Korti yamwachia mtoto wa Keenja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korti yamwachia mtoto wa Keenja

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Oct 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,740
  Trophy Points: 280
  USIOMBE YAKUKUTE WE KAPUKU
  SEGEDANC YAKO

  Korti yamwachia mtoto wa Keenja

  na Happiness Katabazi

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilimwachiria huru mtoto wa mbunge wa Jimbo la Ubungo, Charles Keenja, Eliasa Keenja, na wenzake watatu baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

  Mbali na Keenja washtakiwa wengine waliofutiwa kesi ni Ahmed Mbilinga (Meneja wa NHC, Mkoa wa Tabora), Frola Nhamkolomwa na Damas Ngoiya ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 300.

  Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, alisema amefikia hatua ya kuwaachiria huru washtakiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu.

  Alisema ushahidi uliotolewa hauwezi kuwatia hatiani kwa kuwa hauonyeshi kama kweli washtakiwa hao walivunja nyumba ya mpangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Li Jinglan, na kuiba vitu hivyo.

  Awali, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Mei 9, 2006, katika eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, waliingia kwenye nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) anamoishi, Li Jinglan, na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 300.
   
 2. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Ningependa kumpongeza Eliasa Keenja kwa kuachiwa huru na mahakama katika kesi hiyo,kwa ajili ilikosa ushahidi.
  Nafurahi sana ninaposikia mtoto wa Mbunge Keenja akiachiwa huru,kwa sababu Mbunge Keenja ndiye aliyejenga barabara hizo nzuri za Dar es Salaam,[jambo ambalo lilitufanya wengi tusiamini macho yetu,yaani,uzuri wa barabara],lakini Keenja angegombea Ubunge Mbagala,asingeshinda,kwa sababu barabara zake hazikufika Mbagala.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,740
  Trophy Points: 280
  Nafurahi sana ninaposikia mtoto wa Mbunge Keenja akiachiwa huru,kwa sababu Mbunge Keenja ndiye aliyejenga barabara hizo nzuri za Dar es Salaam,[jambo ambalo lilitufanya wengi tusiamini macho yetu,yaani,uzuri wa barabara],lakini Keenja angegombea Ubunge Mbagala,asingeshinda,kwa sababu barabara zake hazikufika Mbagala.


  NI HATARI PALE UNAPOAMUA KUTEMBEA UCHI UNAKUTA NA MKWEO...USIOMBE HILO
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  what kind of thinking is this?
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,740
  Trophy Points: 280
  what kind of thinking is this?

  KIGOGO USSIMLAUMU KWANZA INATEGEMEA NA SHULE ALIPOSOMA@@#
   
 6. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Ana Hisa mwenzio! hahahahahah! lazima ameahidiwa bonge nono...
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asante sana umetuliza hasira zangu..yaani watu wengine wana thinking ya ajabu kabisa
   
 8. k

  kulumbembe New Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaazikwerikweri!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hakika pongezi hizi nzito si bila sababu .Tutacgunguza tujue
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Keenja ana barabara "zake"?
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, sijui angewezaje kufanya kila kitu kwa miaka miwili na nusu tu. Alijitahidi kibinadamu.
   
Loading...