Nebuchadinezzer
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,403
- 2,550
- Thread starter
- #41
Hii ni hatari sana mkuu...serikali imelala haipo kwa ajili ya raia bali wawekezaji ambao hawatumii haya maji.Hapo hao watu wa mgodi wanatembeza Mpunga mrefu sana kwa viongozi hii issue huwa naijua vizur sana.
Ngojea nikupe brief Mkuu,
Huwa vyanzo vya Maji kwa Kanda ya. Ziwa inasimamiwa na Ofisi za Bonde zinaitwa Lake Victoria Basin Water Board.
Sasa hao watu wa mgodi wakati wa uchakataji wa madini, moja ya end product ni Yale Maji yenye kemikali za sumu.
Sasa Hawa watu wa mgodi wanachitakiwa kufanya kutokana na utaratibu uliowekwa na mamlaka ni kujengwa bwawa ambalo wataweza kuyapeleka Yale Maji ambayo Yana kemikali, Then yakishaingia kwenye lile bwawa wayatibu.
Then Wakishayatibu Maji kutoka kwenye lile bwawa, Wanatakiwa waje wataalamu wa Lake Victoria Basin Water Board wakague wajiridhishe wameyatibu na hayana madhara kwa binadamu na viumbe vya majini.
Wakishathibitisha ndio utaratibu wakuyamwaga(Draining) kwenye mto au ziwa ndo unafanyika.
Sasa hapo kwenye kuyatibu ni gharama, kwahiyo watu wa Mgodi wanafanya ujanja ujanja wakishikirikiana na Mamlaka husika kufanya izo ishu ambazo zinagharimu maisha ya watu.
Na huwa wanawashikisha hao Jamaa pesa ndefu sana, niliwahi kushuhudia tukio Hilo siwez nikaliweka hapa nitajulikana..
So sad