Korea Kaskazini yarusha kombora katika bahari ya Japan

Korea Kaskazini yarusha kombora katika bahari ya Japan

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
686
Reaction score
589
Korea Kaskazini yarusha kombora katika bahari ya Japan

_96793813_northkoreamissile4.jpg

Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
​
⦁ Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
⦁ Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la Korea kusini.
⦁ Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan.
⦁ Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika meizi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.

Kombora hilo la siku ya Jumanne lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40,kulingana na Korea Kusini na Japan.

Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu lakini urefu wake umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul Stephens Evans.

Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei.
Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.

Waziri anayesimamia maswala ya serikali nchini humo Yoshihide Suga aliambia maripota:Uchokozi kama huu wa Korea kaskazini hauwezi kukubalika.Tuliwasilisha malalamishi yetu na kushutumu hatua hiyo.

Rais mpya wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi majuzi ametaka kufanywa kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la taifa hilo.

Bwana Moon pia alikutana na rais Trump wiki iliopita, huku kiongozi huyo wa Marekani akiionya Pyongyang kwamba itapata jibu sahihi.

Kurushwa kwa kombora hilo kunajiri siku moja baada rais Donald Trump kuzungumza katika simu na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na rais wa China Xi Jinping kuhusu Korea Kaskazini.

Viongozi hao walithibitisha jitihada zao za kuhakikisha kuwa hakuna utumizi wa nyuklia katika rais ya Korea.
=============

Hawa jamaa wanatumiwa na nchi nyingine kuchokoza au ni mazoezi kweli ya makombora yao!! Mbona China na Urusi wako kimya au timu moja!! Haka kajamaa kiburi kweli Trump anasemea mbali mbali tu alifika akapaki meli yake halafu akaondoka kimya kimya..
 
North korea anaamini kua ukimfuatilia kila Mbwa anayekubwekea utachelewa safari yako,
Yeye anatizama mbele tu hajali kelele za watu ambao wanataka wao tu ndio wajilimbikizie silaha kali na wenzao wasiwe na silaha ili wao waendelee kuwatawala wenzao kiurahisi tu.
 
North Korea hajamchokoza mtu yeye anafanyia mjaribio silaha zake.
Anayejifanya kukerwa na kitendo hicho aingie msituni kama atauweza mziki
Amevuka mipaka kwa kutuma kombola lililoangukia katika zone ya Japan.. Sasa huo si uchokozi.
 
[QUOTeverKING, post: 22020768, member: 223391"]Ni miaka mingapi sasa huyo mmarekani anaishia kupiga kelele tuu?

Mtu mzima hatishiwi nyau.[/QUOTE]
Hata Saddam mlikua mnamwambiaga vivyohivyo akabwetika na sifa za plastic akajikuta jandoni
 
Kwa silaha zipi?
Au unaziamini hizi anazozijabu?
Atapata shambulizi la kushtukiza ataamkia aheraaaa!
Kama huziamini za north Korea unaziamini zipi?
Na kama hazina madhara kwann kila kukicha huyo shoga wenu Trump na washirika wake wanalialia kila siku?

Wabongo mnashangaza sana USA na ubabe wake ameukubali mziki wa n.Korea na anaugwaya lakn chaajabu nyinyi wa sikonge na chanika mnabisha bisha tu
 
Back
Top Bottom