Je CCM, IGP na AG, wanashirikiana kukuza mgogoro wa kisiasa nchini?

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Kwa muda wa miezi kadhaa sasa kumekuwa na changamoto ya kisiasa kati ya chama tawala, vyama vya upinzani, jeshi la polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali. Changamoto hiyo inatokana na hali ya sintofahamu iliyoibuka juu ya utendaji na shughuli za vyama vya siasa nchini.

Mgogoro huu ulianza baaada ya Rais John Pombe Magufuli kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano akitaka wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa kujiegemeza zaidi katika shughuli za maendewleo badala ya mikutano ya kisiasa au maandamano.

Agizo hilo lilipelekea Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, maandamano na vikao vya ndani kwa madai kuwa shughuli za kisiasa ni hadi mwaka 20120. Chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vinavyounda UKAWA vikawa wahanga wa kwanza wa agizo hilo. Walizuiwa kufanya mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani wala semina na vikao kazi vya chama.

Mwezi May na June kukawa na mfululizo wa matukio ya kuzuiwa mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa CHADEMA maarufu kama CHASO.

Tarehe 20 mwezi June mwaka huu Jeshi la Polisi mkoani Dodoma ilipiga marufuku mahafali ya vijana wa CHADEMA mkoani Dodoma yaliyokuwa yanafanyika katika hoteli ya African Dream, punde si punde Polisi mkoani Kilimanjaro wakazuia mahafali ya vijana wa Chadema yaliyokuwa yakifanyika katika hoteli ya Keys Mjinin Moshi. Hali hiyo iliendelea kwa mikoa mingine kama Morogoro, Mbeya na Arusha.

Mbali na kupiga marufuku mahafali ya vijana wa Chadema Jeshi la polisi lilizuia pia shuguli za vyama vya siasa za ndani kama semina, au makongamano. Kongamano lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya kufundisha vijana masuala ya ujasiriamali huko wilayani Bariadi katika ukumbi wa KKKT Bariadi Mjini, lilipigwa marufuku na Jeshi la Polisi kwa sababu mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa Mhe.Gimbi Masaba Mbunge wa Viti maalumu (CHADEMA) mkoa wa Simiyu.

Barua ya Jeshi la Polisi ya tarehe 128/06/2016 iliyosainiwa na Mkuu wa Polisi wilaya hiyo SP Thedius Kaihuzi inaeleza kuwa kongamano hilo lilipigwa marufuku kwa sababu Mgeni rasmi ni Mbunge amabaye ni mwanasiasa, kwa hiyo Polisi wanaona kuna dalili kongamano hilo likatumika kuonesha kuwa serikali iliyopo madarakani imedumaza maendeleo ya mkoa huo hivyo kuigombanisha serikali na wananchi.

Lakini katika hali ya kushangaza Jeshi la Plolisi halikuzuia mkutano mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) wa kumchagua Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho. Badala yake Jeshi la polisi liliwakingia CCM kifua kwa maelezo kuwa ni mkutano wa ndani. Hali hii ilifanya vyama vingine vya siasa hususani Chadema kuhisi CCM inapendelewa na wao wanaonewa hasa kwa kuzingatia orodha ya matukio mbalimbali ya kuzuia mikutanoi yao na hata vikao vya ndani.

Hii ilipelekea Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kutangaza kwenda Dodoma siku ya mkutano mkuu wa CCM kuzuia mkutano huo ili kuweka hali ya usawa kwa vyama vyote vya siasa nchini. Hali hii ilizua taharuki miongoni mwa jamii lakini vijana hao waliendelea kujipanga hadi pale Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alipotoa wito kwa vijana hao kusitisha mpango huo.

Lakini yote haya yanatokana na hali ya upendeleo wa waziwazi wa kimaamuzi katika mamlaka zinazosimamia sheria nchini. Jeshi la Polisi limeshiriki kuwakamata wanachama na wafuaasi wa vyama vya upinzani waliojaribu kufanya mikutano au makongamano wakati huohuo jeshi hilohilo likiruhusu mikutano na makongamano kwa wafuasi na wanachama wa chama cha mapinduzi. Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG) nayo imeshiriki katika sakata hili kwa kuwafungungulia mashtaka na kuwafikisha mahakamani wafuasi na wanachama wa vyama hivyo.

Rais Magufuli akatoa maelekezo mengine akiwa wilayani Ikungi kwamba wanaopaswa kufanya mikutano ya kisiasa kisiasa ni wabunge wa majimbo husika tu na sio wabunge wa maeneo mengine au watu wasio wabunge.

Lakini vyama vya upinzani vimekuwa vikijitetea kuwa kufanya mikutano, makoingamano ni haki yao ya kisheria na kikatiba na hakuna mtu awezaye kuiondoa hali hiyo isipokuwa pale tu Rais wa nchi atakapotangaza hali ya hatari.

Kanuni za maadili za vyama vya siasa (2007) zinazotokana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, sura ya 258, sehemu ya 4 inasema “Kila chama cha siasa kitakuwa na haki ya kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi, kutoa maoni ya kisiasa na kueleza sera zake kwa wananchi, kushindanisha sera zake dhidi ya vyama vingine vya siasa, kufanya mikutano ya kisiasa na maaandamano kwa mujibu wa sheria”

Hii ina maana kwamba suala la mikutano au mikusanyiko ya kisiasa ni haki ya kisheria ya wananchi na wanachama wa vyama vya siasa. Sio hisani ya Rais, Msajili wa vyama au Jeshi la Polisi kama inavyodhaniwa. Ni haki inayolindwa na sheria na katiba na hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuifuta haki hiyo, isipokuwa tu pale Rais atakapotangaza hali ya hatari. Sasa imekuaje mikutano ya kisiasa imepigwa marufiku wakati hakuna hali ya hatari iliyotangazwa?

Wakati vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya shughuli zao za kisiasa, chama cha mapinduzi kinaendelea na shughuli zake ikiwa ni pamoja na Rais Magufuli kutumia mikutano mbalimbali ya hadhara kukinadi chama chake. Bila shaka hili ndilo linalofanya vyama vya upinzani kuona kuwa wanafanyiwa uonevu lakini chama cha mapinduzi kinapendelewa.

Hali hii ndiyo iliyopelekea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kuandaa mkutano wa usuluhishi utakaohusisha taasisi za serikali zinazotajwa kwenye mgogoro huu, na vyama vinavyozozana vya CCM na CHADEMA. Pamoja na mambo mengine msukumo wa mkutano huu unatokana na Chadema kutangaza Operesheni UKUTA kwa nchi nzima kuanzia September mosi mwaka huu.

Tume hiyo iliandaa mkutano utakaohusisha taasisi sita, ikiwamo Jeshi la Polisi lililozuia mikutano, CCM inayoendesha Serikali na Chadema inayopinga maamuzi ya Serikali kwa madai kuwa yanakandamiza demokrasia na kukiuka misingi ya utawala bora.

Waliopaswa kuhudhuria kikao hicho ni makatibu wakuu wa vyama hivyo, Abdulrahman Kinana (CCM), Vincent Mashinji (Chadema) na Ernest Mangu (Mkuu wa Jeshi la Polisi), Jaji Francis Mutungi (Msajili wa Vyama vya Siasa), George Masaju (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na Katibu mkuu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Mkutano huo uliitishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Ndg.Bahame Nyanduga ambapo ulipaswa kufanyika Jumatano ya August 10 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Kisheria Tume ya Haki na Utawala Bora ina jukumu la kuhamasisha hifadhi ya haki za binadamu, kuchunguza jambo lolote, kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na kuchukua hatua za kukuza, kuendeleza, usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi.

Lakini katika hali ya kushangaza Chama cha mapinduzi (CCM), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu (AG) hawakutokea kuhudhuria mkutano huo wa usuluhishi ulioitishwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kumaliza mvutano ulioibuka kati ya vyombo vya dola na Chadema.

Hatua hii ya vyombo vya dola pamoja na Chama cha mapinduzi kushindwa kuhudhuria mkutano huo ni dalili kuwa hawako tayari kutafuta utatuzi wa mgogoro huo. Hii inaweza kuwa hatua mbaya katika ukuaji wa demokrasia nchini.

Jeshi la Polisi limekuwa likijinasibu kila mara kuwa ni walinzi wa usalama wa raia na mali zao. Sasa mbona wanaona dalili za usalama wa raia kuharibika na hawataki kuchukua hatua? Au wanasubiri hadi September mosi ndipo waanze kuchukua hatua? Kwanini Polisi hawataki kuzuia mgogoro badala yake wanataka mgogogro utokee ndipo wahangaike kuutatua?

Polisi wamekuwa wakizuia matukio mbalimbali ya kijamii kwa taarifa za kiitelijensia. Je hawajapata taarifa za kiintelijensia kuwa September mosi hali ya usalama inaweza kuzorota kama wasipochukua hatua? Sasa kwanini wamekataa kushiriki katika mkutano wa usuluhishi? Wanapenda kuona mgogoro huu ukiendelea?

Chama cha mapinduzi, Ofisi ya mwanasheria mkuu, kwanini nao hawakushiriki? Kutokushiriki kwao kunaleta tafsiri kuwa wamedahamiria kutotafuta suluhu ya mgogoro huo. Ikiwa CHADEMA pekee ndio waliotuma uwakilishi katika mkutano huo wa usuluhishi, ina maanisha kuwa ni CHADEMA pekee wenye dahamira ya kweli ya kutafuta suluhu la mgogoro uliopo.

Je CCM, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwanasheria mkuu ambao ni wadau wakuu wa mgogoro huu hawataki kuona mgogoro huu ukiisha? Kitendo cha kutohudhuria mkutano wa usuluhishi ni dalili kuwa kuna agizo lililowazuia kushiriki. Haiwezi kuwa bahati mbaya. Je ni nani aliyeagiza wasishiriki kikao hicho muhimu?

Kwa kawaida katika hatua za utatuzi migogoro hatua ya kwanza ni kukaa na pande zenye mgogoro na kusikiliza kila upande kabla ya kuruhusu mjadala wa pamoja. Kwahiyo kukutana kwa pamoja kwa pande zinazozozana nia hatua ya kwanza na ya msingi sana katika kutatua mgogoro. Bila kukutana hakuna lolote linaloweza kufanyika ili kutafuta suluhu.

Wataalamu wa utatuzi wa migogoro wanaeleza kuwa ikiwa pande zinazozozana zimekubali kukutana ni dalili nzuri ya kutafuta suluhu. Upande usiokubali kushiriki kwenye hauko tayari kuona mgogoro ukimalizwa. Hii ni kusema kwamba CCM, IGP na AG hawapo tayari kumaliza mgogoro wa kisiasa uliopo nchini.

Hii haiwezi kuwa habari nzuri katika mchakato wa ukuaji wa demokrasia. Pia ni aibu kwa chama tawala na taasisi nyeti kama jeshi la polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu kukataa kushiriki katika mkutano wa usuluhishi. Kwanini hawakushiriki? Nani aliwazuia? Kwa nia gani? Huyo aliyewazuia (kama yupo) je yupo tayari kuona damu za watanzania zikimwagika endapo machafuko yatatokea? Tafakari.!!

________________________________________
Imechapwa; #JamboLeo August 16, 2016.

Malisa G.J
 
Hakuna mgogoro wa kisiasa sana sana kinachofanywa na CHADEMA ni mbinu ya kuzika hoja kuu waliyokuwa nayo kwa zaidi ya miaka nane ya kupinga ufisadi. Sasa wamekula matapishi wanatafuta namna ya kubadili upepo na kufanya watu wasahau walikuwa wanasema nini huko nyuma.
 
Subirini muafaka
 
Are you sure?
 
Hakuna mgogoro,Chadema wameshaona watashindwa kuandamana tar 1.sasa wanalazimisha kusuluhishwa...endeleeni na msimamo wenu na mkiandamana tarehe 1 mtakula virungu mtavunjwa viuno mshindwe kutembea ili kukitokea maandamano mengine muandamane kwa kutambaa.
 
KWA NINI IGP, AG, CCM HAWAKUPASWA KUKUBALI KUITWA NA TUME YA HAKI ZA BINADAM

By:- William Malecela

Mwanafalsafa maarufu wa Ufaransa Baron De Montesquieu mtalamu wa Sheria pamoja na masuala ya utawala katika Ulaya mnamo karne ya kumi na nane aliwahi kuainisha aina tatu za tawala katika Mataifa, Aina ya kwanza ni tawala za Kifalme (Monarch) zinazoongozwa na Wafalme au Malikia, tawala za pili ni zile tawala za Kijamhuri (Republic) ambazo huongozwa na kiongozi mkuu wa nchi ambaye huchaguliwa na wananchi na aina ya tatu ni zile tawala za Kiimla au kidikteta (Depotism). Tanzania tunaongozwa kwa kutumia Tawala ya Kijamhuri ambapo Rais na Chama Tawala huchaguliwa kwa kura za Wananchi. Pia tunajiongoza kwa kutumia Demokrasia ambayo mahali popote Duniani huongozwa na Sheria, na Serikali huongozwa na Taasisi inayoitwa Dola ambayo inahodhi mamlaka tatu muhimu Serikali, Bunge na Mahakama. Mihimili hii mitatu inaundwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kuanzia Kipengele cha Pili mpaka cha Sita ambapo umetolewa ufafanuzi wa kina namna Mihimili hii inavyotakiwa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mwingine kwa manufaa ya umma.

Tanzania pia tunajiongoza kwa kutumia Demokrasia ambapo kila mwananchi anakuwa na haki ya kusikia na pia kupewa haki zake zinazolindwa Katiba. Ndio maana Serikali yetu Mwaka 1977 kwa kutumia Katiba ya Jamhuri Kipengele Namba 129 iliunda rasmi Tume ya Haki za Binadam na Utawala bora (CHRAGG) kama chombo chake huru cha kulinda haki za wananchi na kusimamia utawala bora pamoja na kuchunguza malalamiko ya ukiukwaji wa haki za wananchi na hata kwenda kwenye Sheria inapobidi. Rais wa Tanzania ndiye Amiri Jeshi Mkuu ambaye moja ya kazi zake ni pamoja na kusimamia vyombo vya Dola na kuhakikisha Sheria zilizotungwa na Bunge zinatekelezwa kwa mujibu wa Katiba, kwenye kulitimiza hilo Rais huteuwa wasaidizi wa kumsaidia kwenye kazi hizo. Kwa hiyo linapotokea tatizo lolote la Kitaifa au Kisiasa linatakiwa kufikishwa aidha Mahakamani, Bungeni au kwenye Dola, lakini sio mahali popote pengine. Kama ni tatizo la Vyama vyetu vya siasa Katiba ipo wazi kwamba Msajili wa Vyama vya saisa atahusishwa namna ya kulimaliza au kuishauri Serikali namna ya kulimaliza kama kweli lipo tatizo.

Kwa mantiki hii basi kitendo cha Tume ya Haki za Binadam na Utawala Bora kuwaita Mkuu wa Polisi na Mwanasheria Mkuu hakihalalishwi mahali popote kwenye Katiba yetu, na hata kuwaita CCM na Chadema waje meza moja bado sio kazi yao inatakiwa kuwa kazi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kwa hiyo kitendo cha CCM, IGP na AG kutohudhuria kikao hicho ni halali kabisa kwa sababu IGP na AG ni wateule wa Rais au Mhimili wa Dola sasa Dola inaitwaje na Tume tu ni kichekesho kikubwa sana kwa utawala tunaofuata wa Demokrasia na mgawanyo wa madaraka kwa Mihimili Mitatu mikuu ya Taifa.Tume ya Haki za Binadam na Utawala Bora haina mamlaka Kikatiba ya kuwaita wateule wa Rais kwa ajili ya kuwahoji namna wanavyotekeleza wajibu wao kwaa melekezo ya Kikatiba chini ya Rais wa Jamhuri. Lakini Tume hiyo inaweza kwende mahakamani au kumshauri Rais iwapo itaona kuna tatizo la ukiukwaji wa haki za wananchi ambao mpaka sasa haujatokea bado isipokuwa kuna uvunjwaji mwingi wa sheria ambao umekuwa ukifanywa na Wapinzani kwa kisingizio cha kubanwa Demokrasia.

Na mwisho ni kwamba hakuna tatizo kama tatizo ambalo litashindwa kutatulika kwa kukataa kwa CCM, IGP na AG kuhudhuria kikao hicho cha Tume kuwakutanisha na Chadema, hapana lililopo ni uvunjwaji wa Sheria unaofanywa na Chadema ambao vyombo vya Dola vimekuwa imara sana kwenye kuthibiti tatizo hilo. Ninarudia tena kama lipo ni tatizo linalotakiwa kumalizwa na Sheria, lakini sio mkutano kama huo uliopangwa na Tume ya Haki ambayo huenda hapa inaweza kuwa imepitiliza mipaka yake ya kikazi Kikatiba. Iwapo wangekubali kuhudhuria kikao hicho basi Kikatiba ingeleta hata mgogoro wa Kikatiba kwa sababu ingemaanisha Tume hiyo kuwa juu ya Dola, Bunge na Mahakama vyombo vitatu vikuu ambavyo pekee tu ndio vina uwezo wa kuwaita wahusika wote hao lakini sio Tume ya Haki za Binadam na Utawala Bora kwa sababu hawana hayo mamlaka.

BY: William Malecela.

IMECHAPWA NA GAZETI LA JAMBO LEO TAREHE 16/8/2016 UK/14
 
Subirini muafaka
Sisi wengine tunatumia simu za button na intanet ya bure.
Unapo-qoute uzi mrefu nama hii halafu unaandika maneno mawili, unatutesa sisi wenye simu za buttton na za bei rahisi. Unatufanya tuanze kuupitia tena uzi hali inayofanya tuachane nao.
Samahani kama nitakuwa nimekuudhi.
 
Back
Top Bottom