Mahakama isitumike kulinda wizi, ufisadi na uvunjifu wa Katiba ya JMT

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,225
2,421
Wasalaam.

Nakumbuka july 26 mwaka 2017 aliekuwa spika wa bunge JMT mh ndugai aliwavua ubunge wabunge 8 wa CUF mara baada ya wabunge hao kuvuliwa uanachama na barua ya kuvuliwa uanachama kupokelewa na bunge japo wabunge hao walifungua kesi mahakamani. Spika ndugai alisema nanukuu 'unapovuliwa uanachama moja kwa moja unapoteza sifa ya kuwa mbunge mpaka mahakama itapoamua vinginevyo'

Sasa leo hii inashangaza spika huyu anatafsiri kanuni ile ile kwa namna tofauti na kuwaruhusu COVID 19 kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge kwa point dhaifu ya shauri kuwa mahakamani. Tunakumbuka spika Tulia wakati anakula kiapo aliulizwa juu covid 19 akajibu hajapokea barua ya chadema, leo hii anapokea barua anapata kigugumizi cha nini?

Bunge kuendelea kuwakumbatia na kuwalipa mishahara na posho wabunge feki wasiokuwa na chama ni wizi na ufisadi na ni matumizi ya hovyo ya kodi za watanzania. Haishangazi maana wizi na ufisadi ni jambo la kawaida ndani ya serikali ya ccm lakini watanzania tuna macho tunaona na masikio yanasikia na mungu atawahukumu kwa karama zake.
 

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
30,219
38,705
Wasalaam.

Nakumbuka july 26 mwaka 2017 aliekuwa spika wa bunge JMT mh ndugai aliwavua ubunge wabunge 8 wa CUF mara baada ya wabunge hao kuvuliwa uanachama na barua ya kuvuliwa uanachama kupokelewa na bunge japo wabunge hao walifungua kesi mahakamani...
Mahakama zetu zimeshafanya mambo makubwa na mazito zaidi. Sembuse hayo?
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
11,281
11,962
Wasalaam.

Nakumbuka july 26 mwaka 2017 aliekuwa spika wa bunge JMT mh ndugai aliwavua ubunge wabunge 8 wa CUF mara baada ya wabunge hao kuvuliwa uanachama na barua ya kuvuliwa uanachama kupokelewa na bunge japo wabung...
Hii ndio Tanzania na hii ndio Afrika na weledi wetu wa kitanzania na weledi wetu wa kiafrika
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
210,123
482,161
Siasa za majitaka.. Huyu mupe yure muruke.. Kule waliona kengeza huku eti tulia kaona chongo
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
5,857
7,143
Ni kweli

Profesa Ibrahim Juma, ni lazima ujitafakari kwa makini................

Mhimili wako wa Mahakama, kuendelea kuipindisha sheria, Ili kuendelea kuibeba CCM, ipo siku na wewe utaumbuka!🥺
Nakuona unalalama katika makala nyingi! Kimsingi mtu anakuwa mbunge akiwa ni mwanachama wa chama cha siasa. Akina Halima wataukosa Ubunge kwa vile si wanachama.

Wapo Mahakamani kuonesha kuwa wao ni wanachama! Hivyo ukiwaondoa bungeni ni sawa na kukubali kuwa si wanachama-umeshahukumu: Tulia yupo sahihi mfano ni Zitto na Kafulila, be sober
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom