Kova unawafahamu Commando Yosso?

tatizo ni serikali haitaki kutengeneza vijana na wasomi watakaokua na uwezo wa kujitegemea mara baada ya masomo ama kuwajengea uwezo wa kujifunza kumudu maisha na si kutegemea ajira za serikali... hapa ndio ninaona umuhimu wa elimu ya ujamaa na kujitegemea (ESR) maana nina uhakika ( by intuition) wengi wa hao vijana itakua ni school dropouts... na waliofeli shule.... swali ni waende wAPI?
 
Kuna wimbo umeimbwa na sugu (mhe.) na solo thang na prof. Jay unaitwa bunduki... Nanukuu maneno ya sugu "tufanye nini sasa au tushike bunduki? Tunakomaa na muziki hamtakii...... Au na sisi sasa tushike bunduki tuwe watu wa mitkasi tupige watu kabali kama komando yosso ndio mtatukubali... " anaendelea kusema mengi ikiwa ni pamoja na wamachinga kunyang'anywa mali zao na polisi... Nini matokeo ya haya yote..? Ndio hao panya buku sasa.
 
Nakumbuka udogoni nikipita maeneo ya faya kabla ya kufika jengo la umoja wa vijana huwa naona chata la komando yoso limeandikwa kwa mchoro mwekundu kama kumbukumbu yangu ipo sawa, hawa jamaa walisikika sana nafikiri panya wanafuata nyendo za hawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom