Sijaelewa uhusiano wa CDADEMA na hili suala la kukamatwa kwa Ponda linatoka wapi, huyu ndiye ambaye anapinga hata Bakwata, yaani Waislam wenzie, huyu ndiye ambaye anapinga hata Baraza la mitihani lakini anaunga mkono mitihani ya dini yake itungwe na kusahihishwa na hao hao anaowapinga, kama Riz1 unaunganisha hili na Uchadema maanake unataka kusema hata Bakwata nayo ni CDM ambayo of course sote tunajua uhusiano wao na magamba ulivyo, anyway, kwa mara nyingine tena tumeona jinsi ambavyo polisi walivyo bias, hivi mtu anavunja sheria then una mbembeleza atii sheria? Hicho nacho kama sio kituko basi ni kitu gani? kwanini hakukamatwa siku nyingi? Hapa tukisema serikali hii ni ya kiislam tunakosea wapi? Mbona viongozi wa kisiasa hasa CDM wakikosea tu hapo hapo mnaleta hadi wanajeshi wa kukodi? tena mara nyingine hata sio kukosea sheria but kukataa kauri zenu za uongo? refer to what happened at Nyororo Village, zipo taarifa kuwa baadhi ya askari walitolewa Mbeya na Dodoma, issue tu kuja kuzuia CDM wasifanye mkutano wao wa ndani! Je kuna watu walioko juu ya sheria na wengine chini ya sheria? CCM ndio chama cha Kidini, tumeona mengi kupitia huyu Ponda, kwanza inasemekana sio Mtanzania, ni Mrundi, sina hakika kama anaishi kisheria, hili nalo tatizo nyingine! Anyway, sababu nadhani mnawaogopa because ndio waganga wenu hawa, mnaogopa wasiwaloge au kuwatupia majini!