Kuachishwa ubunge: Je, wabunge wa kuchaguliwa wana hadhi kuliko wale wa viti maalumu?

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Nimewatafakari wabunge wawili Hamad Rashid aliyekuwa CUF na David Kafulila aliyekuwa NCCR ambao waliwahi kufukuzwa uanachama na kukimbilia mahakamani. Bunge halikukimbilia kuwafukuza hadi pale mashauri yao yaliposikilizwa na mahakama japo sina uhakika kama hukumu ziliwahi kutolewa kabla bunge halijamaliza muda wake. Zamu hii kuna wabunge 8 wa Cuf ambao walitimuliwa chamani lakini wamekimbilia mahakamani na cha ajabu hawa walifutwa ubunge papo hapo pasipo kuisubiri mahakama. Juzikati CCM ilimtimua mbunge Nyalandu chamani lakini bunge lilisubiri hadi Nyalandu alipoongea na press na kujiuzulu ubunge ndipo likaifanyia kazi barua ya CCM ya kumvua uanachama. Ndiposa najiuliza hawa wabunge wa kuchaguliwa Hamad, Kafulila, Zitto na Nyalandu walikuwa na hadhi tofauti kuliko wale wabunge " wakinamama" 8 wa CUF?!!!!... Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom