Ombi la Haji Manara kwa Rais wa TFF kuhusu Jerry Muro

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,978
1,781
December 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Club ya SimbaHaji Manara alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe kwa Rais waTFF Jamal Malinzi kumuomba asamehewe afisa habari mwenzake waYanga Jerry Muro ambaye amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.

Kwako Rais wa TFF
Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi
kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini,

kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.
Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,



Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,
Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba,

Tunamiss rikaka zake zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. kwangu Mh Rais nina hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru,
ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.
Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka. Wako
HAJI MANARA
 
Walikuwa wanachekesha sana, nahis amamkumbuka na kiwango chake kinayumba bila Muro kumboost
 
hahahha hawa watu wanajuana wenyewe... Siku ukimskia jerry unaweza sema hawa watu walidhulumiana nini kwani? jerry huwaga anashombo saaana. Ila manara bado Alwatani wa Uswahilini hayupo nyuma nayeye
 
hahaha jery noma sana.naona manara anajaribu kurudisha fadhira kiana kw jery
 
Hali ya Jerry muro sio nzuri sana jamani tff wamsamehe japo waje warijiane tu pale vyurani japo hapo hali nayo ni tete, watu wanapiga miayo tuuu!
 
Back
Top Bottom