Kutokana na nyuzi nyingi kuja humu jukwaani kwa minajili ya kuomba kubadilishana vituo vya kazi kwa kada ya Afya, ipo haja ya kuwa na uzi mmoja utakaokusanya, kujadili na kujibu maombi yote ya aina hii.Uwe Mganga Mwandamizi, Mganga wa Kawaida, Afisa Tabibu, Muuguzi, Mkunga au Muhudumu wa Afya karibu kwenye uzi huu ukutane na wenzako wenye mahitaji kama ya kwako. Kwenye andiko lako ni vema ukasema ulipo, mkoa na wilaya ambako ungependa kwenda na mawasiliano yako. Tunashauri mtumie barua pepe au namba ya simu
KARIBUNI SANA WATUMISHI