ni kutokukubali kubadili maadili au misimamo yako kirahisi. Wakati mwingine ni bora ushindwe huku umebaki na maadili yako kuliko kutafuta ushindi kwa njia zozote zile.
Siasa za TZ ni ngumu mno kwa mtu anayeamini. Mwenyewe nimejiuliza mara nyingi, natafuta nini hapa? Lakini pia unaona opportunities za kuweza kusaidia zilizopo na kwa matatizo ya kule vijijini, hata ukiweza kuwasaidia watu 20 kubadili maisha yao huenda ni bora kujaribu.
- Well kama kawaida yetu, huwa tunataka kwanza kusikia toka upande wa pili yaani hapa umebaki upande wa Kubenea, sasa yeye aliwahi kusema hapa upanga ni kwa upanga, ajitokeze ili tujue ukweli ulipo!
- Ingawa sio siri kwamba baadhi ya habari zake katika hii article, knowing Mwakalinga as I do zina walakini, lakini bado tutnampa the benefit of the doubt kama demokrasia inavyotaka, sasa ajitokeze tuone jinsi upanga kwa upanga, kama kweli ni theory of the truth au ni majungu at best!
Respect.
FMEs!
.- Well kama kawaida yetu, huwa tunataka kwanza kusikia toka upande wa pili yaani hapa umebaki upande wa Kubenea, sasa yeye aliwahi kusema hapa upanga ni kwa upanga, ajitokeze ili tujue ukweli ulipo!
- Ingawa sio siri kwamba baadhi ya habari zake katika hii article, knowing Mwakalinga as I do zina walakini, lakini bado tutnampa the benefit of the doubt kama demokrasia inavyotaka, sasa ajitokeze tuone jinsi upanga kwa upanga, kama kweli ni theory of the truth au ni majungu at best!
Respect.
FMEs!
Tatizo la Tanzania ni kwamba uandishi wa habari wanadhani ni seheme ya kujipatia utajieri hivyo wamekuwa ni mamluki kwa kuhongwa fedha kwa ajili ya kumchafua mtuu thats why wa tz tunadharauliwa sana katika taaluma zetuMovie;
Be aware!
na magazeti ya Kubenea na Kibanda kwenye chaguzi za vyama mbalimbali, na nafasi yao katika jamii!-HATARI!
Ikiwa tunapiga kelele Mengi na vyombo vyake vya habari! mara RA na vyombo vyake vya habari!
Then haya magazeti ya akina Kubenea na Kibanda hayana tofauti na ya akina RA na Mengi, wote wanafanya kitu kile kile.AFADHALI mara mia Mengi na RA!
Kwa waandishi wa habari wahariri kuonyesha personal interest kutumia nafasi zao ni hatari zaidi, hasa katika jamii ambayo hapo kwanza iliwahi kuwaamini! Ulimwengu alishafannya kama haya alijuta baadaye na Rai yake
semeni yote; Kubenea and Kibanda is another ticking bomb, simply kwa sababu walificha makucha yao, wakaiteka jamii sasa wanajifunua wazi wazi ni akina nani!
Yaani nchi hii kila mtu atakuwa na gazeti lake sasa!
George Mwakalinga sio kijana kama unavyotaka kuonyesha, ana miaka 44 ambayo ni zaidi ya kuwa kijana.
Mwakalinga alimaliza shule mwaka 1997. Aliajiriwa na Lucent Technologies miezi michache kabla ya kumaliza shule yake. Baada ya kufanya kazi Lucent miaka minane, December 2005 alihamia Huawei Technologies ambako yuko mpaka sasa. Mwakalinga hajawahi kukosa kazi hata siku moja tokea alipomaliza masomo 1997. Sasa huo ni uanafunzi gani baada ya miaka 12? Lengo ni lile lile kudanganya watu waone Mwakalinga ni kijana tu! ni mwanafunzi tu.
George Mwakalinga hakufuatwa London na Mwakipesile au Mwang'onda. Sijui hata kama Mwakipesile amewahi kuwa London miaka ya karibuni. Mwakalinga aliamua kugombea ubunge tokea mwaka 2007 na March mwaka huo alituma watu kuonana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela, bwana Mwakasumi na kumwambia dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela mwaka 2010. Picha na uthibitisho mwingine wa mkutano huo ambao ulifanyika pale Sativa Kyela vipo. Kumbuka hiyo ilikuwa mwaka mmoja kabla hata report ya Richmond kusomwa bungeni.
Mwakilishi wa Mwakalinga alikutana na Mwakipesile mwaka 2009, February kumwambia kuhusu dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela. Hiyo ni miaka miwili tokea Mwakalinga aanze harakati za kuwaambia baadhi ya wadau wa Kyela kwamba ana mpango wa kugombea. Team Mwakalinga iliamua kumwona Mwakipesile baada ya kupata uhakika wa kiasi kwamba Mwakipesile hana mpango wa kugombea. Kabla ya hapo hakukuwahi kuwa na mawasiliano yoyote kati ya Mwakalinga na Mwakipesile. Kuna watu wengine mbalimbali wa Kyeala, wanasiasa na wasio wanasiasa ambao team mwakalinga imekutana nao kuwaambia juu ya dhamira yake ya kugombea. Kama kukutana na mwana Kyela yeyote London au TZ ni makosa, si wataje wote niliowahi kukutana nao wakiwemo waliotumwa kunishawishi nisigombee? Watajeni akina Kifukwe, na wazito wengine huko jeshini.
Wana JF wanajua maana hiyo safari ilijadiliwa vikali hapa JF. Mwakalinga alikuwa Kyela kwa siku sita. Alifika yeye pamoja na familia yake siku ya Jumatatu (24/07/09) na kuondoka Kyela Jumamosi usiku (30/07/09). Kwahiyo, mwezi August Mwakalinga hakuwa Kyela wala hakukaa Kyela mwezi mzima.
Mwakalinga kila mara anaporudi nyumbani na familia yake yote hufanya sherehe ya pamoja kama njia ya familia yote kukutana pamoja maana kunakuwa hakuna muda wa kutembelea kila mtu katika siku hizo chache. Mwaka 2003 pia alipoenda na familia yake alifanya sherehe nyumbani na kuhudhuriwa na ndugu wote pamoja na majirani. Mwaka huu pia alienda nyumbani na familia ikiwa ni pamoja na mtoto wake wa mwisho ambaye alifika nyumbani kwa mara ya kwanza. Sherehe ya mwaka huu ikaongezewa nguvu na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kugombea ubunge. Sherehe ilihudhuriwa na ndugu na wananchi wengine wa maeneo ya jirani. Hakukuwa na speeches wala maneno ya kwamba anaingia vitani.
Uongo! alitembelea kata 19 kati ya 21. Hakutoa msaada wowote wakati wa ziara nzima. Mwakalinga anatoa misaada mashuleni kwa muda wa zaidi ya miaka 15 sasa. Kuna kitabu cha misaada yote kiko pale Kyela Business Center (KBC) na anayetaka kuangalia anaweza kuhakiki na kuona lini alitoa msaada gani na wapi. Misaada yote hutolewa kiuwazi ila bila sherehe maana muda wote alikuwa hataki publicity.
I wish Mwakalinga angelikuwa na pesa zote hizo. Uwongo mkubwa sana! Hakuna hata mwananchi mmoja wa Kyela anayeweza kuthibitisha kwamba alipewa pesa kati ya shilingi 10,000 na 100,000. Kama yupo aende polisi kutoa taarifa. Tunamtafuta huyo Edson Matai ili kama kweli ni raia basi tumsaidie kumpeleka polisi ili akatoe ushahidi. Tumechoka Kyela kusingiziwa mambo ya ajabu. Inabidi tuanze kuwashughulikia wale wanaoona wanaweza wakasema au kuandika lolote bila ya chembe ya ukweli.
Hata ukimwuliza kichaa Kyela anajua kuna sehemu panaitwa KBC. Sasa mwandishi gani huyu na uchunguzi wa muda mrefu hata hajui kwamba hiyo kampuni inaitwa Kyela Business Center (KBC)? Hiyo KDC labda ni kampuni ya Kubenea ya kufikirika. Unajua habari za kupewa na watu wengine huwezi kuwa sahihi nazo.
Sasa huyo Mwakipesile, yeye mwenyewe anagombea ubunge na mara anaratibu shughuli za ubunge za Mwakalinga, mbona hayo maajabu?
Ni aibu kwa mtu kama Kubenea ambaye unajifanya mpiganaji, kuanza kutumia gazeti lako kuchafua watu wengine bila sababu zozote. Najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli? Mmezunguka kutafuta uchafu wowote na mmeshindwa sasa mnataka kumchafua mtu kwa kumhusisha kwa karibu na watu ambao mnawaona wachafu. Tatizo lenu ni kwamba hamuwezi hata sehemu moja kupata mahali ambapo Mwakalinga yuko karibu au hata anafahamiana na akina Lowassa, RA, Karamang au huyo Patel.
Mlianza na kusema Mwakalinga amepewa milioni 400. Mmeona wana Kyela wote wamewadharau baada ya kuona hizo milioni 400 hawazioni na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza hata akasema amepewa laki moja na Mwakalinga. Sasa mnaanza majungu mengine ya kijinga, lakini na yenyewe yataishia patupu maana hamna data na uongo haudumu hata siku moja.
Acheni majungu na fitina; waache wana Kyela wachague kiongozi wanayemtaka kwa utashi wao. Kama mna ugomvi na Mwakipesile, pelekeni nguvu huko, kuanza kujaribu kumhusisha kila mtu haitawasaidia maana wana Kyela sasa wanajua nani anasema ukweli na nani anakimbilia magazetini kila saa kupaka wana Kyela wenzake.
Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?
Shame on You Kubenea and your Newspaper!
Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?
Shame on You Kubenea and your Newspaper!
huyu sio tu ni upande wa mwakalinga, ndiye mwakalinga haswaaaaa
soma hapa najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli?
....................Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?
Shame on You Kubenea and your Newspaper!
Waungwana ni bora tubandike hoja kwa hoja na tuachane na mambo personal. Sidhani kama ni jambo la busara kuhusisha crime aliyofanyiwa mtu na mpambano wa hoja hapa JF,binafsi naamini hiyo ni foul...Kama Kubenea angekuwa amepigwa kisu ama risasi,basi huwezi kuja hapa na kusema kuwa ndiyo maana ulipigwa risasi ama ulichomwa kisu,ni sawa na mnapodai kuhusu kumwagiwa tindikali,kama hayo ya kumwagiwa tindikali hayahusiani na dhumuni hasa la mjadala huu ama hoja zake,basi si vyema kuzi bring up kwa style hiyo kwasababu ni kama uonevu,kwani kumwambia kuwa alifanyiwa shambulizi la kinyama kwa kukosa hoja ni sawa na kumdiscourage na yeye kutoa hoja zake hapa JF,na kama shambulizi hilo alifanyiwa kwasababu nyinginezo kama inavyokuwa speculated kuhusu mke wa mtu,je hilo linahusiana kivipi na uandishi wake?Ama uwezo wake wa kuchangia hapa JF?ama linahusiana vipi na makala yake hiyo kuhusiana na kina Mwakalinga?Na kwahiyo watu mnaojiita great thinkers mnakubaliana na watu kujichukulia sheria mkononi?Kuna mtu humu ndani ambaye hajawahi kumuudhi mtu mwingine the same way Kubenea alivyomuudhi mshambuliaji wake?Na kama wamo watu ambao wameshawaudhi wengine kwa namna moja ama nyingine,je muna encourage kuwa wajichukulie sheria mkononi?Na kwahivyo basi hata yule aliyem mwagia tindikali Kubenea kama na yeye anapita hapa JF basi anafurahia tu na kuona amefanya jambo la maana.
So naamini kabisa ujumbe ungekuwa umefika bila ya kum "Blackmail" victim wa crime kwenye mijadala,hiyo ni personal issue,ni shambulizi lililomwathiri kwa kiasi kikubwa na si ustaarab kufurahia mabaya yanayompata mtu na on top of that unam nyanyapalia.
Ma two cents.
Mwakalinga has taken out his veil and announced that he is our JF'S Mtanzania!! Mwakyembe inasemekana yeye anaingia humu JF kwa majina mengi tu lakini si la Mwakyembe;
will he be courageous enough like his nemesis to announce his true identity hapa ukumbini? hiyo itatusaidia kujua kama ninani anaetoa hoja badala ya sasa ambapo wahusika ndio wanaoandika nasi tunadhani ni wapambe wao!!
Mtu yeyote anaeandikaka kitu anachokiamini na si majungu hawezi kujificha kwa kutumia majina bandia; mbona sisi wengi tunatumia majina yetu humu janvini!!
Wana JF toeni hoja acheni kutukanana kupitia thread. Kama mna visa vyenu pelekeni uswahilini. Pinganeni kwa hoja si kwa matusi! Mf."Shame on You Kubenea and your Newspaper!" by Mtanzania, na "3.Wapo maswahiba wake hapa(MWAFRIKA NA MASANILO) watatufafanulia zaidi kuhusu Ujinga wa mbunge huyu mwenye mdomo mkubwa.Kulia kwenye media ndiyo kutatua matatizo yake." by Samwel Let the JF be The Home of Great Thinkers and not rigmaroles.
Mengine uliyoandika ni safi......however this one
Yes wewe ni binadamu kama wengine lakini..........that one........speaks volume..........
Hebu msome Mangi hapa chini........
.........notwithstanding the above.......Nakutakia kila la Kheri Mwakalinga aka Mtanzania wa JF
.
1.Mwakyembe ka-divorce na Mengi na sasa ameoana na Kubenea.Huyu bwana ndiyo maana alimwagiwa tindikali usoni.Ata gazeti lake limeanza kukosa ubora tena.Limejaa majungu,unafiki na uongo.
2.Inasemekana Mwanadishi wa nakala hiyo ni Mwakyembe mwenyewe na hiyo ni tabia yake.Alikuwa akiifanya ata kwenye gazeti la Nipashe bila kutaja jina la mwandishi.Sasa huko wamemshitukia alipoandika habari za uzushi kuhusu kuchomwa kisu ili watu waamini eti anaandamwa na mafisadi.
3.Wapo maswahiba wake hapa(MWAFRIKA NA MASANILO) watatufafanulia zaidi kuhusu Ujinga wa mbunge huyu mwenye mdomo mkubwa.Kulia kwenye media ndiyo kutatua matatizo yake.
Mengine uliyoandika ni safi......however this one
Yes wewe ni binadamu kama wengine lakini..........that one........speaks volume..........
Hebu msome Mangi hapa chini........
.........notwithstanding the above.......Nakutakia kila la Kheri Mwakalinga aka Mtanzania wa JF