AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,190
- 18,080
Habari wana JF na Watanzania kwa Ujumla.
Kama ilivo wazi kwa wadau na wanaharakati wa Siasa hapa inchini, Moja ya eneo of Great interest katika Masuala ya Siasa ni kubadilishwa/kurekebishwa kwa Katiba. Kwa ufupi katiba ni Moja ya kiungo muhimu katika kuendesha shughuli kiufanisi hasa zinazogusa kundi la watu kwa mapana katika nyanja zote husika ili kuweza fikisha lengo kuu la hicho chombo kwa maslahi ya Wahusika (hicho chombo kiwe shirika/kundi/Chama/Serkali n.k). Kwa kuangalia angle moja wapo; Umuhimu wa Katiba na Umanufaa wake kwa Watanzania. Bila kujali ushabiki wa chama husika cha mtoa maoni. Kwa kutegemea michango na maoni yalo huru na kuzibwa/gubikwa na chuki dhidi ya Chama kingine... Hii hasa nikilenga wana CCM na CDM.
Uzuri wa kuhusu katiba yetu ya hapa Tanzania ni kua walioweengi wanaelewa kua katiba ina Mapungufu makubwa ambayo inabidi yabadilike/rekebishwe kwa jinsi yoyote ile – hasa kama malengo ya hio katiba ni kuwagusa Watanzania wengi katika nyanja mbali mbali na kwa pamoja. Ingawa pia kuna upande wa pili wa shilingi... Na hio ni Ubaya. Ubaya kuhusu hio utambuzi wa hio katiba yetu ni kua katika hilo kundi la wengi waelewao na tunaokubali/kugombea/shabikia kwa nguvu zoote katiba ibadilishwe/rekebishwe ni wachache ambao kweli tunaelewa yale yalo ya Msingi katika (ki)Viini cha/vya Katiba hio ambacho(vo) huleta/changia Matatizo katika maeneo mbali mbali ya sasa kwa Mtanzania; hasa wa kawaida – ili kuweza kweli kua na katiba ambayo wengi wataikubali kua "Sasa yafaa"; na sio kukubali tu – bali pia ionekane kwamba kweli Katiba ipo kwa ajili ya kuwakilisha Watanzania pale kiutendaji.
Interest yangu ipo kwa Wanaharakati na wadau wa Siasa na mawazo yao katika Suala zima la Kubadilishwa/rekebishwa; Taking note and baring in mind kwa kuacha pembeni kwanza blah blah za kusema kua kila Mtanzania ana haki na anatakiwa kushirikishwa ndipo katiba ibadilishwe.. (Ni maoni ya Msingi na Mazuri – likitatizwa na ukweli kua bado saana Wanachi kujua hasa nini kipo katika katiba, na nini/wapi hasa hupelekea/changia matatizo katika jamii). Hii inapelekea Uhalisia wa wazi kua tukitaka iwe hivo ndo zoezi liendeshwe baas siku/miezi/miaka yaweza katika kimzaha hivi hivi bila hio katiba kubadilishwa huku mamillioni/malaki ya pesa yakipotea bila efficiency wala end result ya kuridhisha katika jina la kukusanya maoni toka kwa wananchi.
Sasa baas Maswali ya Msingi ambayo naamini wanaharakati na wadau wa Siasa wanauliza na kujiuliza pia ni kama; Watanzania wangapi wanajua Katiba ni nini? Wangapi wana utambuzi wa katiba kua ina husika/changia vipi katika kuendesha inchi? Wangapi walikua hata hawajui kua kuna katiba mpaka hapa karibuni ambapo kumekua na habari lukuki katika vyombo vya habari? Tukiachana na Mtanzania wa Kawaida wasomi wangapi hata wana interest na mambo ya Katiba? Katika idadi ya Wananchi ambao wanafuatilia na kutaka kujua hatima-ni wangapi wana mawazo huru ambayo hayajatokana tu na ushabiki bali kwa utambuzi wa kuijua katiba na kutaka ibadilishwe/rekebishwe kwa kuzingatia na kulenga maeneo husika katika katiba? Kua katiba isha wahi rekebishwa (na mara ngapi na kwa nini na kama hayo marekebisho yalileta mabadiliko tarajia)? Na maswali mengine kibao ya Msingi. Ukweli na Uhalisia wa maswali yoote haya katika haya hii ni kua ni Wachache.... Wachache mno. Sad but true.
Kwa muktadha wa aya hii hapo ya juu; Swala la msingi linabaki kua kama ni Watanzania wachache mno wanaelewa na kutambua majibu ya Maswali haya... Je kuna Matumaini kweli kua kuja kwa Katiba mpya ama ilorekebishwa ndio itafanya Tanzania na watu wake Maisha yabadilike na kua bora zaidi; hivo kua na Tanzania mpya? Na kama jibu ni NDIO... How?
Pamoja Saana
AshaDii.
.