The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Wapendwa wana JF,
Salaams!
Napenda kushirikiana nanyi katika hili kwa kuwa uzoefu umenifundisha kwamba wengi wetu tunapenda sana tuwe na mahusiano yaliyokamilika kadri tunavyoona inafaa. Ila ukweli ni kwamba si watu wengi wamebahatika kupata nafasi ya kupenda na kupendwa kwa kiasi kinachowaridhisha wahusika au watu wanaowazunguka.
Pale mapenzi yanapoingia maumivu tujitahidi kujadiliana namna ya kusaidia kupata furaha na inaposhindikana tusisikitike sana kwa kuwa hakuna aliyeahidi kwamba mapenzini watu watafurahi milele. Siku hizi wife akinikera sana namwambia unachokifanya si sawa halafu nachukua time zangu kudeal na mambo mengine. Akinitaka radhi nashukuru Mungu na asipojali na mie naamua kutojali. Furaha si kubwa katika mazingira ya namna hiyo lakini maumivu pia si makubwa pale akili yako inapokuwa inatarajia lolote kutoka katika ndoa/mahusiano mazuri kwa mabaya.
Nimeapa sitafanya ukorofi kumforce mwanamke kuniheshimu kama ninavyopenda lakini nitamwambia siridhiki. Nikiona amenikera kupita kipimo kwa mambo niliyokwisha mwambia naenda kushuhulikia swala tofauti na kumpuuza kabisa. Ikishindikana tunaachana tu. Lakini sitarajii kutamani kujiua au kukata tamaa ya maisha kisa Mama watoto anafanya ambayo sikuyatarajia.
Yooote tunayokumbana nayo huwakuta watu na hakuna mahala ambapo tulikosea kiasi cha kusema tujute saaana na kuwachukia wapenzi wetu hawa.

- Kuna wandani wachache sana (kama wapo) ambao wanapendana kwa dhati na kila mmoja ameridhika na mwenzi wake kiasi cha kufurahia uhusiano wao tangu mwanzo hadi wanapoaga dunia. Under normal circumstances kama si wote basi japo mmoja wao kuna siku atakerwa na kuwaza pengine mambo yangekuwa bora zaidi kama angemchagua mwingine.
- Wapo wengi waliodumu sana kwenye mahusiano kwa kuvumililana tu wakitarajia mambo yatabadilika siku moja bila mafanikio. Mfano wanawake wanaopata kipigo mara kwa mara lakini hawatoki katika mahusiano hayo (ndoa au mchukuano). Baadhi yao hudhani hawana namna ya kuweza kupata mwingine kama huyo.
- Ni rahisi kujifunza kumpenda mtu (japo kwa maigizo) kuliko kumfanya mtu akupende kwa namna unayoona unastahili. Mwanaume angependa mwanamke anayempa heshima na kumsikiliza kuliko yule anayejaribu kushindana naye muda wote kama hawa wa siku hizi wanaodhani Bwana akichelewa kurudi home basi hata Bibi anayo haki hiyo, lakini si rahisi kumbadili mwanamke kuwa msikivu kama si wa aina hiyo.
- Kama watu walivyo tofauti kwa majina, maumbile, rangi, makabila nk ndivyo ilivyo namna yao ya kupenda, kuheshimu, kuthamini, kuonesha shukrani nk. Nilichagua mwanamke wa kawaida tu (simple) nikitarajia kuthaminiwa zaidi kwa kuwa niliamini hakuwa akiuzika kama walivyo wale mastar wanaowindwa na kila mwanaume na hivyo asingekuwa jeuri sana. Alinipenda sana (nilivyoamini) na nilijua itakuwa rahisi kwangu kuishi naye kwa kuwa nilichotakiwa kufanya ni kuthamini hisia zake na kumfanya ajihisi malkia. Polepole nikajikuta nampenda kuliko nilivyodhania awali. Cha ajabu badala ya maisha yetu kuwa rahisi. Mambo yanazidi kuniwia magumu maana hajali hisia zangu. Anakosa haombi msamaha, kila jambo anataka lifanyike anavyotaka yeye. Amekuwa msumbufu kwa sasa hadi nimefikia hatua namwangalia tu. Nashukuru Mungu kwamba sijagundua kama anatoa nje hivyo naamini hata kama anatoa basi, anatoa kiwizi sana.