Kubali Umekataliwa Maisha Yaendelee

Kubali Umekataliwa Maisha Yaendelee

Mpende mtu na tumia akili mkuu na sio hisia. Mwanamke anavyokuignore ukazidi kumganda ndio anakudharau mara 100 zaidi.

Kupenda ni jambo la hiari sio la kufosiwa kwahiyo mtu akiacha kukupenda kubali uendelee na maisha yako hata kama umemzoea vipi. Sijui tunaelewana kesi ishakuwa ngumu.
 
Bora ametoa kucha mapema na umeshituka kuanza upya siyo ujinga anza sasa
 
Pole sana mkuu.....

Mwanaume kwenye mahusiano unatakiwa kutumia akili, sio hisia.... ukitumia hisia utaumia sana tena sana, lazima utambue wanawke msimamo wao inatengenezwa kama hakutengenezwa kwa wazazi wake hiyo ni ntihan
 
Mtu Akichagua kukuona sio wa Thamani kwake hata Ufanye nn Bado wewe sio wathamani kwake.

No Call, No Sms Kubali kua Hakuitaji na Ujipe Tumaini kua Maisha yanaendelea, nilijenga mpaka nyumba Ili nimpe chumba awe anachukua Kodi lakini aliniacha kwa Dharau na nyodo kibao.

Niilijifunza kukubali kukataliwa, Hiyo nyumba Imekua kumbukumbu yangu ya Upendo kwake. Nilikua nampenda sana Tena sana, nimejifunza mwanadamu ukimpenda anakudharau.
Nilimpenda sana mpaka nilikua kama mjinga kwake Dharau zilizidi ananiblock Kila nikimtafuta kwa namba ngeni anablock. Nilijipa Moyo kua Yatapita tu na nitamsahau.
Upaswi kumpenda mtu sana. Hata siku Moja usimpende mtu sana utateseka. Mtamani ila usimpende maana Binadamu unapompenda yeye anakuletea Dharau.
Nilidharaulika sana.Ktk Maisha usiombe Kumpenda mtu.
Miongoni mwa jambo Baya Ktk Maisha ni kumpenda mtu na yeye asikupende. Utaona Kila Dharau ambazo ujawai ziona mtu anakutazama kama Kinyesi au Funza wa Chooni, Binadamu sio Poa ni Bora umpende Hata mnyama ataelewa Upendo wako ila sio mwanadamu ukimpenda nyodo na dharau atakazokuonyesha.
Sio kweli watu wenye damu kama group lako hata mpendejwe Huwa mnaona hampendwi
 
Back
Top Bottom