Korea Kaskazini yafichua ushahidi wa kwanza wa silaha za kinyuklia

HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
313
Korea Kaskazini imezindua vichwa vidogo vya nyuklia ambavyo imesema vinaweza kuwekwa kwenye makombora ya masafa mafupi.

Korea Kaskazini kwa muda mrefu imekuwa ikidai kuwa na silaha za nyuklia zenye uwezo wa kulenga shabaha nchini.

e83a53f0-cd5e-11ed-be2e-754a65c11505.jpg
i Korea Kusini.
Lakini picha ilizochapisha katika gazeti lake rasmi siku ya Jumanne ndizo za kwanza kutoa ushahidi wa hili.
Hata hivyo, haiwezekani kuthibitisha ikiwa hizi ndizo silaha zilizokusudiwa, hadi Korea Kaskazini itakapojaribu moja.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, Pyongyang imezindua msururu wa kile inachosema ni silaha za nyuklia, huku ikiiga mashambulizi ya nyuklia huko Seoul.

Ukweli ni kwamba ni vigumu kufuatilia mkondo wa makombora ya Korea Kaskazini siku hizi.

Kujaribu pekee hakutoshi tena kutengeneza vichwa vya habari kama ilivyokuwa zamani, lakini tukiangalia kuna mengi tunaweza kujifunza.

Korea Kaskazini inasema inaziadhibu Marekani na Korea Kusini kwa kufanya mazoezi yao makubwa zaidi ya kijeshi kwa miaka mingi.

Washirika hao wawili (Marekani na Korea Kusini) walipata mafunzo ya jinsi ya kuishinda Korea Kaskazini iwapo kutatokea shambulizi.

Ni hali ambayo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hakupenda.

Siku za nyuma, Korea Kaskazini ilijibu mazoezi hayo ya kijeshi kwa kurusha mchanganyiko wa makombora mafupi, ya kati na ya masafa marefu, na inaweza kuongeza makombora kadhaa kwa hiyo.

Wakati huu, Pyongyang ilizindua, kwa muda wa wiki mbili, kombora lake lenye nguvu zaidi linalovuka mabara jingine, ambalo kinadharia linaweza kufika sehemu yoyote kwenye ardhi ya Marekani.

Korea Kaskazini ilirusha makombora kutoka kwa manowari na kile kilichoonekana kuwa jukwaa la chini ya ardhi.
Jeshi la Korea Kaskazini pia liliiga shambulio la nyuklia kwenye uwanja wa ndege wa Korea Kusini.

Kim Jong-un pia alifichua ndege mpya isiyo na rubani ya chini ya maji, akidai kwamba ndege hii inaweza kutumika kama silaha ya nyuklia chini ya maji inayoweza kusababisha tsunami kubwa ya mionzi ambayo inaweza kuharibu meli za adui.

Zaidi ya hayo, Korea Kaskazini sasa inafichua vichwa vya nyuklia ambavyo inadai vinaweza kuwekwa kwenye silaha hizo.

Utaratibu huu wa matukio nchini Korea Kaskazini unatia wasiwasi.

Elaine Kim, mtaalam katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, anasema Korea Kaskazini inaichukulia kama "maonyesho ya mtindo" - rejeleo ya koti la Dior lililovaliwa na binti wa kiongozi wa Korea Kaskazini wakati akihudhuria majaribio ya silaha.

Wachambuzi, akiwemo Elaine Kim, wanaelezea wasiwasi wao kuhusu aina mbalimbali za silaha ambazo Pyongyang imeonyesha msimu huu.

Pyongyang ilifichua silaha mpya na za hali ya juu zaidi ambazo zinaweza kurushwa kutoka nchi kavu na baharini, zikilenga shabaha nchini Marekani, Korea Kusini na Japan.

"Hapo awali, hatukujua wanaweza kurusha makombora kutoka kwa nyambizi, au kutoka kwa majukwaa ya chinichini," anasema Ellen Kim. "Ni silaha ambazo zinazidi kuwa ngumu kuzifuatilia na kuzinasa," Bi. Kim alisema.

bccff750-cd5a-11ed-be2e-754a65c11505.jpg

Hii inaibua tishio la nyuklia linaloletwa na Korea Kaskazini.

Chukua, kwa mfano, makombora ya umbali mrefu ambayo Pyongyang ilirusha kutoka kwa manowari.
Makombora haya ndiyo yanayotia wasiwasi zaidi, anasema Yang Yuke, mtaalam wa silaha katika Taasisi ya Asan huko Seoul, kwa sababu aina hii ya kombora la chini ya maji ni vigumu kugundua mapema kabla ya kuanza shambulio.

Na baada ya kurushwa, makombora haya huruka katika miinuko ya chini ambapo yanaweza kubadilishwa katikati na kutatiza mfumo wa ulinzi wa kombora.

Kim Jong Un amekuwa akihofia kwamba Marekani itashambulia nchi yake kwanza, na kumaliza silaha zake kabla hajapata nafasi ya kuzitumia.

Ujumbe anaoonekana kutuma na safu hii ya majaribio, ni kwamba Kaskazini sasa ina uwezo wa kujibu au hata kuanza shambulizi.

Ni vigumu kuharibu silaha zilizofichwa chini ya ardhi au chini ya maji.

Au, kwa maneno mengine, kiongozi wa Korea Kaskazini anataka kusema: "Usifikiri hata kutushambulia."
Hata hivyo, tunapaswa kuwa waangalifu. Bw Kim ana tabia ya kuzidisha uwezo wake wa kijeshi.

Swali lililopo siku zote limekuwa ikiwa Korea Kaskazini kweli ina vichwa vya nyuklia vya kuvishikamana kwenye makombora haya.

Hadi sasa, hatujaona ushahidi kwamba Pyongyang imeweza kuziendeleza.

Siku ya Jumanne, ilitoa ushahidi wa kwanza. Picha zilizochapishwa katika gazeti kuu la serikali zinaonyesha Kim Jong Un akikagua safu ya kile ilisema ni vichwa vidogo vya nyuklia.

Hakuna njia ya kuthibitisha vichwa hivyo vya nyuklia ndivyo wanavyozungumzia.

Hii ndiyo sababu jumuiya ya ujasusi imekuwa ikinyamaza kwa muda mrefu, ikingojea jaribio hilo la nyuklia.
Wakati ambapo Korea Kaskazini ina uwezo wa kutengeneza vichwa vidogo vya nyuklia kwa kiwango kikubwa, ndio wakati ambapo vitisho vyake vilivyoigizwa vinakuwa vya kweli, na inaweza kushambulia Korea Kusini na Japan kwa silaha za nyuklia.

Kuna baadhi ya wanaohoji kuwa Marekani na jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya zaidi ili kurejesha Korea Kaskazini kwenye meza ya mazungumzo, kuzuia jaribio hili la nyuklia.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekwama kwa zaidi ya miaka minne.

Lakini Pyongyang haijaonyesha dalili yoyote ya kutaka kuzungumza.

Inaelekea kuchagua wakati ambapo inafikiri itakuwa wa faida kubwa upande wao.

Huku China na Urusi zikikataa kuiadhibu Korea Kaskazini katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inaweza kuendelea kutengeneza silaha zake bila matokeo yoyote. Kwa nini iache sasa? Kadiri silaha zake zilivyo bora, ndivyo inavyokuwa na nguvu zaidi, na bado ina zaidi ya kuthibitisha.

Kando na vichwa vidogo vya nyuklia, bado haijaonyesha kuwa vichwa vyake vya kawaida vya nyuklia vinaweza kustahimili umbali wa mabara.

Hivi sasa, Kaskazini inajaribu makombora ya masafa marefu kwa kurusha juu angani.

Pia inataka kuunda ICBM ya kisasa zaidi, ambayo haihitaji kutiwa fyueli kabla ya kuzinduliwa, na hivyo inaweza kurushwa kwa onyo kidogo.

Yang Uk anaamini Kim Jong Un pia anasukumwa na hali ya kukata tamaa nyumbani.

Akiwa na uchumi unaodorora, na watu wake wakiwa na njaa, mpango wake wa kuendeleza silaha za nyuklia ndio "kadi pekee ambayo amebakisha kucheza", Yang anasema.

Kwa hivyo Korea Kaskazini inaonekana kuwa iko tayari kusonga mbele, kutengeneza silaha mbalimbali za kisasa zaidi.

Kwa Ellen Kim, jambo moja tu ni hakika: "Majaribio zaidi yatashuhudiwa."

chanzo cha habari bbc swahili.

picha kwa msaada wa shirika la habari la korea kaskazini KCNA.

Nami ni Hery Hernho
 
Back
Top Bottom