Kosa tulilolifanya CCM lisitokee tena, ni fedheha

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
555
1,000
Wadau hasa wale wa Chama chetu cha CCM, tukubali na tuseme ukweli Uchaguzi umeisha,kuna kitu kimoja kimetuharibia Uchaguzi huu na kuwaweka viongozi wakuu katika wakati mgumu, japo tunajikaza kisabuni.

Tukubaliane kuwa uchaguzi wa mwaka huu tumevuruga, kiukweli tumejipanga kimkakati kushinda uchaguzi na tulifanya matayarisho makuu ya kuwa tunaondoka na ushindi mnono, mbinu zetu zimefanikiwa na kweli tumeondoka na kilo nzito ya ushindi haijawahi kutokea,tokea mfumo wa vyama vingi uanze.

Kosa kubwa liliweka dosari ni kushindwa kudhibiti tusitoe kipigo na mbinu zetu kuweza kupita un-noticed,hili ni kosa ambalo kwa hali yeyote itabidi tulirekebishe,mbinu zetu zingeweza kutuvusha bila ya makelele ya milango.

Moja ya kosa ni kupiga watu au tuwaite wananchi au kwa lugha inayoendana na wakati wapiga kura,kuua wapiga kura,kuwacharaza kwa kutumia marungu waya na vitu kama hivyo, Polisi wametuharibia na kututilia doa ushindi wetu wa Tsunami.

Kwa kweli hatukufanikiwa kuupata ushindi huu bila ya kumwaga damu,athari ambayo ameondoka nayo Mkapa mtu aliejutia tendo hilo. Kwa ufupi kilichofanyika Unguja hasa Pemba kimeathiri ushindi wetu ndani ya nchi na hata kimataifa,hivi kulikuwa na haja gani ya kupiga watu au kurusha mabomu ndani ya nyumba kupitia dirishani,Je hawa tuliwatuma kuyafanya yote haya,unatia bomu dirishani ,tulihitaji yote haya ili tushinde?

Wadau tumekosea sana ,ilikuwa hatuna sababu ya kupiga hata bakora mtu mpiga kura yeyote zaidi ya kutumia maji ya washawasha na mabomu ya machozi yanayopigwa nje tena pale inapobidi kuwachawanya wapiga kura sugu, na ukienda kwenye waliopigwa risasi hili ndio jambo ambalo lilikuwa liepukwe kwa hali na mali ili kuisafisha njia ya ushindi, asingekuwepo mtu wa kulalamika zaidi ya kura zimeibiwa,jingine ni lile la kuwatupa wapiga kura tuliowakusanya kama ni waleta fujo, hawa tusingeliwapiga na baada ya uchaguzi tungewashusha chini ya milango ya nyumba zao,tungelisema tu tumewahifadhi kwa ajili ya usalama wao,ingelitosha kuongeza nguvu ya ushindi wetu.

Yaani kama ni kujisafisha ni kuwasaka wahuni waliofanya matendo haya japo halafu tuwaachie kwa mbinu zetu. Wadau uchaguzi ujao asikanyagwe hata mdudu, tupange mikakati yetu tuondoke na ushindi wa karne.
 

uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
5,554
2,000
Mlitumia mbinu za hovyo sana, Halafu mkawa mnaogopa reactions, and you had to use force to maintain!

Kilichotokea sio kosa wala kwa ccm, wala siwalaumu, ukifanya dhuluma na usipogeuka na kutubu, You will be exposed!

Watalaam wanasema Mungu haukumu mtu, ila hukumu yake ameifungamanisha kwenye sheria yake!

That means ukifanya kosa umechagua hukumu yake ambayo ni matokeo ya hilo kosa!

CCM mmetumia fedha zetu kutuazibu, Mungu ninayemjua Mimi hawezi Kuwaacha hata siku moja! Mtaanguka tu!

All the best, you have all what you wanted, so you should be okay by now, fanyeni mnayoona ni sawa kwenu!
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,729
2,000

Bob Marley and The Wailers - Guiltiness

Guiltiness (talkin' 'bout guiltiness)
Pressed on their conscience. Oh yeah.
And they live their lives (they live their lives)
On false pretence everyday -
Each and everyday. Yeah.

These are the big fish
Who always try to eat down the small fish,
Just the small fish.
I tell you what: they would do anything
To materialize their every wish. Oh yeah-eah-eah-eah.

Say: Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sorrow!
Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sad tomorrow!
Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sorrow!
Oh, yeah-eah! Oh, yeah-eah-eah-eah!

Guiltiness
Pressed on their conscience. Oh yeah. Oh yeah.
These are the big fish
Who always try to eat down the small fish,
Just the small fish.

I tell you what: they would do anything
To materialize their every wish. Oh, yeah-eah-eah-eah-eah-eah.

But: Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sorrow!
Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sad tomorrow!
Woe to the downpressors:
They'll eat the bread of sad tomorrow!
Oh, yeah-eah! Oh yeah-e-e-e-e-e!

Guiltiness. Oh yeah. Ah!
They'll eat the bread of sorrow everyday

Source: Musixmatch

Songwriters: Bob Marley

Guiltiness lyrics Cayman Music, Odnil Music Ltd., Fifty Six Hope Road Music Ltd., Blackwell Fuller Music Publishing Llc
 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
3,993
2,000
....Yaani kama ni kujisafisha ni kuwasaka wahuni waliofanya matendo haya japo halafu tuwaachie kwa mbinu zetu.
Duh.. Kama mbwa kafanya uharibifu, unakamata mbwa au mwenye mbwa aliyemtuma mbwa?

Hao wahuni mtawaonea tuu. Waovu na wahalifu halisi ni watumaji
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
2,914
2,000
Hakuna kitu kama hicho.

Ushitwike kofia ya CCM wakati wewe ni Unatokea Ufipa st.

Uchaguzi ulikuwa huru na haki.

#LoserLissu.

#PoleniUpinzani
 

mr.London

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,120
2,000
Kukodi majeshi kutoka burundi jee wakilipwa kila 1 milioni kwa siku.,, na walikuwa wakiwaambia wananchi vituoni sisi tumeletwa kwa moja tu, ukikaidi tunakupiga risasi
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
555
1,000
Kukodi majeshi kutoka burundi jee wakilipwa kila 1 milioni kwa siku.,, na walikuwa wakiwaambia wananchi vituoni sisi tumeletwa kwa moja tu, ukikaidi tunakupiga risasi
Tatizo wapinzani upepo mnashindana na propaganda za uchaguzi.

Kosa kuu tulilolifanya ambalo hatukulitegemea na limetupotezea krediti ni haya matukio,matukio ambayo yalikuwa yasitokee kabisa kabisa,matukio ambayo yangelifuta fingerprints na kuzuia makelele,sasa umeona wapinzani hawa wanaokuja kwa msimu na kukua kama uyoga ,wamepata pa kuparamia na dalili zinaonyesha hili tutalivuka kwani dalili za miti kuteleza kwa upinzani zimeanza kuzaa matunda.

Wadau wa timu ya CCM ya ushindi kama hawa wanaoona miti yote imeanza kuteleza kama watakuwepo basi ,mpja ya mkakati ni kuondoka na ushindi bila ya kukanyagwa mtu ,completely ushindi na binu ziwe ni stealthy kabisa,wabaki wakijiuliza tumeshindwaje,kuliko huku kupata sababu za hapa na pale.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom