AL SADY OLPLANER
JF-Expert Member
- Nov 21, 2016
- 294
- 211
KWELI TENDA WEMA NENDA ZAKO .....USISUBIRI SHUKURANII.
Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.
Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.
Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.
Badae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake 'chongo' anayemtia aibu.
Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.
Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.
Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..
Mtoto kwa hasira akamuuliza "mama umekuja kufanya nini hapa? Kama una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako"
Mama yake akasema "samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe". Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.
Baada ya siku chache kupita, yule mtoto akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.
Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.
Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hivi...
"Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee... Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.
Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa nami....
Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongo....
Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu,ukiwa bado mchanga tulivamiwa na majambazi katika harakati za kupambana nao walikuchukuwa wewe nia na madhumuni yao ilikuwa wanataka kukuua lkn nilipambana kama mwanamke shupavu nikafanikiwa kupambana nao japokuwa walifanikiwa kumuua baba yako.Mimi walinichoma na kitu chenye ncha Kali jichoni ili nisiweze kuwatambua lkn nilifanikiwa nikawaua wote,na ndio ikawa chanzo cha hiii chongo,mwanangu mpendwa pasipokuchukuliwa wewe chongo hiii nisingekuwa nayo.nilipata chongo ili niokoe maisha yako Leo chongo hii imenifanya kiwe chanzo cha kifo changu .kweli tenda wema uendezako mungu akusamehe bure .
Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kupoteza jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care for everything
Akupendaye,
Mama"
Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.