Hiyo unayosema "misemo ya kibongo huwa haimake sense" - ni lugha imetumika kwa ufundi, nadhani jamaa anahitaji kupongezwa kwa kutumia "uvaaji wa koti" kufikisha ujumbe wake. mtu akivaa nguo, mfano koti, ambayo tuseme ni several sizes greater, kwanza anakuwa kichekesho. watu hata hawasikilizi anachosema, wanatazama alivyovaa. wakati mwingine watu wa COMEDY wanatumia mbinu hiyo. lakini pia koti kubwa mpaka unaliburuza chini unaweza kulikanyaga na ukaanguka. maana yake umerushiwa jambo ambalo umeshindwa jinsi ya kujibu mapigo vizuri, ukadhurika. hiyo ndio ladha ya lugha. tujivunie lugha yetu ya kiswahili, na tuitumie vizuri kufikisha ujumbe. ndio kukua kwa lugha. ukianza kuidharau kwamba ni "misemo ya kibongo", utapoteza nafasi ya kuiendeleza, labda Kenya wakusaidie kwa faida yao wenyewe.
Nape hakutakiwa kujiingiza kuishambulia CHADEMA. angetakiwa kujipanga vema ili aanzishe kitu na kukimaliza vizuri. mwanasiasa makini harukii mambo wala hakurupuki. anajenga reputation ya kusimamia machache na kuyakamilisha vizuri, badala ya kushika hiki mara kile, na hakuna hata moja unalofanikisha. hiyo ni signature ya JK, na hatumshangai, lakini Nape alitakiwa angalau alete ladha mpya basi.
Na hata kama ni kuishambulia CHADEMA, alitakiwa aende kwa hoja basi, badala ya kufanya personal attacks. yale yale, "simple minds discuss people..." Nape ajipange upya, ajijengee signature ya kwake mwenyewe, na itakayomsaidia na kuleta fresh breath katika CCM, ni signature ya umakini na uhakika