Hawa jamaa kweli wamedhamiria kuinyoosha nchi.
Ni zaidi ya mara tatu nimeshuhudia aina hii ya utumbuaji wa viongozi!
Nilianza zengwe la hivi kule Songwe kwa Chiku Galawa, akaja Kamishina wa Tra, sasa na huyu!
Unaonywa hadharani ili ujirekebishe juu ya utendaji wako wenye mapungufu, kumbe huku memo za kukutumbulia zikiendelea kutembezwa chini ya meza!
Nilichokigundua kwa hao viongozi ni kwamba, ukiona ziara ya mkubwa imekubadikikia, upepo umevurugika, aidha hata kwa watendaji wako wanaokuwajibikia, usijione 'umesevu' ukaanza kujipendekeza kwa maneno ya kimbelembele, kama alivyofanya Mchechu wa NHC kule dodoma kwa kumwita Jpm 'baba' badala ya 'mheshimwa' utakuwa unajidhalilisha tu.
Yakikutokea hayo nuna kabisa, usicheke na mtu, wala kujipendekeza kwa maneno ama kwa vitendo.
Jiandae kupokea walichokipanga kukufanyia.
Kufanya chochote hakibadilishi maamuzi, maana utakuwa umeshachelewa.