Kubadili ajira serikalini ( job recategorazation)

Nicky nicky

Senior Member
Aug 20, 2011
106
9
Poleni na majuku! Binafsi mi ni mwajiliwa wa halmashauri moja kama mwalimu mwenye shahada ya elimu.pia nina post graduate diploma ya ununuzi na ugavi. Nina mambo mawili nayoomba mnijuze; je, kwa kuwa nina post graduate diploma ya fani mpya ninaweza kuruhusiwa kubadili ajira yangu na kuhamia idara ya manunuzi? Pili, ni taratibu gani za kufuata ili zoezi la kubadili ajira likamilike? Naomba kuwasilisha huku nikitumai kupata majibu sahihi. J.tatu njema.
 
Huo utaratibu upo ila tatizo siku hizi ukiritimba ni mwingi sana.

Kuna mshikaji wangu alifanikiwa ila ilimbidi azunguke mbuyu kwa mkurugenzi na maafisa wake ili kumfanikishia.

Nadhani anza kufanya mawasiliano na watu wa kwa mkurugenzi, hii nchi ccm walishaibinafsisha bila rushwa mambo hayaendi.
 
Inawezekana,unaafanyiwa re-categorization ila kwa insu yako labda utumie njia za panya sababu degree yako ya kwanza sio ya manunuzi-huwa wanafuata degree ya kwanza umesomea kitu gani.pili ni lahisi sana kama akidi haijatimia ktk idara/kitengo husika unaongea na Afisa utumishi na mkrugenzi wako.kila la kheri
 
Ndugu,ukisikia maneno ya watu hutafika unapotaka.Recategorization haingalii kama ni masters,au degree,au vyovyote.Maadamu umesomea fani nyingine haijalishi kwa kiwango gani cha elimu,andika barua upeleke kwa mkurugenzi na utabadilishiwa.Acha kutumia watu wala kuzunguka mbuyu,jiamini.
 
YAANI TANGU UZALIWE LEo UMEONGEA KITU CHA MAANA SANA,
KULIKO WENGINE HAPO JUU!
 
Duh!mkuu muundo wa utumishi katika lako hauruhusi hilo,recategorisation inakua based na first degree,PGD ni stahada ya uzamivu.
Unaweza kuwa hujelewa vyema,ngoja nieleze zaidi,ili kuwa recategorised lazima kwanza ikama iruhusu,halmashauri nyingi zina changamoto katika eneo hilo,lakini kama nilivyosema awali ili uwe afisa ugavi II(Supplies officer II) unatakiwa uwe na shahada/stashahada ya katika manunuzi,hivyo muundo unataka Bachelor/advanced diploma,bad thing ni kwamba miongozo ya kitumishi iliopo hairuhusu deviation.
 
upuuzi wa recategorization ni kwamba hata kama ulikuwa principal unarudi kuwa procurement and supplies officer II...mshahara unarudi kwenye level za TGS D ambayo haifiki hata laki nane....gadem
 
Kama ulitaka kua afisa ugavi Kwanini ulisoma ualimu mwanzoni? Anyway Andika barua kwa mkurugenzi wako Kama Akipata upungufu eneo LA manunuzi anaweza Kufanya internal recruitment, ila kama alivosema mchangiaji WA juu hata kama ulifika TGTS E +

UNARUDI KUANZA NA TGS D
 
I doubt kama unaweza kuwa recategorized, labda ufanya manuva ambayo si sahihi. kama alivyoeleza mdau mmoja hapo juu, nafasi ya kazi inaangalia kama ni shahada basi ni shahada ya kwanza, hiyo ndio taaluma yenyewe. saaa wewe huna shahada ya ugavi, then its impossible kuwa recategorized.

Wanaoweza kuwa recategorized ni mf, jamaa yangu m1, alkuwa mwalimu akiwa na stashahada ya ualimu then akaenda kufanya shahada ya uhasibu. alivyomaiza bht wilaya mpya ikawa imeanzishwa na shule aliyokiwa akifundisha ikaangua wilaya mpya then akawa easily recategorized na kuwa mhasibu kwa kuwa kulkuwa na demand ya new employees.
 
Poleni na majuku! Binafsi mi ni mwajiliwa wa halmashauri moja kama mwalimu mwenye shahada ya elimu.pia nina post graduate diploma ya ununuzi na ugavi. Nina mambo mawili nayoomba mnijuze; je, kwa kuwa nina post graduate diploma ya fani mpya ninaweza kuruhusiwa kubadili ajira yangu na kuhamia idara ya manunuzi? Pili, ni taratibu gani za kufuata ili zoezi la kubadili ajira likamilike? Naomba kuwasilisha huku nikitumai kupata majibu sahihi. J.tatu njema.
Mkuu naomba utupe mrejesho ulifanikiwa kufanyiwa recategorization ?
 
Hiyo kiti haiwezekani kwa mujibu wa muundo labda ungerudi kusoma upya first ya procurement!postgraduate hakukupi fursa ya kiwa na ujizi wa taaluma husika,huo ni ubobevu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!mkuu muundo wa utumishi katika lako hauruhusi hilo,recategorisation inakua based na first degree,PGD ni stahada ya uzamivu.
Unaweza kuwa hujelewa vyema,ngoja nieleze zaidi,ili kuwa recategorised lazima kwanza ikama iruhusu,halmashauri nyingi zina changamoto katika eneo hilo,lakini kama nilivyosema awali ili uwe afisa ugavi II(Supplies officer II) unatakiwa uwe na shahada/stashahada ya katika manunuzi,hivyo muundo unataka Bachelor/advanced diploma,bad thing ni kwamba miongozo ya kitumishi iliopo hairuhusu deviation.
Hivi siku hizi kuna chuo kinachotoa advance diploma?? Na sifa zikoje na ni miaka mingapi hadi kumaliza??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru wadau wote kwa michango wenu.Nitafanyia Kazi kadri ya maelekezo.Baraka Tele kwenu
Mkuu Nicky nicky tunaomba utupatie mrejesho ikiwa ulifanikiwa kufanyiwa recategorization au la, na kama haukufanikiwa tuambie sababu ni zipi hasa za kiutumishi.
Shukran.
 
Back
Top Bottom