Kuanzishwa Chuo Kikuu Butiama ni siasa

Kuanzishwa Chuo Kikuu Butiama ni siasa

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
282
Miaka kadhaa imepita tangu Rais Kikwete atangaze kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo huko Bitiama ili kumuenzi mwalimu. Baada ya muda mfupi ikatangazwa kuwa chuo kingine cha kilimo kitaanzishwa huko Katavi. Juzi tena nikasikia habari za Chuo kuanza mwezi March, 2015. Majengo yako na miundo mbinu viko wapi. Ni siasa au ni kitu gani?
 
Mimi na ndugu zangu wa Musoma, akiwamo mleta mada tuna tatizo moja-kusubiri Serikali. Hii habari ingekuwa ni kwa mikoa ya Kagera au Kilimanjaro, siku nyingi chuo kingekuwa kimeshaanza. Michango ingekwishatolewa. Tumebaki kulalamika tu. Serikali hii ukisubiri ikupe unachotaka, unajidanganya.
 
hamasisha wananhi watoe michango hamjachelewa
 
Mimi na ndugu zangu wa Musoma, akiwamo mleta mada tuna tatizo moja-kusubiri Serikali. Hii habari ingekuwa ni kwa mikoa ya Kagera au Kilimanjaro, siku nyingi chuo kingekuwa kimeshaanza. Michango ingekwishatolewa. Tumebaki kulalamika tu. Serikali hii ukisubiri ikupe unachotaka, unajidanganya.

Ndugu yangu Manyerere, suala siyo kulalamika. Suala kubwa hapa ni hadaa inayotolewa kwa wananchi huku wakijua kwamba hawezi kutekeleza. Kwanini wanatoa ahadi hewa?
 
Miaka kadhaa imepita tangu Rais Kikwete atangaze kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo huko Bitiama ili kumuenzi mwalimu. Baada ya muda mfupi ikatangazwa kuwa chuo kingine cha kilimo kitaanzishwa huko Katavi. Juzi tena nikasikia habari za Chuo kuanza mwezi March, 2015. Majengo yako na miundo mbinu viko wapi. Ni siasa au ni kitu gani?

Wanataka kuanzisha chuo kikuu cha kilimo cha BUTIAMA na mie nilishalisikia na mpango huo sina uhakika utatekelezwa lini.
Ila ninachokijua kuhusu majengo ya chuo kikuu hicho ni kutaka kubadili Shule ya Secondary ya Osward Mang'ombe high school (Osward Mang'ombe boys high school) ambayo ni shule ya mchepuo wa sayansi tuu ibadilishe kuwa chuo kikuu.

Binafsi sina shaka na majengo ya ile shule maana ni majengo ya kisasa zaidi ya tunavyofikili, pia ina maabara 3 za sayansi za kisasa naweza sema kuliko shule binafsi nilizowahi kuziona, na ina mazingira bora zaidi, ilijengwa na mbunge wa Musoma vijijini ndg Nimrod Mkono, na hata kama ukiingia google ukaitafuta hii shule utaamini hiki nachokuambia kuhusu majengo ya kisasa na makubwa na maabara ya kisasa.

Hofu yangu ni utekelezaji wa huu mpango ambao hauna dira kuwa utaanza lini hapo ndo nashindwa kujua kwanini Mkoa wa Mara unashindwa kuanzishiwa chuo hiki mapema huku tukijua ule ukanda wa mkoa wa Mara ni ukanda wa mvua na ardhi yenye rutuba ambao hata kama chuo kikianzishwa basi wanafunzi watapata fursa nzuri ya kunufaika na tafiti nyingi za kilimo kutumia ile ardhi.
 
Mbona viongozi wa hicho chuo wameshateuliwa, huna habari?
 
Mimi na ndugu zangu wa Musoma, akiwamo mleta mada tuna tatizo moja-kusubiri Serikali. Hii habari ingekuwa ni kwa mikoa ya Kagera au Kilimanjaro, siku nyingi chuo kingekuwa kimeshaanza. Michango ingekwishatolewa. Tumebaki kulalamika tu. Serikali hii ukisubiri ikupe unachotaka, unajidanganya.
Kagera wamejenga vyuo vingapi?
 
Si na makamu mkuu wa chuo ameshatangazwa! Nasikia ni Prof. Kambarage. Au nayo SIASA?
 
Pole JK kwa miaka 10 aliyokaa madarakani hajaanzisha hata chuo kikuu kimoja. Maana hata UDOM alieanza kujenga ni Ben Mkapa.

JK alikikuta njiani akamalizia???
 
Miaka kadhaa imepita tangu Rais Kikwete atangaze kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo huko Bitiama ili kumuenzi mwalimu. Baada ya muda mfupi ikatangazwa kuwa chuo kingine cha kilimo kitaanzishwa huko Katavi. Juzi tena nikasikia habari za Chuo kuanza mwezi March, 2015. Majengo yako na miundo mbinu viko wapi. Ni siasa au ni kitu gani?

Mkwele ataacha vituko nchi hii!
 
Pole JK kwa miaka 10 aliyokaa madarakani hajaanzisha hata chuo kikuu kimoja. Maana hata UDOM alieanza kujenga ni Ben Mkapa.

JK alikikuta njiani akamalizia???

Acha kujitowa ufahamu ww chuo cha udom ameanzisha kikwete na mh lowasa tena kwakuwatisha wakuh wa hifazzi ya mi f ko ya pension ndio nssf akajitokeza akasema atajenga chuo kile
 
Management ya Chuo-VC na ma DVC wawili wameshachaguliwa na mwezi huu wamereporti wizarani tayari kuelekea Chuoni waanze kazi.
 
VC anaitwa nani? Na hao DVCs ni nani na nani?

Professor Dominick Kambarage (VC) na Prof. Mellau (DVC - Academic) wote hao wametoka SUA DVC Wa mambo ya fedha na utwala simkumbuki jina lakini ametokea ARDHI University. Nimesoma gazeti la mwananchi la tarehe 12 mwezi huu wanasema chuo kinaanza udahili September 2015 na watatumia majengo ya Oswald Mang'ombe na campus nyingine itakuwa chuo cha ualimu Bunda! Tayari hao VC na wasaidizi wake tayari walisharipoti eneo la kazi! Kwa hiyo hii siyo siasa Mzee Wa show amedhamiria!

Hivi vikabila vidogo vidogo vinapenda show sana, wacha ajioneshe!
 
Hivi siku hizi kuanzisha vyuo imekuwa fasheni nn maana kila mtu anataka kuanzisha chuo
 
Udom lenyewe limewashnda,itakua hcho kipya?
 
Wanataka kuanzisha chuo kikuu cha kilimo cha BUTIAMA na mie nilishalisikia na mpango huo sina uhakika utatekelezwa lini.
Ila ninachokijua kuhusu majengo ya chuo kikuu hicho ni kutaka kubadili Shule ya Secondary ya Osward Mang'ombe high school (Osward Mang'ombe boys high school) ambayo ni shule ya mchepuo wa sayansi tuu ibadilishe kuwa chuo kikuu.

Binafsi sina shaka na majengo ya ile shule maana ni majengo ya kisasa zaidi ya tunavyofikili, pia ina maabara 3 za sayansi za kisasa naweza sema kuliko shule binafsi nilizowahi kuziona, na ina mazingira bora zaidi, ilijengwa na mbunge wa Musoma vijijini ndg Nimrod Mkono, na hata kama ukiingia google ukaitafuta hii shule utaamini hiki nachokuambia kuhusu majengo ya kisasa na makubwa na maabara ya kisasa.

Hofu yangu ni utekelezaji wa huu mpango ambao hauna dira kuwa utaanza lini hapo ndo nashindwa kujua kwanini Mkoa wa Mara unashindwa kuanzishiwa chuo hiki mapema huku tukijua ule ukanda wa mkoa wa Mara ni ukanda wa mvua na ardhi yenye rutuba ambao hata kama chuo kikianzishwa basi wanafunzi watapata fursa nzuri ya kunufaika na tafiti nyingi za kilimo kutumia ile ardhi.

Kwa hiyo chuo hakitajengwa tena kyuba na kitahamishiwa Butuguri.? Ninachofahamu eneo lipo tayari na kuna wadhamini walishatafutwa na mbunge mzee mkono lakini mzee mkono amefanya ule mradi wa chuo ng'ombe wake wa maziwa. Kelele za chuo hiki utazisikia tu pindi mda wa uchaguzi ukikaribia.
 
Hahahahaha
Unanifanya nicheke tu, Unakifahamu chuo cha Kilimo Ukiriguru-Mwanza?

Kina Eneo na Madarasa-Lakini hakuna hata mmoja anayekijali.

Kwa hiyo hata hiyo inaweza kuwa Porojo tu. kanda ya ziwa tuna nuksi
 
FI: Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Butiama (Sijajua hasa official name ya chuo ni ipi) kitakuwa na Campus Nne
1. Butiama ambapo ndo itakuwa ofisi kuu na itakuwa na College of Agriculture
2. Bunda Campus ambako kutakuwa na College of Education
3. Musoma Campus ambako kutakuwa na Colleg of Medicine
4. Serengeti Campus ambako kutakuwa na College of Wildlife.

Nimewamegea kidogo kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom