Japo mimi sina Chama ninachosabikia lakini nitoe maoni yangu kuhusu huu mradi wa Slaa dhidi ya Lowasa.slaa ameamua kuiua chadema yake kwa mikono yake mwenyewe. hii ni hatari sana aise...
Mapadre ni watu waliosoma sana falsafa na hadi kupata upadre anakuwa amekamilika sana busara kutokana na malezi anayopitia, lakini anayofanya sasa Slaa (padre wa zamani) anajidhalilisha sana kiasi hata cha mtu mwenye elimu ya kawaida tu lakini mwenye busara hawezi kufanya. Slaa ndiye mtu wa mwanzo kabisa kumtafuta Lowasa hadi kufanikiwa kumuingiza CHADEMA, leo anafanya jitihada kubwa kuhakikikisha anammaliza Lowasa na CHADEMA. Akumbuke hakuna mtu mmoja anayeweza kuiua CHADEMA. Pia wale watu 11 aliowataja kuwa mafisadi pale Mwembeyanga asidhani watamsamehe asilani kwa sababu ya huu mradi mpya wa Lowasa. Kisasi kwa mwafrika kipo siku zote.
Nadhani Slaa hadi anamaliza maisha yake hapa duniani atakuwa amedhalilika na kudharaulika sana. Nadhani kile kiapo cha upadre alichoasi kinammaliza (mimi ni mkatoliki) Aelewe kuwa hataweza kummaliza Lowasa kama anavyodhani, Tusubiri uchaguzi upite.