Miaka kumi na moja iliyopita nakumbuka ndio nimemaliza la saba nikaenda kijijini kwetu mimi na mama yangu mdogo.
Huyu mama yangu mdogo kule alikuwa na mchumba wake wamepanga waowane basi tulivyofika kule bibi yule akawa siku tatu analala nyumbani siku tatu kwa huyo mwanaume kifupi mapenzi yalikuwa mubashara.
Basi baada ya miezi mitatu ilibidi turudi Dar. Basi bwana yule alimfungashia zawadi za kutosha yule mama yangu mdogo na gunia la mkaa. Akatusindikiza hadi kituoni tukaleta mjini.
Wiki moja baada ya kurudi Dar tukiwa tunatumia ule mkaa tukakuta barua nzito kutoka kwa yule bwana anamwambia mama yangu mdogo kuwa hamtaki tena uchumba umekufa yule mama yangu mdogo alivyopewa ile barua alivyosoma pressure ilimpanda tukampeka hospitali.
Basi ikabidi yafanyike mawasiliano na yule mchumba wa mama mdogo alikubali kuwa kweli ile barua kaweka yeye na kilichoandikwa amemaanisha kabisa wala sio utani.
Hapa nikasema kuna baadhi ya wanaume wamekosa hata chembe ya huruma kama mtu asie na uvumilivu si anaweza kujiua.
Nawasilisha.