Kova: Sasa ninaweza kuwa hata mwanasiasa

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,035
Wakuu habari za sikukuu,

Wakati kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam akitanganza breaking news za kustaafu rasmi jeshi la polisi pale kituo cha television cha ITV pamoja na mambo mengine aliyosema, alisema kwamba sasa anaweza kuwa mwanasiasa akitaka, maana sheria inamruhusu. Hili ndilo jambo ninalotaka tulijadili kwamba endapo ataamua kuwa mwanasiasa;

1. Atajiunga na ccm?, na akijiunga na ccm hii maana yake nini?
2. Atajiunga na Moja ya vyama vinavyounda ukawa?, na je yupo tayari kupata mshikemshike wanaoupata upinzani?
 
Alishakuwa mwanasiasa kabla ya kustaafu na alishakuwa CCM kabla ya kustaafu,tofauti yake ni kwamba sasa ataingia rasmi na jezi za chama.
 
Alishakuwa mwanasiasa kabla ya kustaafu na alishakuwa CCM kabla ya kustaafu,tofauti yake ni kwamba sasa ataingia rasmi na jezi za chama.
Lakini ana haki ya kuhama chama, pengine alikuwa analazimika kuipenda ccm ili kulinda ugali wake?
 
Hivi kuwa mwanasiasa lazima ujiunge na chama cha siasa...??
 
Nchi inatia kinyaa hii,bora ningezaliwa Congo tu nijue moja,kuliko kushudia haya maigizo
Sasa subiri uje usikie kinyaa zaidi utakaposikia ameteuliwa kuwa naibu waziri kule kwa Nape ili kitengo cha wasanii wenzake akisimamie kwa ufanisi zaidi. Ha ha ha
 
Hii sasa kutaka mijisifa ambayo itamtokea puani aiseee....
Huyu mzee akitaka apate amani ya roho na mwili, anapaswa atafute sehem atulieee kama watangulizi wake then alee wajukuu
 
Kada wa CCM wa muda mrefu huyo pia unashangaa nini kama mwanasheria mkuu wa serikali ni kada wa CCM. Hii nchi inahitaji kukombolewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom