Kosa linalopuuzwa na Rais

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
KOSA LINALOPUUZWA NA RAIS

Na, Robert Heriel

Dunia itakuwa salama endapo wanawake watafundishwa adabu. TUtawafundisha kuwaheshimu waume zao na kuwatii. Mara nyingi nimekuwa nikiongea na kuwa na msimamo huu ambao watu wengine wanaonisikiliza wamekuwa wakiniona kama mtu ninayependa mfumo dume. Si vibaya kunifikiria hivyo na si lengo langu kukushawishi kuwa na msimamo kama wangu. Ila Wanaume thabiti bila shaka wananielewa, Watu wacha Mungu wananielewa, Wanafalsafa na wenye akili za kuona mbali wananielewa,

Mwanamke lazima afundishwe adabu ili akamilike. kutomfundisha mwanamke heshima na adabu ni jambo hatari kwa usalama wa jamii husika na ulimwengu kwa ujumla.

kwa nini naamini kuwa mwanamke lazima afundishwe heshima, adabu na utii. Ni kutokana na hoja zifuatazo;-

1. Kuokoa Maadili ya kizazi/vizazi vijavyo.
Jukumu la malezi kwa kiiasi kikubwa ni la Mama. Mama ndiye mwenye jukumu hili kwa asilimia kubwa. Mama ndiye huweza kuathiri maadili ya mtoto kwa kiasi kikubwa. Mama ndiye huamua fikra za mtoto wake ziweje juu ya Baba yake na watu wengine. Hii ni kutokana na ukaribu wa mtoto na Mama yake. Endapo mama atakuwa hana maadili basi kuna uwezekano mkubwa mtoto akachukua tabia za mama yake. Tabia za watoto wa siku hizi si matokeo ya bahati mbaya. Bali matokeo ya kutowafundisha wanawake heshima na utii. Wanawake wa siku kumtukana mwanaume bila kujali ni mume wake hawaoni tabu. Wengine husema pasipo na mipaka wakiita hiyo ndio haki na demokrasia. Jambo hili limeenda hata kwa watoto na vijana ambao siku hizi hutukana bila akili. Usijiulize uwezo wa vijana wa siku hizi kumtukana mtu kama Rais wa nchi hii umetoka wapi. Chanzo kimoja wapo ni hichi.

2. Kuzalisha vijana wachapakazi
Utakuja kuona kuwa mwanamke asipokuwa na adabu, heshima, ana utii huweza kusababisha vijana wa jamii husika kuwa walegevu. Ikiwa jamii inawanawake wasio na adabu ni rahisii kujua vijana walivyo wavivu. Mama asiye na adabu hawezi kuwahamasisha watoto wake kufanya kazi. Mara nyingi huwadekeza watoto na kuwafanya wawe legelege. Hata mtoto wake akiadhibiwa na mtu mwingine kwa kufanya kosa fulani basi utasikia kelele zake mpaka kesi kwenye serikali za mitaa. Mke mwema na mwenye adabu huwa mchapaka kazi hivyo huzaa watoto wachapakazi. Mwanamke mwenye adabu hapendi njia za mkato hivyo atazaa watoto wasiopenda njia za mikato. Lakini kwa bahati mbaya zama hizi wanawake waliowengi hupenda njia za mikato, hutegemea vitu vya bure hivyo usishangae kuona vijana nao wakipenda njia hizo hizo kama walivyolelewa.
kumbuka; jukumu kubwa la mwanamke ni kulea na kufundisha watoto utii, heshima na adabu. Baba itokee kwa dharura tuu ikiwa ataona mama anamapungufu.

3. Kwa Amani na usalama wa nchi yetu.
kumfundisha nwanamke adabu ni kulinda amani ya nchi. Ni kuiweka nchi yetu salama. ikiwa watoto hawajafunzwa kumuheshimu Baba ndani ya nyumba unafikiri watamheshimu nani kwenye jamii? Ndio maana vijana siku hizi hawaoni tabu kumtukana Rais wa nchi yao matusi ya nguoni.
Rais utajihangaisha sana kupambana na vijana badala ya kupambana na wenye jukumu la kuwapa malezi. Yaani maana yake unapambana na tatizo badala chanzo cha tatizo. Lazima ujue kuwa chanzo cha haya yote ni wanawake wasio na adabu.

4. Kuokoa na kurudisha heshima ya taasisi ya ndoa.
Ndoa ni moja ya mambo muhimu katika jamii na nchi kwa ujumla. Katika ndoa humo ndipo familia hutokea. Zamani wanawake walifunzwa adabu na utii pindi waolewapo. Si kwamba ili wanaume wawatawale bali kulinda jamii husika kimaadili na kiuchumi. Wanawake walifundishwa kuwaheshimu watu wa kiume bila kujali umri. Walifundishwa uchapakazi na tabia njema kwani ndio nguzo kubwa ya ndoa. Lakini siku hizi kwa vile serikali imekuwa dhaifu ndio maana hata ndoa zinafunjika kipumbavu pumbavu tuu. Kuishi na mwanamke asiye na adabu ni upumbavu wa hali ya juu. Ni sawa na kuishi na shetani nyumba moja.

serikali lazima iliangalie hili kwani linaathari kubwa katika jamii. Ndoa siku hizi hazina thamani tena. Wanawake hawafundishwi kama zamani. Na wakati mwingine serikali inaywatetea bila akili kubwa yaani bila kufikiri. Hivi unadhani wazee wa zamani kwa jamii zote yaani kuanzia ulaya, Asia, AMerika na hapa kwetu Afrika, unafikiri hawakuwa na akili mpaka wawabane hawa Mama zetu, dada zetu, wake zetu, bibi na shangazi zetu.

Kosa kubwa linalofanywa na dunia ni kuwapa dunia ni kuwaachia wanawake kiholela hollela. Kuwafanya wajione wapo sawa na wanaume ni kuhatarisha usalama wa dunia.

Ni kuwafanya wanaume wawe wanawake. Usishangae kuona mashoga, usishangae kuona wanaume wanaopenda vitu vya bure bila kufanya kazi, usishangae kuona wanaume wanaojipodoa tadhani wari. Hizi ni athari zilitetwazo na kutowafundisha mama zao adabu na heshima.

Mwanamke akiwa hana adabu humfanya mwanaume kuwa kiumbe duni. Hufanya dunia kuwa na maasi mengi.

Dunia itakuwa salama ikiwa wanawake watadhibitiwa kikamilifu. Yaani watafunzwa adabu na wanaume waliokamilika wenye nafasi kubwa serikalini.

Hilo ndilo kosa kubwa linalofanywa na Maraisi wa Tanzania ambalo ni mwiba kwa miaka ijayo. Wenye macho wanaweza kuona. Wenye akili watatafakari, wenye ufahamu wataelewa.

Niite Taikon wa Fasihi.

 
Hivi unasemaje wewe?

Zaa wanao au dada zako na mama yako uwafundishe hiyo adabu unayoosemea hapa,

Tuendako huwezi kumfanya mwanamke rimoti km mliweza zamani

By the way kajambe mbele huko,


Ndio ninyi tunaowazungumzia. watu msio na adabu. mtendao pasipo kufikiri. Unawezaje kutumia lugha kama hiyo kwa mtu usiye mjua
 
Ndio ninyi tunaowazungumzia. watu msio na adabu. mtendao pasipo kufikiri. Unawezaje kutumia lugha kama hiyo kwa mtu usiye mjua
Nasema ungaliwahi kuzaliwa miaka hiyo ya akina Yesu na Muhammad huenda mawazo yako yangechukua hatam,

Pamoja na kuoneka kituko ni upuuzi kuzungumzia hili, tena eti unamshairi rais?

Labda nikufunze weye adabu kwa kutoheshimu wengine,

Narudia tena km mliweza hapo mwanzo kwa Leo usahau,
 
Nasema ungaliwahi kuzaliwa miaka hiyo ya akina Yesu na Muhammad huenda mawazo yako yangechukua hatam,

Pamoja na kuoneka kituko ni upuuzi kuzungumzia hili, tena eti unamshairi rais?

Labda nikufunze weye adabu kwa kutoheshimu wengine,

Narudia tena km mliweza hapo mwanzo kwa Leo usahau,


hata sasa bado tunawamudu, hamjawa kikwazo kwa jamii ya zama hizi. Tahadhari ni kwa vizazi vitatu vijavyo. Kwa sasa athari bado ni ndogo. Hivyo usijitape hapo.
 
Ulianza vizuri Sana , sema umeharibu mwishoni kuhusianisha siasa na malezi, mkuu kwenye siasa tunajenga hoja tu na hta kma ni baba yako unampinga tu
 
Unatoka mzima akili zako umesoma mpaka chuo kikuu na kazi yako nzuri, unaanza kupakuliwa nyuma na wanaume wenzako, ukiwa na akili zako timamu. Then mama yako alaumiwe kwa kipi... Adabu hamna nyie wenyewe wanaume mjirekebishe
 
Ulianza vizuri Sana , sema umeharibu mwishoni kuhusianisha siasa na malezi, mkuu kwenye siasa tunajenga hoja tu na hta kma ni baba yako unampinga tu


Baba hapingwi abadani. Labda kwa watoto wasiojua nini maana ya Baba. Watoto waliokosa malezi stahiki.
Huwezi elewa hii bila kufikiri mkuu
 
Back
Top Bottom