Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani imefanya uchaguzi wa ngazi ya mkoa.Katika uchaguzi huo ambao ulifanyika Kibaha,Yusuph Kikwete ambaye ni mpwa wa Rais Jakaya Kikwete, alibwagwa vibaya na John Machemba, kwa kuambulia kura 82 tu ya kura 302 zilizopigwa.Labda wote tujiulize swali hili, kubwagwa huku kwa Yusuph kuna maana gani hasa?Kwangu mimi kuna maana moja tu,hii ni kura ya maoni kwa Kikwete binafsi na Chama cha Mapinduzi.Kama hoja za msingi ambazo wananchi zina wakera hazitatafutiwa ufumbuzi, Kikwete kushinda 2010 itakuwa kioja.Kazi kwako Kikwete.