Kubali ukweli huu....! Mapenzi hayana kanuni wala ujanja.

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
245
Wapendwa wana JF,
Salaams!
Napenda kushirikiana nanyi katika hili kwa kuwa uzoefu umenifundisha kwamba wengi wetu tunapenda sana tuwe na mahusiano yaliyokamilika kadri tunavyoona inafaa. Ila ukweli ni kwamba si watu wengi wamebahatika kupata nafasi ya kupenda na kupendwa kwa kiasi kinachowaridhisha wahusika au watu wanaowazunguka.
  • Kuna wandani wachache sana (kama wapo) ambao wanapendana kwa dhati na kila mmoja ameridhika na mwenzi wake kiasi cha kufurahia uhusiano wao tangu mwanzo hadi wanapoaga dunia. Under normal circumstances kama si wote basi japo mmoja wao kuna siku atakerwa na kuwaza pengine mambo yangekuwa bora zaidi kama angemchagua mwingine.
  • Wapo wengi waliodumu sana kwenye mahusiano kwa kuvumililana tu wakitarajia mambo yatabadilika siku moja bila mafanikio. Mfano wanawake wanaopata kipigo mara kwa mara lakini hawatoki katika mahusiano hayo (ndoa au mchukuano). Baadhi yao hudhani hawana namna ya kuweza kupata mwingine kama huyo.
  • Ni rahisi kujifunza kumpenda mtu (japo kwa maigizo) kuliko kumfanya mtu akupende kwa namna unayoona unastahili. Mwanaume angependa mwanamke anayempa heshima na kumsikiliza kuliko yule anayejaribu kushindana naye muda wote kama hawa wa siku hizi wanaodhani Bwana akichelewa kurudi home basi hata Bibi anayo haki hiyo, lakini si rahisi kumbadili mwanamke kuwa msikivu kama si wa aina hiyo.
  • Kama watu walivyo tofauti kwa majina, maumbile, rangi, makabila nk ndivyo ilivyo namna yao ya kupenda, kuheshimu, kuthamini, kuonesha shukrani nk. Nilichagua mwanamke wa kawaida tu (simple) nikitarajia kuthaminiwa zaidi kwa kuwa niliamini hakuwa akiuzika kama walivyo wale mastar wanaowindwa na kila mwanaume na hivyo asingekuwa jeuri sana. Alinipenda sana (nilivyoamini) na nilijua itakuwa rahisi kwangu kuishi naye kwa kuwa nilichotakiwa kufanya ni kuthamini hisia zake na kumfanya ajihisi malkia. Polepole nikajikuta nampenda kuliko nilivyodhania awali. Cha ajabu badala ya maisha yetu kuwa rahisi. Mambo yanazidi kuniwia magumu maana hajali hisia zangu. Anakosa haombi msamaha, kila jambo anataka lifanyike anavyotaka yeye. Amekuwa msumbufu kwa sasa hadi nimefikia hatua namwangalia tu. Nashukuru Mungu kwamba sijagundua kama anatoa nje hivyo naamini hata kama anatoa basi, anatoa kiwizi sana.
Baada ya kutafakari sana maisha ya watu wengi wanaolalamikia maisha yao ya ndoa/mahusiano nimegundua kwamba mapenzi hayana formula ambayo mtu anaweza kuifuata ili mambo yamnyookee. Unachotakiwa ni kuchagua unachokitaka kama kilivyo pasipo kutarajia zaidi ya uliyoyaona na kushuhudia. Mkaka ukipata mwanamke mwenye mwonekano au tabia unazozipenda mchukue kwa hayo hayo uliyoyaona na si kutarajia ambayo hujayaona. Si kila mwanamke mrembo na msafi sana kazini lazima awe mke msafi huko home. Kuna wengine kuoga inabidi mkumbushane mkitaka kupumzika lakini asubuhi akitaka kwenda kibaruani hata kama hamna maji atanunua hata ya chupa ili awe msafi atakapokuwa kibaruani. Kina dada nao hivyo hivyo unapomwona handsome mwenye fedha nk si lazima awe mume anayejali. Hawara anayehonga sana si lazima awe mume anayejitolea sana kwa mkewe.
Pale mapenzi yanapoingia maumivu tujitahidi kujadiliana namna ya kusaidia kupata furaha na inaposhindikana tusisikitike sana kwa kuwa hakuna aliyeahidi kwamba mapenzini watu watafurahi milele. Siku hizi wife akinikera sana namwambia unachokifanya si sawa halafu nachukua time zangu kudeal na mambo mengine. Akinitaka radhi nashukuru Mungu na asipojali na mie naamua kutojali. Furaha si kubwa katika mazingira ya namna hiyo lakini maumivu pia si makubwa pale akili yako inapokuwa inatarajia lolote kutoka katika ndoa/mahusiano mazuri kwa mabaya.
Nimeapa sitafanya ukorofi kumforce mwanamke kuniheshimu kama ninavyopenda lakini nitamwambia siridhiki. Nikiona amenikera kupita kipimo kwa mambo niliyokwisha mwambia naenda kushuhulikia swala tofauti na kumpuuza kabisa. Ikishindikana tunaachana tu. Lakini sitarajii kutamani kujiua au kukata tamaa ya maisha kisa Mama watoto anafanya ambayo sikuyatarajia.
Yooote tunayokumbana nayo huwakuta watu na hakuna mahala ambapo tulikosea kiasi cha kusema tujute saaana na kuwachukia wapenzi wetu hawa.
 

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
245
Too long for me!
Sorry! I was trying to make a point. May be it's not your kind of stuff. Unajua kuna watu wemesoma hadi University lakini hawajawahi kusoma makala gazetini wala riwaya yoyote kwa kuwa kwao ni ndefu mno. Some can still do it though.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,793
105,625
Sorry! I was trying to make a point. May be it's not your kind of stuff. Unajua kuna watu wemesoma hadi University lakini hawajawahi kusoma makala gazetini wala riwaya yoyote kwa kuwa kwao ni ndefu mno. Some can still do it though.

You're right. Me and long-windedness don't mix up too well.
 

shalis

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
270
64
asante sana analyst , sana sana naweza sema ulijuaje kama nahitaji ushauri kama huu na kwa wakati na kipindi kigumu kama hich nilichonacho
asante sana kweli JF ni sehemu salama na yenye manufaa
i was so down this morning ila nashukuru huu ujumbe take me up again.
asnte sana na unachokisema kipo sahihi sana sana ....mkuu unaweza kuona ni kitoto cha mjusi kumbe ni cha kenge mpaka kinapokuwa lol kuhamaki umeshmfuga na haiwezekani kutoa .mmh mapenzi hay jamani uuuwwiiiiiiii
 

clet 8

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
1,127
318
Thanks mr. Analyst it is real good and interesting, big up sana.
 

eyetyna

Senior Member
Jun 24, 2011
148
17
POLE SANA MKUU,ila ur so strong just keep it on,endelea na mambo yako tu,na tene uendelee kumpenda na kumuonyesha mapenzi yote ya nayostahili ili nae aone kama hayo anayofanya ni sahihi au si sahihi!
 

fredduar

Member
Oct 4, 2011
16
0
sure ni kweli kabisa. ila inategemea na wapandanao wenyewe. wanaweza wakayafanya yawe na fomula ila by default hayana fomula ni kitu kipo automatically. ukiona mpenzi anahitaji some kind of formular huyo siyo wako.try another one
 

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
790
the real Analyst! Mapenzi yana ujamja bwana. Imagine dogo form 4 them anachukua demu 2nd year kwa swagga zake, huu si ndio ujanja au?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom