Kuachishwa kazi (cheti feki) ni swala la fairness, hata Yesu angewaondoa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kumekuwa na minong'ono ya hapa na pale kuhusu uamuzi wa Serikali kuwaondoa kazini mara moja Wafanyakazi wote waliogushi vyeti vyao!

Binafsi naunga mkono uamuzi wa Serikali kwa 100%, na sababu ni moja tu nayo ni fairness, fairness kwa wale wote ambao wametumia muda wao mwingi, akili yao na rasilimali zao kuwekeza kwenye Elimu na kufanikiwa kumaliza masomo kwa Jasho lao dhidi ya wale ambao wamelala nyumbani na wakiutumia muda mwingi kufanya anasa huku wakikimbiza Wanawake kila siku na kuwabadilisha kama nguo halafu kuja kununua cheti na kupata ajira ambazo hawakuzistahili!

Hivyo haihusiani na uzoefu au sijui pension na blah blah nyingine bali ni swala la fairness na fundisho kwa wengine kwamba ktk Maisha hakuna njia ya mkato!
 
Tunataka FAIRNESS hiii hii ipelekwe kwa wanasiasa na viongozi wetu.
Hatuwezi kuongozwa na watu wahalifu wa jinai ya kugushi vyeti na wenye elimu yenye mashaka.
 
Waliotajwa kuwa na vyeti feki, kienyeji wakiacha kwenda kazini watahesabika kama watoro kazini! Inatakiwa waandikiwe barua ya KUWATOA kazini kama ambavyo waliandikiwa barua za kuwaingiza kazini!
 
Hii nchi ni kama nigeria,uwizi,uwongo na utapeli umezidi,na hata sheria zilizoko hivi sasa ni ya kupendelea matapeli,mfano mtu akikimbia na hela yako sheria inasema ukafungue kesi yeye anakoishi,au akikupa cheki hewa,na vyeti feki wanaambiwa watoke tu kwanini wasishtakiwe,unajua hasara ya kuajiri mtu asiokuwa na taaluma miaka nyingi,uchumi wetu haukuwi kwa sababu tuna wataalamu ambao siyo wataalam.
 
Najaribu kufikiria kwa masafa marefu huku nikijiuliza swali, je ni sifa gani kaburi linatakiwa kuwa nazo ili lisifukuliwe? "Sifukui makaburi" hii kauli ni kidhani ni sawa na ule msemo yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo. Kumbe nilikosea kudhania.

Na washawasha!
 
  • Thanks
Reactions: SMU

wakikagua Huko tutawakosa wakuu wa mkoa hasa dar
 
Nani aliwaweka Kazini? yaani Serikali inajipinga yenyewe ajabu
Hii nchi ni kama nigeria,uwizi,uwongo na utapeli umezidi,na hata sheria zilizoko hivi sasa ni ya kupendelea matapeli,mfano mtu akikimbia na hela yako sheria inasema ukafungue kesi yeye anakoishi,au akikupa cheki hewa,na vyeti feki wanaambiwa watoke tu kwanini wasishtakiwe,unajua hasara ya kuajiri mtu asiokuwa na taaluma miaka nyingi,uchumi wetu haukuwi kwa sababu tuna wataalamu ambao siyo wataalam.
 
Najaribu kufikiria kwa masafa marefu huku nikijiuliza swali, je ni sifa gani kaburi linatakiwa kuwa nazo ili lisifukuliwe? "Sifukui makaburi" hii kauli ni kidhani ni sawa na ule msemo yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo. Kumbe nilikosea kudhania.

Na washawasha!
Sheria kwa nchi z kiafrika huwa zinawahusu vidagaa tu. Mapapa haziwahusu! Ile kauli ya waziri Kairuki, ni kauli ya uonevu uliopitiliza. Ni kwa vipi makosa ya jinai yanaanza kuangalia status ya mtu? Ni kauli ya kupingwa na wapenda haki wote. Ningetarajia kuona Bunge likiungana pamoja kupinga uonevu huu wa serikali.
 
Huko nako si salama ubavu wakupinga utatoka wapi!
 
Nani aliwaweka Kazini? yaani Serikali inajipinga yenyewe ajabu
Sheria iko wazi ukigushi siyo unaondolewa kazini,inatakiwa ushitakiwe na kifungo chake ni miaka 7,kujipatia ajiri kwa njia ya udanganyifu,wewe ukitapeliwa haitakiwi umlaumu aliotapeliwa.
 
Hebu vaa viatu vya mtumishi wa umma ambaye ni kati ya hawa 9932. Kakaa katika utimishi takribani miaka 30 sasa kutokana na makosa yake anatakiwa mpaka tarehe 15 mwezi huu awe amendoka kazi.

Upande mwingine mtumishi wa umma aliye iingiza serikali kwenye mikataba mibofubofu na ya kifisadi yenye kapasiti chenji. Yeye anaendelea/kastaafu utumishi analipwa stahiki zake zote na bado anafaudu bakhshishi ya kapasiti chenji kwa raha zake. Eeh mwenyezi Mungu Baba yetu kwa nini maisha hapa duniani yako so unfair kiasi hiki,? tuhurumie Bwana Mungu wetu. Jamani shetani ni mbaya sana na wala hana huruma.

Na washawasha!
 
Back
Top Bottom