Kova: Jerry Muro kuchunguzwa kwa hate crimes dhidi ALBINO. Ashangazwa na kimya cha DRFA na TFF

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
Kuna taarifa kuwa si mara ya kwanza kwa Jerry Muro kutoa matamshi ya vitisho na kashfa dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) . Polisi mkoani Dar wamesema kuwa Jerry Muro anaweza kushitakiwa kwani matusi na vitisho dhidi ya Hajji Manara ambaye pamoja na kuwa ni hazina ya Taifa hili kwenye medani ya soka pia ni mlemavu wa ngozi (Albino) zinaangukia kwenye hate crime achilia mbali matusi yake dhidi ya kabila na section ya jamii.

Lakini pia Polisi Mkoani Dar wameshangazwa na kimya kutoka kwa Jamal Malinzi wa TFF na Almasi Kasongo wa DRFA na hii inaonekana kuwa Jamal Malinzi na Almasi Kasongo ambao wana asili ya mikoa ambayo mauaji ya alibino yanafanyika kwa kiasi kikubwa kuonekana kuwa wana muunga mkono Jerry Muro.

Taarifa zaidi juu ya tukion hili mtaziona kwenye ukurasa wa Polisi Mkoani Dar.
 
Nini maana ya WATANI WA JADI?
Huyo Kova bila shaka ni shabiki wa Simba,sasa vidonge vya Jerry vimemchoma analeta ubabe katika utani.
Jerry hana maana yoyote zaidi ya utani wetu wa jadi baina yetu Mabingwa tusiofungika Young Africans dhidi ya Wachovu S.C Simba.
cc GENTAMYCINE
 
Last edited by a moderator:

duuh tuseme yanga mmeunga mkono?
 
Last edited by a moderator:
Nina wasiwasi na IQ ya Kova au ka anajitoa fahamu na kutumiwa na timu pinzani. Suala hilo nadhani Jerry alizungumza kama anaingea na mtu wa mpira na si mlemavu wa Ngozi.Isitumuwe huruma ya ulemavu wa Ngozi tuangalie the concept ya Jerry Muro!
 
Nini maana ya WATANI WA JADI?
Huyo Kova bila shaka ni shabiki wa Simba,sasa vidonge vya Jerry vimemchoma analeta ubabe katika utani.
Jerry hana maana yoyote zaidi ya utani wetu wa jadi baina yetu Mabingwa tusiofungika Young Africans dhidi ya Wachovu S.C Simba.
cc GENTAMYCINE

Kumbe na ww unapenda mpira? Tena yanga
 
Last edited by a moderator:
Nina wasiwasi na IQ ya Kova au ka anajitoa fahamu na kutumiwa na timu pinzani. Suala hilo nadhani Jerry alizungumza kama anaingea na mtu wa mpira na si mlemavu wa Ngozi. isitumuwe huruma ya ulemavu wa Ngozi tusiangalie whats the concept!

Una akili sana wewe.
Ila hapo mwisho rekebisha mkuu,nadhani ulimaanisha "Tuangalie what's the concept (Ya Jerry)"
 
duuh tuseme yanga mmeunga mkono?
Mambo ya mpira hasa utani nani asiyeyajua?
Vijembe katika mpira vipo duniani kote.
Unakumbuka vita ya maneno kati ya Mourinho vs Fergie?
Mourinho amewahi muambia Prof. Wenger ni special failure,ilikuwaje?
Kila mtu alichukulia utani yakaisha.
 
Hapo naona hakuna uhusiano wowote na kutukanwa kwa maalibino, mh Kova yeye aimalishe ulinzi kwa hawa ndugu zetu, wasikatwe viungo vyao tena, wala kutolewa uhai wao kwa imani za kishirikina. Mwaka jana nilienda kuchoma sinda ya homa ya manjano pale mnazi mmoja, nikiwa kwny foreni walikuja watoto kama 10 wenyenye ulemavu wa ngozi, wakiwa wamekatwa viungo vyao, walikuja kuchomwa sindano, walikuwa wanaenda Marekani kuwekewa viungo vya bandia. Kiukweli nilivyowaona, na kuhadidhiwa yaliyowakuta, nilitokwa na machozi.
 
Nini maana ya WATANI WA JADI?
Huyo Kova bila shaka ni shabiki wa Simba,sasa vidonge vya Jerry vimemchoma analeta ubabe katika utani.
Jerry hana maana yoyote zaidi ya utani wetu wa jadi baina yetu Mabingwa tusiofungika Young Africans dhidi ya Wachovu S.C Simba.
cc GENTAMYCINE

ubaguzi wa rangi haukubalikh...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom