Nape abeba gunia la kokota, atalitua wapi au kumwuzia nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape abeba gunia la kokota, atalitua wapi au kumwuzia nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 22, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Nape Mnauye, Katibu Mwenezi wa CCM

  Na Saed Kubenea
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye sasa amebeba "gunia la kokoto" na hajui mahali pa kulitua. Hadi sasa Nape amejiingiza katika mgongano wa ndani kwa ndani katika chama chake; amepanua wigo wa maadui kwa kuandama anaowaita "watuhumiwa wakuu wa ufisadi;" na anabembea katika malumbano na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Tangu kukabidhiwa wadhifa wa ukatibu mwenezi wa CCM, Nape amekuwa akisisitiza, "…kung'oa mafisadi ndani ya CCM, ni jambo ambalo halina tena mjadala." Amesema, "Kinachosubiriwa sasa ni suala la utekelezaji tu; NEC imetoa siku 90 kwa mafisadi kuondoka" katika chama hicho. Katika hili, Nape alijiapiza kuwa barua za kujulisha mafisadi kuondoka katika chama tayari zimeandaliwa na zitatolewa kabla ya kumalizika Sikukuu ya Pasaka. Hazijatoka.

  Viongozi ambao wametajwa na Nape kuwa wanatakiwa kujiondoa kwenye uongozi au chama ndani ya siku 90 kwa kuwa ni "mafisadi wanaochafua sura ya chama mbele ya jamii," ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge. Wote watatu ni wajumbe wa NEC na wabunge wa Bunge la Muungano. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, "…hakuna mahali popote katika maazimio ya NEC panapotaja siku 90." Alisema, "Kama ni muda basi ni pale mwenyekiti wetu aliposema NEC ijayo. NEC hukutana kila baada ya miezi minne na kwa hiyo kama ni siku, basi ni 120 na siyo 90." Hatua ya Nape ya kutamka kuwapo kwa barua za kufukuza mafisadi ndani ya chama chake au azimio la NEC, lilikuwa kosa la kwanza kisiasa. Hata kama Nape alikuwa ametumwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kusema aliyosema, bado alipaswa kuwa makini na mzigo aliobebeshwa.

  Kwa wanaomfahamu Kikwete tangu alipokuwa Tanga Sekondari, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hadi ikulu, wanajua jinsi alivyo bingwa wa kutumia wenzake na kisha kuwaacha njiani pale maslahi yake yanapoguswa. Hili linathibitishwa na hatua yake ya kuridhia kujiuzulu kwa Edward Lowassa katika wadhifa wake wa waziri mkuu. Lowassa ambaye mwaka 1995 aliandamana na Kikwete kuchukua fomu ya kuwania urais na kufanikisha harakati zake za kuingia ikulu katika uchaguzi wa mwaka 2005, alitoswa huku akiona. Kisa: Kikwete alihofia kile kilichoitwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe "hatukusema yote, ili kuokoa serikali na rais."

  Taarifa zinasema, Kikwete aliamua kuepusha malumbano ambayo yangeweza kumhusisha na ujio wa makampuni tata ya Richmond na Dowans. Si hivyo tu. Kikwete ameridhia kuondoka katika nafasi yake ya uspika, Samwel Sitta ambaye tangu mwaka 1995 walikuwa wote katika kutafuta urais. Ni Sitta aliyemjengea Kikwete msingi wa mbio za urais tokea mwaka 1995 alipokubali kumpeleka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kupata baraka za kugombea urais. Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Sitta alikuwa makamu mwenyekiti wa kundi la mtandao uliomuingiza Kikwete madarakani.

  Lakini bila sababu za msingi zenye kuathiri maslahi ya taifa, Kikwete aliamua kuweka sharti la kutaka spika mwanamke; sharti ambalo lilimuondoa Sitta katika kinyang'anyiro hicho. Wengine ambao walitumiwa na Kikwete na wakaachwa njiani kwa sababu hizohizo au zinazofanana, ni pamoja na Bernard Membe, Amos Makalla na Zakia Meghji. Makala ndiye alikuwa katibu wa mtandao wa Kikwete, huku Meghji akitajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliofanikisha, kwa kiasi kikubwa, kampeni za urais wa Kikwete. Wakati Membe alitumika "kufanikisha mkakati" wa kuwafukuza Rostam, Lowassa na Chenge katika vikao vya maamuzi, Kikwete katika staili yake ya kuuma na kupuliza, aliamua kutopeleka jina lake katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na sekretarieti ya chama. Hata kuondoka kwa Yusuf Makamba na kuingizwa kwa January Makamba, mtoto wake, kumefanywa kwa njia hiyohiyo.

  Hivyo basi, hatua ya Nape ya kujiingiza katika mgongano wa ndani kwa ndani na wenzake ; na kung'ang'ania hoja ya kufukuza wanaoitwa "mafisadi ndani ya chama," inaweza kumgharimu.
  Kikwete anaweza kuamua kumuacha Nape solemba kwa kuwa kibarua alichompa kimemshinda; hawezi kutetea alichoagizwa; hafahamu anachotakiwa kufanya na hajui anachotenda. Kwanza, badala ya kujibu hoza zilizosheni takwimu na uhalisia wa maisha ya kila siku ya wananchi zinazotolewa na CHADEMA, kwa mfano "serikali kufilisika," yeye amejiingiza katika hoja dhaifu ya posho za watendaji wa chama hicho akiwamo katibu mkuu Dk. Willibrod Slaa. Anasema Dk. Slaa analipwa mshahara wa Sh. 7.5 milioni kila mwezi. Anadai kitendo hicho ni sawa na ufisadi. Anamtuhumu kuwa huko nyuma aliwahi kunukuliwa akisema mishahara ya wabunge ipunguzwe kwa kuwa inaangamiza taifa. Nape haishii hapo. Amezungumzia pia kile anachoita "ununuzi wa magari chakavu" yaliyonunuliwa kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Hatua ya Nape kunyooshea kidole CHADEMA, haiwezi kukisaidia chama chake katika mkwamo wa tuhuma dhidi ya ufisadi, badala yake imekizamisha chama chake katika tope.

  Kwa mfano, wakati Nape anasema mshahara wa katibu mkuu wa CCM, ni Sh. 1.5 milioni, ukweli ni kuwa kima cha mshahara kwa watendaji wakuu wa chama hicho, kinategemea mhusika ametokea wapi kabla ya kupewa kazi hiyo. Yusuph Makamba, katibu mkuu aliyeondoka madarakani, alikuwa anatakiwa kulipwa Sh. 1.5 milioni. Huu ni mshahara ambao alikuwa anapata wakati akiwa mkuu wa mkoa. Lakini Makamba aliamua kuachana na mshahara huo kwa kuwa yeye tayari alikuwa mbunge. Alibaki na mshara wake mmoja wa ubunge ambao ni zaidi ya Sh. 7.1 milioni anazolipwa Dk. Slaa. Aidha, katibu mkuu wa CCM anamiliki magari matatu – la kwake, linalotumiwa na wasaidi wake katika msafara wake na lile linalotumiwa na mkewe. Magari yote haya matatu huhudumiwa na CCM.

  Mbali na Makamba kupewa magari matatu, alikuwa analipwa posho ya Sh. 135,000 (laki moja na elfu thelathini na tano) kwa kila siku ambayo anakuwa nje ya Dodoma. Hapa Makamba atakuwa amejichukulia kitita cha zaidi ya Sh. 11.5 milioni kwa mwezi. Kwa kuwa Makamba alikuwa mbunge, aliendelea kunufaika na stahiki zote za mbunge. Alilipwa mafuta – Sh. 2.5 milioni kila mwezi. Alilipwa posho ya dereva – Sh. 400,000 kila mwezi, huku chama chake kikigharamia dereva, mafuta na baadhi ya safari zake zikiwamo zile za nje ya nchi. Hata safari yake ya matibabu nchini India, pamoja na safari za kikazi mkoani Dodoma, zote hizo ziligharamiwa na Bunge na chama chake.

  Ndivyo ilivyokuwa pia kwa Jaka Mwambi aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho. Mwambi alilipwa Sh. 1.5 milioni kwa mwezi kwa kuwa kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa. Baada ya muhula wake wa ubunge kumalizika, ndipo Makamba akaanza kulipwa fedha hizo, lakini alijilipa mamilioni mengine ya shilingi kama posho ya kujikimu.

  Katibu mkuu mpya, Wilson Mukama, kwa kuwa ameacha utumishi akiwa katibu mkuu serikalini, atachota kitita cha Sh. 3.8 milioni; posho ya Sh. 135,000 kwa kila siku asiyokuwapo Dodoma na atakuwa na wasaidizi sita wanaolipwa posho ya kati ya Sh. 30,000 na 55,000 kwa siku. Mukama amekabidhiwa magari matatu yanayohudimiwa na chama chake – mawili yake na moja la mkewe – na atakuwa anaendelea kulipwa stahiki yake ya kiinua mgongo kama katibu mkuu mstaafu.

  Je, Nape alikuwa anafahamu haya kabla ya kuamua kuangamiza chama chake? Anajua kuwa maelezo haya yametosha kuwapa mtaji wa kisiasa wapinzani wake? Kimsingi kabla ya Nape kuzungumza alichokusudia, alipaswa kupima maelezo yake. Alipaswa kuangalia athari zitakazokipata chama chake. Matokeo yake, sasa analazimika kufanya kazi tatu kwa mpigo – kuokoa chama chake, kujiokoa yeye mwenyewe na kuendelea na kibarua cha Kikwete kwa kuhubiri "mwisho wa mafisadi" usiowadia. Badala ya kusisitiza umuhimu wa chama chake kuachana na mafisadi, analazimika sasa kujibu madai yaliyoporomoshwa na CHADEMA na kuthibitishwa na Fred Mpendazoe juu ya ushiriki wake katika kuunda, kusajili na kutumikia Chama cha Jamii (CCJ).

  Badala ya kutumia muda na akili yake kueleza wanachama na viongozi wenzake jinsi chama hicho kilivyodhoofika kisiasa kwa kukumbatia ufisadi na mafisadi, sasa anapaswa kujibu hoja juu ya jinsi alivyonufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia kwa mmoja wa watuhumiwa, Jeetu Petel. Badala ya kujenga chama chake, Nape anapaswa kujielekeza sasa katika tuhuma juu ya usaliti kwa chama chake; na hatua yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo, kupitia CHADEMA.

  Atachoka au tuseme tayari amechoka asubuhi. Amejitwisha vineno asivyoweza kutetea na amekitumbukiza chama chake katika mbio ambazo hawezi kushinda.

  Huyo ndiye Nape Nnauye. Kijana anayedhani anaweza kuokoa CCM kwa kuvurumisha madai dhidi ya upinzani.Waswahili husema aendaye mbio za Nape, amebeba gunia la kokoto. Je, Nape anapeleka wapi gunia hilo? Atamuuzia nani?

  Mwanahalisi
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Atachoka au tuseme tayari amechoka asubuhi. Amejitwisha vineno asivyoweza kutetea na amekitumbukiza chama chake katika mbio ambazo hawezi kushinda.
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umesema mkuu! Kijana anahali ngumu kisiasa,na mzigo mzito wa kujisafisha maana kajipaka matope mwenyewe.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Angetulia kwanza asome upepo unavyokwena na jinsi ya kuhimili kishindo chake, lakini yeye anajiingiza kichwa kichwa, yaliyomshinda Luten Makamba mwanamgambo Nape atayaweza?
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  MPENDA MADARAKA ALITAKA KUHAMIA CHADEMA IKIWA ATAPEWA AGOMBE JIMBO LA UBUNGO..... AKAAMBIWA HANA VIGEZO ZIDII YA DOGO MNYIKA........................ HANA LOLOTE ATAENDA CCJ ... CMM WAKAMPA U-DC, NA SASA U- MC WA CHAMA CHA MAGAMBA(CCM)
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siasa za Chama chake ni ngumu sana maana watu wanalindana na kuwindana. Naye bado ni kijana ana sikunyingi za kuwa kwenye siasa alipaswa kwanza kusoma na kujua nani ni nani kwenye magamba maana kukurupuka na kuwasema akina EL hadharani kuna mweka pabaya na sasa anapambana kutoka kila mahali, Porokwa nae kaingia kwenye game hili Napelape anakazi
   
 7. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Very true. Hii vita inaonyesha kama ni Nape against mafisadi (in short Nape ameachiwa mzigo wote hivyo ni ngumu sana kuji-defend). Ingekua CCM wanania dhabiti yakujivua gamba ingekua CCM against Mafisadi; na ingekuwa easy kwa Nape ku-attack. I believe ana-fight his own war without knowing. Wale wanaomshauri au kumtuma ndio hao hao wana-fight the other side. I can't see how he can succeed without knowing who the real enemy is.
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Asante sana kubenea kwa uchambuzi makini
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mfupa uliomshinda fisi mbwa atauweza?
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Nampa pole mdogo wangu huyu.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sijamsikia Rais Kikwete akitamka au kumnyoshea kidole ye yote kati ya mafisadi wanaotajwa, kwa maana nyingine yeye anaonekana rafiki wa mafisadi katika vikao vyao na kwa upande mwingine anawachonganisha wengine na timu ya mafisadi hatima yake ni kusambaratisha chama.
   
 12. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Bwn Nape akiona mawaidha aya,atalia na kusaga meno. Pole ndugu Nape asiyeipenda cdm ati kwa kuwa ya wachaga,kama ingekuwa ya wahaya basi Nape angekimbilia cdm. Pole nape,ubungu tulikuwa na Kamanda Mnyika,tusingeweza kukupa upeperushe bendera. Ifikapo 2015 mrithi wa nafasi yako ya ccm ya leo ataongoza chama cha upinzan ccm. Pole Nape.
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nadhani nae ameshaona kuwa kazi aliyopewa ni ngumu tofauti na alivyotegemea, maana hajasikika siku hizi mbili...
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mpendazone ametoa tu utangulizi kuhusu waasisi wa CCJ, baada ya hii comma, bora Nape ajaribu kutafakari maana akirukia tena Chadema kwa stile ile, Mpendazone itabidi atoboe siri ambazo Nape alikuwa anavujisha toka CCM kwa ajili ya uanzishwaji wa CCJ, hapo atalia na kusaga meno.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu umejiandaa kwa ban? Maana picha hiyo isije kuwa ni photo shop? Hata ikiwa lakini imependeza tehe tehe Nape una kazi wewe.
   
 16. z

  zamlock JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  si alisema chiligati alikuwa awezi kuzungumza eti alikuwa anajikanyaga eti saizi ccm imeoata mtu wa kujibu hoja tena makini nikamcheka sana
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Sidhani kama hii pic ni photoshop, kuna tokeo fulani kwenye mkutano mkuu wa Chadema, yeye Nape alitumwa kama mwakilishi wa CCM, nadhani ni pic halisi.
   
 18. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyo dogo nape ameshaanza kufyata mkia, mana hana support hata ya katibu wake, yuko mwenyewe tu anaropokaropoka kila siku kwenye rediombao na ma facebook
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Political sayans ni nzuri sana hasa ukitambua maovu ya nyuma ya mpinzani wako! Siasa za tz za leo zinaongwa na wananchi hivyo mwanasiasa mwenye ushawishi kwa jamii ndie mwenye maamuzi ya mwelekeo wa siasa hizo! Nionavyo mm cdm ndio wanaoamua na ndio wenye jibu sahihi la magumu na machungu ya watz!!
  Mnyonge nyongo ikitumbukia hata kwa ubani na unajimu hata kuelewa!!!
   
 20. Tympa

  Tympa Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ukiwa na mawazo finyu/mafupi kwenye ulingo wa siasa, utapotezwa haraka kama nape mnauye.
   
Loading...