KUBAKI KWA KONDO LA UZAZI(RETAINED PLACENTA)

KUBAKI KWA KONDO LA UZAZI(RETAINED PLACENTA)

mchau

Member
Joined
Nov 16, 2024
Posts
89
Reaction score
95
Habari wafugaji natumaini wote ni wazima Leo nimekuja na kitu kipya kabisa kuhusu kubaki kwa kondo la uzazi kwa mifugo wako.

👉Kondo la uzazi ni kiungo kinachounganisha ndama na mfuko wa mimba ili kuruhusu upitishaji wa virutubisho na hewa. Kwa kawaida, kondo hutoka ndani ya saa 6 baada ya kuzaa. Iwapo haitatoka ndani ya muda huo ndani ya saa 12 Hadi 24, hali hiyo huitwa retained placenta.

Ni tatizo la kawaida sana hasa kwa ng’ombe wa maziwa.

---

2. SABABU (Causes):
  • Upungufu wa lishe bora – hasa vitamini A, E na selenium.
  • Kuzaliwa kwa ndama aliyekufa
  • Ugonjwa wa kifua kikuu au Brucellosis
  • Kuzaa kwa upasuaji au shida wakati wa kuzaa
  • Mimba ya mapacha
  • Maambukizi ya virusi au bakteria

---

3. MADHARA (Effects):
  • Maambukizi ya mfuko wa uzazi (metritis)
  • Kupungua kwa maziwa
  • Kushindwa kurudia joto kwa wakati
  • Kushindwa kushika mimba
  • Kutofanya uzalishaji kwa ufanisi
  • Kifo kwa mnyama ikiwa hali itazidi (kwa nadra)

---
Kama unapitia changamoto hii karibu sana tukuhudumie na changamoto nyingine
Kwa mawasiliano zaidi
0674740836
0792263640
 
Back
Top Bottom