SoC01 Kubadili Mwelekeo ni Katika Njia ya Kufikia Mafanikio, Using'ang'ane na Ulichonacho

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
544
558
Katika maisha kuhangaika ni jambo la kawaida bila kujali wewe ni mfanyabiashara, mkulima, mfugaji, mwanasiasa, mtumishi wa uma, mvuvi, msanii au mwanasanaa, fundi nk. Kila mmoja ana jambo ambalo linamshugulisha ili aweze kuendesha maisha yake ya kila siku. Kupitia shuguli hizo baadhi yetu hupata mafanikio kwa kuyafik amalengo yao na wengine wakiishia kubakia katika hali zao za kawaida huku maisha yakienda, na wengine wakiona mambo hayaendi katika shuguli moja hujiingiza katika shuguli njyingine (code switching).

Kuhama shuguli moja kwenda katika shuguli nyingine ni katika njia mojawapo za kufikia malengo na kwa utafiti mdogo nilioufanya wengi katika waliofanikiwa wamepitia hili la kuhama shuguli. Kuna wakati unafika ukaona shuguli unayoifanya haina tija na haileti mabadiliko chanya kwako, na hata ufanye vipi huwezi kuibadilisha hali hiyo. Kwa akili iliyopevuka itakuelekeza kwenye kufikiria kubadilisha shuguli na wale wenzangu na mimi kwa sababu zingine huendelea na shuguli hizo hizo hata kama hazileti maendeleo.

Katika maisha hakuna shuguli yako, sio kwamba wewe umeumbiw autakuwa mtu Fulani na hivyo kwa shuguli hiyo utakufa nayo. Hapana! Muda wa kuwa upo hai na fursa zingine zipo zitumie, jichanganye kwenye shuguli zingine. Sambamba na hilo usikariri juu ya shuguli Fulani kwa kuwa imemletea mtu Fulani mafanikio ukadhani na wewe utapata mafanikio kwa shuguli hiyo..! hivyo sivyo, mambo hayaendi hivyo! Badilika, maisha hawaigani, maisha hayana kanuni kwamba ukitumia kanuni hiyo basi utafika kwenye jibu sahihi la hasha!

Kubadilisha shuguli kuna faida kubwa sana na ni kichocheo cha mafanikio. Mifano ipo mingi sana tunayoweza kuipiga, kwa haraka haraka muangalie yeyote wa karibu yako aliyefanikiwa katika maisha yake kisha angalia kabla ya hapo alipofikia alikua anajishugulisha na nini? Utakuta alibadilisha shuguli yake na kujiunga/kujishugulisha na shuguli nyingine. Kuna watu walikuwa maarufu kwa shuguli zao mpaka wakapachikwa majina bila kuyaona mafanikio kama vile John Kuku, Side Viazi, Dulla Mayai, Edga Mbao nk. Lakini walibadili shuguli zao na kweli wakaona mwanga wa mafanikio.

Niwashauri wana JF wote na kila atakaesoma bandiko hili, tusiridhike au tusijisahau kunako shuguli zetu tunazojihangaisha nazo hasa pale tunapoona hazileti mabadiliko endelevu. Fanya maamuzi kubadili shuguli kwani huenda kwa kubadili kwako shuguli kukakubadilisha jumla. Kwa sisiwenye Imani ya uwepo wa Mungu muumbaji, tunasema badilika hukuumbwa uwe hivyo tu huenda mafanikio yako hayajawekwa kwenye shuguli hiyo unayofanya. Nenda kwenye shuguli nyingine ukutane na ulichoandikiwa. Wakati mwingine wachawi wa mafanikio yetu ni sisi wenyewe kwa kuwa wang’ang’ani na shuguli moja kama tumechanjiwa. Hivyo kubadili mwelekeo ni katika njia ya kufikia mafanikio, using’ang’ane na ulilonalo utachelewa kufika au hautofika kabisa.

DustBin
 
Back
Top Bottom