Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Ndio tatizo la polisi ku-recruit watu wenye elimu fupi na ndogo....MwanaHalisi kaandika kuwa Polisi wetu hua wanaacha akili zao nyumbani...Naona kama vile ni kweli eeehh!
 
hii ndio Tanzania, tunaadhimisha miaka 50 ya UHUNI bila hata ya kuwa na uhuru wa kujiexpress! Hao Al shaabab wamehamia Tanzania lini au ndo propaganda za kutuzuia kusambaza sumu za ANTI-DOWANS tu. Wana intelijensia watakuepo kutulinda.
 
katika moja ya post zangu leo asubuhi nimesema

'' nimesikia kuna maandamano yanafanyika dar jumamosi juu ya kupinga dowans na ufisadi....ningeshauri maandamno yafanyike nchi nzima lakini nasikia leo jioni au kesho asubuhi watakuja na tangazo la kusema habari za kiintelijensia zimesema kundi la alshabaabu linaweza kulipua dar mda wowote na hivyo kuyasambaratisha maandamano......maana wanasema toka ubungo hadi huko jangwani ni parefu mno so wanahisia machafuko ili kuwatisha watu watatoa vitisho vya alshabaab....''
jana walitka kulisema pale wakati mwema anaongea na na waandishi wa habari lakini wakaihilisha na leo ndo huyo kova kabwatuka....wanadai haya yatakuwa maandamano makubwa kama yakifanyika na hunda yakaibua kitu kingine ikiwa ni pamoja na kumtaka raisi ajiuzuru...so wamtumia kigezo cha alshabaab kama sababu na hata jana mwema kuliongelea swala hili ilikuwa ni mkakati wa kulifanikisha leo...
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....
al shabaab inahusiana vp na dowans?kuna watu wanafikiria na masaburi sana
 
Naombeni sana haya maelezo yake yakae vizuri kwenye kumbukumbu ile keshokutwa wakisema hakuna Alshabab tumsute kwa ndimu....
 
Umefika wakati viongozi waache kutumia MASABURI kufikiri.
 
wajuaje, labda alshaabab wanaunga mkono dowans, LOL:crutch:
Ukichunguza sana unaweza kuta al shabaab wana uhusiano na wamiliki wa Dowans mana hata andiko la Mwakyembe polisi, lilionesha ushiriki wa watu wanaohisiwa kuwa ni al shabaab katika kupanga njama za kumdhuru. So inawezekana wametaarifiwa kuwa waTZ bado tunaleta utata juu ya hayo malipo. So inawezekana Kova na Serikali wanawatumia Al shabaab katika uhalifu wao.
 
Nguvu ya umma jamani tupooooooo!!!!! Hawa magamba watatutambuga siku si nyingi! Leo Kova anakubaliana na wizi unaoendelea macho macho? Jamani nimeanza kuchafukwa na roho kbs! Ngoja ntarudi na mapya. Shwine kabisa Kova!!
 
Nashauri hata wizara zisitishe sherehe za upuuzi wa Tanzania ili kupunguza mikusanyiko kwasababu ya Tishio la wanaume wenzao!!!!!!
 
Mkuu nafikiri hata hizi sherehe za 50 ya uhuru wa (Tanganyika) wao waita Tanzania tusimamishe pia !


swali dogo tu wakati wa bajeti inasomwa ulisikia bajeti ya miaka 50 ya uhuru? sasa hivi kila wizara inafanya kufuru ya sherehe hizi na kwenye bajeti sikusikia mwakani january nchi itakuwa haina pesa
 
Wee Kova na hao waliokutuma kuzungumza upupu! BADO TU HAMJAJIFUNZA KWA GADDAFI! Unafikiri hiyo ndiyo hekima ya kuzuia maandamano? Sisi ni Great Thinkers bwana!
 
kwani Al adawi anauhusiano wowote na Al shabab ?
 
kova hana uwezo wa kuwazuia kuandamana. waendelee na maandamano yao...labda intelijensia imewaambia huo ndo utakuwa mwanzo wa mwisho wa dola ya ccm...
 
kwani yule mmliki wa dowans kutoka uarabuni sio al-shababa??yawezekana ni kweli.basi intelijensia ya polisi ina apply arusha tu kwenye maandamano.
 
Back
Top Bottom