DC Jerry Muro umeusoma ujumbe huu na ukalinganisha na majukumu yako? Jiandae

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Naomba tusome hii story ya Jerry Muro akijitetea baada ya kumkamatwa wakili nakumweka ndani kinyume kabisha na sheria.

DC anadai alifanyiwa vurugu, kwa Jerry Muro huyu afanyiwe vurugu tusione clip mtaani? Hata Wananchi anaowasingizia wasipige hata picha? Vijana mnapewa madaraka kwanini mnayatumia kunyanyasa watu kwa kisingizio Cha kusaidia watu? Kwanini usiwaelekeze watu wakaripoti polisi au waende mahakamani au mabaraza ya ardhi? Watu wote wenye migogoro ya familia wakipanga foloni kwa DC kazi zitafanyika? Ningekuwa na mamlaka kwa stori hii naunda tume then natumbua akajifunze namna ya kuishi na watu. Hawa mawakili nao sijui huko shule wanafundishwa Nini Kama wanashindwa kumfungulia huyu mashtaka kwa matumizi mabaya ya ofisi na kutengeneza stori zisizo na justification


UFAFANUZI WA KUKAMATWA KWA WANASHERIA WAWILI NDUGU MERINYO ARUMERU

Siku ya Alhamisi Tarehe 06/05/2021 Mzee Godwin Siokino Merinyo alifika ofisi ya Dc Arumeru akiwa na kero ya Jirani yake Mzee Nelson Siokino Merinyo ambae ni kaka yake kuwa amepanda miti ya Eukaliptasi jirani na Eneo la choo chake na upande wa pili wa nyumba hatua ambayo miti hiyo imeanza kuleta madhara katika choo na upande wa nyumba yake

Hapa mgogoro ulikuwa kati ya Ndugu wawili Mzee Godwin Siokino Merinyo na kaka yake Wakili Nelson Siokino Merinyo mgogoro wa miti ambayo inatishia usalama wa eneo la mzee Godwin Siokino Merinyo

Jambo hili limezungumzwa kwa nyakati kadhaa katika ngazi ya kijiji na kata na kukosa muafaka ndio ikabidi liletwe ofisini kwa Dc kwa utatuzi

Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ilipanga siku ya jumamosi Tarehe 08/05/2021 kwenda kusikiliza mgogoro katika eneo la tukio Ngaramtoni kona na wahusika wote walitakiwa kuwepo katika eneo la tukio

KILICHOTOKEA
Mkuu wa wilaya alifika eneo la tukio na kuanza ukaguzi wa eneo husika, mara baada ya ukaguzi tukataka kuanza kikao tukiwa na wananchi wa maeneo hayo lakini cha kushangaza Mzee Wakili Nelson Siokino Merinyo hakuwepo hivyo Dc akaomba baadhi ya wahusika waambatane kwenda nyumbani kwa Mzee wakili Nelson Siokino Merinyo kuangalia kama yupo au hayupo mana tusingeweza kujadili mgogoro pasipo pande zote kuwepo mana ni eneo hilo hilo tu ambapo kuna changamoto ya maelewano

NYUMBANI KWA MZEE WAKILI NELSON SIOKINO MERINYO
Tukifika nyumbani na kugonga geti tukiongozwa na mtoto wa mdogo wake Mzee Neslon Siokino Merinyo na geti ikafunguliwa na mwanamke ambae ni mke wa Wakili lesilian Nelson Merinyo na kukaribishwa ndani tukaingia ndani ya geti, Mkuu wa wilaya alijitambulisha kwa majina na wadhifa na kuwatambulisha aliokuwa ameongozana nao na kuomba kujua kama Mzee wakili Nelson Siokino Merinyo yupo, Jibu likatolewa mzee hayupo ndipo mkuu wa wilaya alipoomba kuandika ujumbe kwa mzee apewa atakaporejea

Tukiwa katika hatua ya kuandika ujumbe alikuja kijana wa mzee wakili Nelson Siokino Merinyo anaejulikana kwa jina la Wakili Lesilian Nelson Merinyo na kuhoji tunafanya nini nyumbani kwao pasipo taarifa

Mkuu wa wilaya alijitambulisha tena na ujumbe wake na kueleza kwanini wako pale, pamoja na mkuu wa wilaya kujitambulisha lakini wakili Lesilian Nelson Merinyo hakuridhika na kuanza kutoa lugha kali za matusi na kumfukuza mkuu wa wilaya ambae hata hivyo aliendelea kusisitiza hawezi kuondoka kwa kuwa yuko katika eneo lake la kazi na yuko katika kutekeleza majukumu ya kazi hivyo yeye kama kiongozi anapaswa kuachwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo ya kuandika ujumbe wa kuacha kwa mzee wakili Nelson Siokino Merinyo

Cha kushangaza mbele ya umati wa watu wakili Lesilian Nelson Merinyo akiwa pamoja na ndugu zake akiwemo wakili mwinginr walianza kumshika mkuu wa wilaya kiunoni na kumtoa nje uku akimsukuma kwenye ukuta kwa kutumia nguvu hatua iliyosababisha mkuu wa wilaya kujeruhiwa mkononi na shingoni

Kutokana na kuzidiwa nguvu na kutokana na mkuu wilaya kutoambatana na askari alizidiwa nguvu na kusukumwa nje ya geti na kisha geti kufungwa, ndipo hapo mkuu wa wilaya aliwasiliana na kamanda wa polisi wa wilaya OCD na kuomba msaada wa polisi

BAADA YA POLISI KUFIKA
Baada ya muda mchache askari watatu wa kiume na wakike mmoja walifika uku baadhi wakiwa wamevaa nguo za kiaskari na wengine nguo za kirai walifika na kugonga geti kuomba mlango ufunguliwe

Watoto wa mzee Wakili Nelson Siokino Merinyo wakiwa ndani pembeni ya geti waligoma kufungua geti kwa muda wa dakika 15 ndipo askari walipolazimika kutumia nguvu na kufungua geti wakachukuliwa na kupelekwa kituoni kwa kosa la SHAMBULIO

MSIMAMO WA OFISI YA DC ARUMERU
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru inaalani kitendo cha kushambuliwa kwa mkuu wa wilaya na wana familia ambao ni wasomi na wanajua sheria na wanaojua majukumu ya kazi za mkuu wa wilaya, hii imedhihirisha wazi kuwa familia hiyo imekuwa na matatizo sio tu kwa mkuu wa wilaya hata kwa majirani wanaoishi eneo hilo ambap wengi walionyesha kukerwa na kitendo cha kushambuliwa kwa Dc Arumeru

Ofisi ya mkuu wa wilaya imebaini kuwa katika familia hiyo kumekuwa na matukio mengi ya uvunjwaji wa haki za wananchi unaofanywa na familia hiyo kwa muda mrefu na ndio sababu huenda wakaamua kumfanyia vurugu mkuu wa wilaya

Ofisi ya mkuu wa wilaya inakusudia kuandika barua kwenda chama cha wanasheria Tanzania kuomba hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wanasheria hawa wanaotumia taaluma zao vibaya

Kwa sasa jambo tayari liko kwenye vyombo vya kisheria na ofisi imelicha katika mikono mingine ya uchunguzi na sheria ili haki itendeke

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru
09/05/2021
 
Lengo la maelezo haya yote ni Nini hasa wakati unayo mamlaka ya Kamata weka ndani?

Pili kazi iliyokupeleka uliifanya kwa capacity ipi? Kamati ya usuluishi? Wajumbe wake ni kina Nani? Je ulikua na instruments zipi kukufanya itekeleze jukumu Hilo? Kuingia kwenye makazi ya mtu hata Kama wewe ni kiongozi Kama huna Ruhusu ni kosa. Hujuwa na RB Wala sijui warrant ya mahakama au polisi kwa vyovyote walikua na haki ya kutokukusikiliza Wala kukukaribisha kwenye makazi yao.

Mama alisema " ukinizingua tutazinguana" lakini pia alisema " sijakuchagua uende ukawapandishie mabega"

Mh. Jipime Kama unatosha kwenye hiyo nafasi, jishushe kwa kujiuzulu. Kama mama itapendeza atakurudisha au kukupa kazi ingine Biblia inasema " ajikwezae atashushwa"
 
DC anadai alifanyiwa vurugu, kwa Jerry Muro huyu afanyiwe vurugu tusione clip mtaani? Hata Wananchi anaowasingizia wasipige hata picha? Vijana mnapewa madaraka kwanini mnayatumia kunyanyasa watu kwa kisingizio Cha kusaidia watu? Kwanini usiwaelekeze watu wakaripoti polisi au waende mahakamani au mabaraza ya ardhi? Watu wote wenye migogoro ya familia wakipanga foloni kwa DC kazi zitafanyika? Ningekuwa na mamlaka kwa stori hii naunda tume then natumbua akajifunze namna ya kuishi na watu. Hawa mawakili nao sijui huko shule wanafundishwa Nini Kama wanashindwa kumfungulia huyu mashtaka kwa matumizi mabaya ya ofisi na kutengeneza stori zisizo na justification
Jerry Muro hana mamlaka ya kwenda kusuluhisha migogoro yaa ardhi. Anaweza akatoa ushauri na kuishia hapo. Kuna mahakama za ardhi aziachi kazi yake. Hao wenye migogoro ya ardhi wangelishauriwa kwenda Mahakamani ambapo haki ingelitendeka. Kwanini Jerry/Mkuu wa wilaya anajipa mamlaka asiyokuwa nayo?
 
Ofisi ya mkuu wa wilaya inakusudia kuandika barua kwenda chama cha wanasheria Tanzania kuomba hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wanasheria hawa wanaotumia taaluma zao vibaya
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
 
Jerry Muro hana mamlaka ya kwenda kusuluhisha migogoro yaa ardhi. Anaweza akatoa ushauri na kuishia hapo. Kuna mahakama za ardhi aziachi kazi yake. Hao wenye migogoro ya ardhi wangelishauriwa kwenda Mahakamani ambapo haki ingelitendeka. Kwanini Jerry/Mkuu wa wilaya anajipa mamlaka asiyokuwa nayo?
Now we can witness without fuss 'the load' of stupidity of our dear DC
 
fu na ndio sababu huenda wakaamua kumfanyia vurugu mkuu wa wilaya

Ofisi ya mkuu wa wilaya inakusudia kuandika barua kwenda chama cha wanasheria Tanzania kuomba hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wanasheria hawa wanaotumia taaluma zao vibaya
Hii ni trailer tu picha yenyewe bado, kumbuka kuwa kuvunjwa kwa sheria hakujaanzia kwa hao mawakili
  1. Mwajiri namba moja analalamikiwa juu ya teuzi anazofanya pasipo kuzingatia sheria
  2. Mtunga sheria kule Dodoma na yeye anachambia kitabu kitakatifu cha nchi
  3. Huyu DC na yeye ameyataka mwenyewe, alitakiwa kwenda na hao askari in advance, uliona wapi msafara wa kiongozi unakosa ulinzi
 
Hapo sijaona kama aliambatana na watu wa Ardhi
Kuna wakati akili lazima itumike hata kama una cheo lakini pia kuwashirikisha ardhi ilikuwa muhimu sana

Mambo mengine hayahitaji ubabe bali hekima
Hawa ndio walipewa madaraka wakaambiwa wataenda kujifunza huko huko kazi zao na haya ndio matokeo
 
Back
Top Bottom