Kubadilisha mwelekeo wa Taifa kutoka kwenye ubinafsi kuja kwenye utaifa.

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Swali hili limekuwa likiulizwa sana miongoni mwetu, tumekuwa tukijiuliza kwanini Tanzania ni maskini pamoja na maliasili zote tulizonazo?

Leo ningependa kutafakari kuhusu jambo hili kwa kina na kwa mantiki ili wote tujue kwanini Taifa letu ni maskini na njia gani tufuate ili tutoke hapa tulipo.

Ili tuendelee lazima tubadilishe mawazo yetu kutoka kwenye ubinafsi tuyalete kwenye utaifa na tujenge Taifa hili tofali baada ya tofali itakuwa hatua ya kwanza ya kuondoa umaskini, kwani Taifa haliwezi kujengwa katika ubinafsi bali katika umoja na kujitolea kwa watu wake kujenga Taifa lao wenyewe kwa faida yao na vizazi vyao hii itakuwa hatua ya kwanza muhimu kwenye kupiga hatua kwa Taifa letu, hatutaweza kuendelea kama hatutakusanya nguvu zetu kwa pamoja kukabiliana na changamoto tulizonazo kama hatutatumia nguvu zetu na jitihada zetu za pamoja kuondokana na hali hii.


Kwenye maandiko yangu mengi nimeandika kuhusu nini maana ya Taifa na kwanini watu wanaishi pamoja kama Taifa, leo sita gusa sana huko lakini tulijua Taifa ni kusanyiko la watu wenye malengo mamoja, tulifahamu pia Taifa lazima liwe na dira ya sehemu inayotaka kuelekea na dira hiyo lazima iliridhishwe kizazi hadi kizazi, kama Taifa ni lazima liwe na malengo, na mwelekeo wa Taifa lolote ni ”nguvu” na ”utawala”. Lakini pia kama Taifa tunahitaji mafanikio yatayotupa faraja na heshima miongoni mwa mataifa mengine.



Sababu ya kwanza ya kutofanikiwa kama Taifa ni kuwa na viongozi wasiokuwa na malengo na kama yapo basi sio dhabiti. Hii inaonekana katika mfumo wa uongozi wetu unaoyumbayumba na usio na msimamo juu ya masuala inayosimamia. Lakini pia tumeona poor organization ya serikali yetu pale kauli mbilimbili zinapotoka katika serikali moja hii inaonyesha udhaifu katika mfumo wa uongozi.


Kabla ya kwenda mbele tuangalie kazi ya kiongozi ni nini katika Taifa.
1. Mobilization
2. organization
3. Direction
4. Governance





MOBILIZATION


kiongozi lazima awe na uwezo wa kuwashawishi watu cause anayopigania kwa manufaa ya Taifa, ni lazima ajenge uaminifu kwa raia na kuwaonyesha mambo ambayo anapigania ni kwa manufaa ya wote na yatakuwa na faida kubwa sana kwa Taifa na kuwashawishi kulitumikia Taifa lao wenyewe na kujenga umoja miongoni mwao.




ORGANIZATION.



Baada ya kuwashawishi na kumkubali jambo linalofuata ni ku organize jamii ili wafanya kazi kwa manufaa ya umma. Tunafahamu ya kuwa bila organization no function unit will work.




Kwahiyo Taifa linaundwa na watu tofauti, tofauti sawa? kuanzia katika makabila na ndani ya kabila hizo tofauti tofauti kuna dini tofauti na familia tofauti hivi vyote vinaunda Taifa moja na kufanya a ”complex thing” Kazi ya kwanza ni kuunganisha na ya pili ni kuwaonyesha malengo ya ”Taifa”. Kwanini sisi ni Taifa ndoto zetu ni nini na matumaini yetu ni yapi na jinsi gani tutayafikia kama Taifa. Kwahiyo juhudi ya kwanza ni kuunganisha na ya pili kufanya organization and structureling.


Sehemu ya pili tutatengeneza Taasisi zinazoserve public na zile binafsi na jinsi zitakavyokuwa zinaingiliana. Lengo la sekta zote hizo mbili ni kuwa na functional unit itakayofanya kazi kwa faida ya umma lazima tuangalie jinsi ya kufanya coordination kati ya sekta hizo mbili. Lakini hatutaweza kufanikiwa pasipo kujenga umoja na uzalendo miongoni mwetu.
Tukiisha jenga umoja na uzalendo, tukiisha ji organize sasa linakuja suala la management of our resources na jinsi gani tutazitumia kwa faida ya umma kumbukeni kwamba bila ya ” order” ” harmony” na coordination katika organization yeyote hakuna kitu kitazalishwa iwe kwenye mitambo au taasisi kama organization.



Mfano wa gari na components zake kwenye gari kila kifaa kina kazi yake na system yote inafanya kazi kama kitu kimoja na dereva akiwa mfano wa kiongozi ni sawa sawa na katika nchi hakuna tofauti sana.




” Effeciency of any government depend on the unit of it’s parts to form a functional unit ” Kwahiyo inategemea raia, Taasisi zilizoundwa kutumikia jamii kufanya kazi kama kitu kimoja ili kuzalisha na kusiwe na any discordant element.
Kwa Wanaonifutatilia nilianza kwa ku organize familia ni jinsi gani zina uhusiano mkubwa na Taifa na umuhimu wake katika Tafakari yangu ya Mwanzo ya UJENZI, MUUNDO na MWELEKEO wa Taifa. Tuki order vizuri familia zetu itakuwa rahisi kuzi govern na majukumu ya kila mzazi kwa familia yake is for the sake of the nation sio kwake yeye tu, a health nation is the one which has strong families. Without order nothing Valuable we can produce.




” Operation of any organization depend mainly on the function of it’s parts in order to produce results ”
Tunapozungumzia kuhusu system ni mfumo unaofanya kazi kwa pamoja ili ku produce result na kama hakuna result kuna tatizo katika parts za hiyo unit, hiyo structure organization na structure organization inamhusu kila raia kwasababu ni sehemu ya nchi. Kwahiyo ni lazima tufanye reformation ya jamii yetu kama tunataka tuendelee na kui order upya na mifumo mingine kama ya elimu ili ifanye kazi kama kitu kimoja.





Hili sio suala la ubinafsi bali ni suala la kila mmoja wetu anazalisha nini kwa manufaa ya taifa na vizazi vyetu vijavyo. Kwasababu bila ya hivyo hatutaenda salama kama Taifa kama kila mtu akijiangalia mwenyewe boti yetu haitofika salama sisi sote tuliopo duniani sasa hivi tunawajibu wa kuwafikishia salama vizazi vyetu vijavyo Taifa hili, tuna majukumu ya pamoja. Kwahiyo kila mmoja wetu anamajukumu ya aina mbili kwasababu sisi tumeamua kuwa Taifa lazima tuliangalie Taifa letu na tujiangalie wenyewe as induviduals lazima tulijali na tuli preserve kama kingo zinavyo preserve mto na kupeleka maji yake baharini na hivyohivyo taifa letu lazima liwe ni lenye kutoa faida na wakati huo huo tukilinda kile ambacho Tayari tumeisha kijenga.






DIRECTION



Tumeishajenga organization yetu na kui structure in a very coordinated way iko katika order kama completely ”thing” sasa inakuwa ni kazi ya kiongozi wa kuendesha huo mfumo kama nilivyosema hapo mwanzo ni kama gari na components zake sasa ni kazi ya kiongozi kuonyesha mwelekeo ni wapi Taifa lielekee lakini ili kulinda mfumo ni lazima tuwe na polisi kwaajili ya maadui wa ndani na jeshi kwaajili ya maadui wa nje.
Ili jamii yetu iwe pamoja lazima iwepo haki na tunajua haki ni harmony ya jamii kwahiyo mahakama lazima ziwepo kuhakikisha jamii inaendelea kuwa moja na haki inatendeka. Tunatakuwa na bunge ambao watakuwa wawakilishi wananchi jambo la tutawapataje ni la kutafakari zaidi lakini mfumo wa sasa unafanya watu wasiostahili kuingia bungeni.




GOVERNANCE



Suala la ku govern ni kulinda mfumo ambao tayari umeisha tengenezwa na unafanya kazi kama kitu kimoja.
Kuna mambo mengi sana yanayofanya Taifa hili lisiendelee kitu kikubwa kingine ni ”motive” Iliyopekea watu wengi kuingia kwenye siasa kusema kweli sio kuleta maendeleo ya nchi bali wengi wao ni kupata faida binafsi na hawajali kabisa kuhusu utaifa na Taifa ambalo ni muhimu pia na kwao, Taifa hili likikosa mwelekeo sisi sote tutakosa mwelekeo. Tutambue kwamba sisi tulio duniani sasa hivi tunatengeneza maisha ya generation ijayo na kama tumeamua kuwa Taifa kutoka makabila mbambali sisi ni Taifa na lengo letu ni moja kuhifadhi kizazi chetu na kujiletea maendeleo yetu sote.



”Tukikumbuka kwamba mafanikio ya pamoja huleta furaha ya Taifa zima na kila mtu atafarijika na kila mtu anastahili heshima katika Taifa lake mwenyewe”



Sasa ni wakati wetu wa kubadili fikra zetu jinsi tunavyofikiri kuhusu Taifa letu, Tunalibomoa wenyewe na hakuna atakayeathirika zaidi yetu, tukumbuke kwamba hatuna ardhi nyingine zaidi ya hii tulioachiwa na mababu zetu na jukumu letu ni kuangaliana na kujaliana na sio kuharibu Taifa letu.



Tunavyofanya sasa ni hatari sana ni sawasawa na kukata Tawi ambalo tumekalia tutaanguka hakuna kitu chochote utakacho mfanyia mtu wa Taifa lako ambacho hakita kurudia kumbukeni ya kwamba sisi ni ”Taifa” which means we are one and we share the same destiny.
 
Back
Top Bottom