Unapokataza watu kuandamana kisa Al-Shaabab ni ishara tosha kwanza hao jamaa wapo hapa nchini.
Pili huo uwepo wao ni kwamba polisi imeshindwa kuwazuia wasiingie nchini,
Tatu wameshaingia, pia umeshindwa kuwazuia wasilete madhara.
Mikusanyiko iko mingi tu, si lazima iwe Maandamano ya Dowans.
Mbona wakati wa Kampeni za Siasa hawazungumzii Al Shaabab? Kwenye masoko makuu ya Nafaka kama Tandale, Urafiki, Tandika, Kariakoo kote huko mbona hawazngumzii hao Al Shaabab?
Ubungo Bus Terminal, Mwenge, Mbagala kote huko kuna mikusanyiko mikubwa ya watu, hao Alshaabab hawawezi kufika?
Jumamosi inayokuja kuna Mechi kati ya Simba na Yanga ambapo takriban watu Alfu 50 au zaidi wanategemewa kuingia, hakuna uwezekano wa hao Alshaabab kuwepo?
Yani hao Alshaabab wapo kwenye maandamano ya Dowans tu??!!!!
Kwanza kama kweli wapo, hao Alshaabab wakitaka hata hiyo mikusanyiko yao ya miaka 50 ya uhuru wa bendera watailipua tu.
Napata mashaka na uwezo wa huyu Mzee, kwani amekua mtu wa majigambo mengi kuliko uhalisia wa kitu.