Kuanzisha saccos

Tody's vision

Member
Sep 10, 2011
14
2
Bila kuwapotezea mud me ni Graduate wa IT na ktk kutafuta kazi sioni mafanikio ila nina wazo la kuanzisha saccos ambayo itajumuisha vijana wote wa mahali ninapo ishi tatizo cjui utaratibu wa kuanzisha saccos ukoje na changamoto zake ni zipi? Malengo yangu ni vijana tujijengee uwezo wa kujiajiri hasa ktk kuanzisha kiwanda cha bidhaa za ngozi ila cntopata mtaji kama sina rasilimali za kutosha na njia pekee ya kupata rasilimali fedha ni kuwa na rasilimali watu, mawazo ninayo mengi uwezo ninao mkubwa wa kupanga na kusimamia hata kuendesha biashara nahitaji njia sahii mwenye ujuzi zaidi tafadhali tujuzane zaidi
 
kwanza unatakiwa mjiunge nyie vijana muandae katiba ya chama chenu jina,hisa ni sh ngapi,amana zitakuwaje nk,then mnakutana na mtendaji wa eneo mnamueleza lengo lenu ila kwa ushauri mzuri wasailiana na afisa ushirika wa wilaya unapoishi
 
Unataka kuanzisha saccos au kiwanda cha bidhaa za ngozi? Hujaeleweka hapo.
 
MKUU HONGERA SANA KWA HILI.
- MIMI NINAUSHAURI MDOGO SANA KWAKO, KWANZA NI JIBU HAYA.
1. UKO MITAA GANI? MEANS MKOA
2. MKO IDADI GANI?
3. WOTE MNA MALENGO SAWA? AU NDO WENGINE WAKO KIMASILAHI ZAIDI?

- MKUU KUHUSU SACCOS, MIMI SIPINGANI NA WEWE ILA NATAKA NIELEZE UKWELI KUHUSU SACCOS KWA NYAKATI HIZI

- Mkuu SACCOS kwa sasa hivi zimegeuka kuwa mawakala wa mabenk na zimekamatwa na mabenki, zamani saccos zilikuwa zina sound sana but kwa miaka ya hivi karibuni zimekamatwa na mabenk kama vile CRDB na wao CRDB wana chanel mikopo yao kupitia SACCOS, so inawabidi SACCOS kwa sasa badala ya kutumia riba nafuu kwa member wao wameanza ku adapt riba sawa na mabenk ya biashara,

- Kwa sasa SACCOS nyingi zinapewa mikopo kutoka benki ili ziweze kukopesha wanachama wao, na SACCOS ikisema itoe mkopo wa riba nafuu kwa wanachama wake wakati yenyewe imekopa benki kwa riba ya juu nu uongo, so na wao kwa sasa inabidi watumie riba za juu ili waweze kusavaivu na warudishe mikopo ya benki, Ila kwa sakosi ambazo hazikopi benki hizo hazina shida kabisa katika swala zima la riba.

- So kama mkianzisha SACOOS hakikisheni mnajitoshereza kwa fedha zenu za kutoa mikopo, mkijaribu kwenda kukopa benki mmekwisha inabidi na nyie muanze kutoa mikopo yenye mashariti magumu kama ya mabenki.

-
Kama mko 30 kuna hii kitu inaitwa VSLA Village Saving and Loan Asociation, hii kitu kama mkijiunga mkiwa kama 30mna wote mkawa na nia moja na lengo moja na mkawa mnafahamiana vyema ni kitu kizuri kuliko SACCOS ambazo kwanza zinafuatiliwa sana na Serekari na kuna michango kibao ya kutoa Serikalini kwnye kile chombo cha Serikali cha kusimamia SACCOS.

- Jaribuni hiyo kitu ya VSL ni nzuri sana na inafanana na SACCOS isipokuwa yenyewe haina mlolongo wa mambo ya kwenda kumuona Afisa ushirika, ila proses za kuendesha ni sawa na za SACCOS.
 
I THINK NINA USHAURI TOFAUTI KIDOGO
UME GRADUATE IT RIGHT??
KWANINI USIFANYE BIASHARA INAYOENDA NA PROFESSIONAL YAKO...
i think utafanikiwa zaidi sisemi hautafanikiwa kwa saccos utafanikiwa ila ukifanya biashara inayoendana na professional yako utafanikiwa ZAIDI
mmmh........
 
Siyo lazima mtu afanye biashara inayoendana na proffesion yake....Tena mara nyingi wanaofanya biashara tofauti na proffesion zao hufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko waliozisomea wanafanikiwa zaidi kwasababu kila siku wanapenda kujua zaidi
Got me CTU?
 
Bila kuwapotezea mud me ni Graduate wa IT na ktk kutafuta kazi sioni mafanikio ila nina wazo la kuanzisha saccos ambayo itajumuisha vijana wote wa mahali ninapo ishi tatizo cjui utaratibu wa kuanzisha saccos ukoje na changamoto zake ni zipi? Malengo yangu ni vijana tujijengee uwezo wa kujiajiri hasa ktk kuanzisha kiwanda cha bidhaa za ngozi ila cntopata mtaji kama sina rasilimali za kutosha na njia pekee ya kupata rasilimali fedha ni kuwa na rasilimali watu, mawazo ninayo mengi uwezo ninao mkubwa wa kupanga na kusimamia hata kuendesha biashara nahitaji njia sahii mwenye ujuzi zaidi tafadhali tujuzane zaidi
Habari mkuu
Vp ulifanikiwa kuanza?
 
Back
Top Bottom