Kosea Kujenga nyumba lakini usikosee kuoa

Kosea Kujenga nyumba lakini usikosee kuoa

Smart Finance

Member
Joined
Apr 10, 2025
Posts
35
Reaction score
112
Baada ya kuishi pamoja kwa miaka 16 bila ndoa rasmi, Mkurugenzi wa lebo ya “Cash Money Records”, Birdman (56), na mwimbaji mashuhuri wa RnB, Toni Braxton (57), waliamua kufunga ndoa kimya kimya wiki iliyopita.

Hata hivyo, ndani ya siku 3 tu baada ya ndoa hiyo, Toni Braxton aliwasilisha maombi ya talaka akidai kuwa ndoa hiyo ilifungwa kimakosa kisheria. Kilichovutia zaidi ni madai yake ya kutaka kugawana utajirinusu Kwa nusu, ambao unakadiriwa kuwa dola za Marekani milioni 160 – sawa na zaidi ya TSh bilioni 419.

Hii imeibua mjadala mkubwa kuhusu ulinzi wa mali binafsi katika ndoa, hasa kwa watu wenye utajiri mkubwa. Kesi hii inaonesha umuhimu watu kuingia kwenye ndoa wakiwa na mikataba ya kabla ya ndoa (prenup agreements), ili kuzuia migogoro ya kifedha iwapo mambo yataharibika.

Ni somo muhimu kwa wawekezaji na watu wenye malengo ya kifedha – uhusiano wa kimapenzi haupaswi kufumbiwa macho kwenye mipango ya kifedha. Ulinzi wa investment s zako ni ni sehemu muhimu sana.

Telegram:

Whatsapp:
1744724818118.jpg
 
Back
Top Bottom