Kuanguka kwa Kikwete Toka Jukwaani, Prof Mwakyusa Ataka Maelezo!

Lakini ni vizuri kasema hili, kwa sababu kesho tunaweza kumshika shati na kumuuliza "Muheshimiwa sana Mbunge Dakta Profesa Waziri vipi ulipata zile habari? Na zinasemaje ?"

hahaaaa... umesahau
Malafyale, chifu, dokta wa nyerere, mtaalam, bosi, sir, mkuu.... lile swali ulilouliza ni la msingi sana, hawa watu hawakujui wewe hawa:confused2:
 
Huyu mzee hajatulia kabisaa, si angewauliza wao. Ugonjwa wao huo, wasituzingue wananchi.
Protocol mbofumbofu!
 
Huyu Mwakyusa naye ni maringo tu. Tangu lini hali ya afya ya Rais ikaripotiwa kwa waziri!

Akumbuke yeye hapo alipo ni waziri wa afya siyo mganga mkuu wa nchi kama anavyoonyesha. Ni mgongano tu kwamba yeye ni waziri ambaye pia ki taaluma ni daktari lakini Anna Abdallah alikuwa waziri wa afya na asingeomba maelezo ya afya ya Rais. Siyo kazi ya Waziri. Hiyo ni kazi ya physician wa Rais.

Kuomba maelezo maana yake aambiwe hata aina ya ugonjwa, hiyo si ni siri ya Rais na daktari wake? Nadhani bado anajiona kama physician wa Rais, kazi aliyoifanya kwa miaka mingi.
 
Anatakiwa kutoa maelezo kwetu akishayapata kutoka kwa daktari wa raisi. Unadhani kwa sasa hivi mwakyusa anaweza akapata wapi kweli majibu ya kutujibu sisi, just in case hajapewa na daktari wa raisi?
Sasa anamuuliza nani???
Ina maana mwasiliano yake na Daktari wa JK yanapitia thru ,agazeti
 
Jamani huo ni unafiki. Waziri kwa vyovyote vile anajua tatizo la rais. Lakini mie kwa hali ilivyo ni lazima rais ana ugonjwa sugu uwe wa kuambukizwa au wakutoambukizwa. Swali ni je tukishajua anaumwa na kwa mfano leo ikathibitishwa officially kuwa ana ugonjwa unaomsababishia kuanguka hadharani na faraghani, je what next? Ajiuzulu? Jibu hapo ni kwamba hawezi kujiuzulu mpaka apende mwenyewe? Na sijui kama kuna sheria inamtaka hivyo. Na kwahiyo hatutaweza kumfanya kitu! Tukae tukijua rais wetu ana chronic condition, lakini hatuwezi kufanya lolote! Na bado kura atapigiwa pamoja na kwamba ni mgonjwa na licha kuli-embarass Taifa. Ndio raha ya ubabe! Haatoki huyo mpaka amalize kipindi chake cha mwisho.
 
Asipoangalia badala ya kumaliza kipindi chake cha mwisho, kipindi chake cha mwisho kitammaliza yeye.
 
Hawa ma prof wanaovamia siasa wanachekesha. Ungekuwepo mfumo ukiwa prof ukaingia kwenye siasa(ubunge na uwaziri) unakuwa degraded academic qualification za u dr na uprof.

Maana mambo mengine wanaongea wanadharirisha qualification. Hajui official channel of communication Au alimaanisha atataka maelezo wakikutana na bar.
 
Hiyo ni namna ya kuomba uwaziri kwa JK mara atakaposhinda! Mbona wazazi wanalala chini wodini baada ya kujifungua na haombi maelezo wala kutoa maelezo? Mbona hayati Nyerere alikufa St. Thomas hospital UK na yeye ndiye aliyekuwa daktari wake, mbona hakuombwa kutoa maelezo? Haelewi kuwa mambo mengine yapo beyond our reach!!!!
 
Mwanamayu umenena ni mbinu za kitoto za kuusaka uwaziri,Profesa amezungumza kabla hajaunganisha ubongo wake.
 
Mi nadhani Profesa Mwakyusa asilaumiwe! alifuatwa na mwandishi wa habari hii. Angeitisha "Press conference" ingekuwa issue nyingine.
 
Back
Top Bottom